waliojiajiri maarufu kama Boda Boda wanauliwa Kinyama Jijini

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
ni jambo la kusikitisha sana kuona vijana wetu baada ya kuamua kujiajiri kwa kukopa pikipiki au kukodi na kujipatia ajira siku hizi ajira yao imekuwa chungu sana hata kupelekea kuuliwa kinyama na watu wenye tamaa ya kupata utajiri haraka kwa kuziuza bei ya kutupwa yaani mtu anauliwa kwa sh. laki nane au saba,

polisi wako kimya kwa nini kusianzishe ukaguzi nci nzima kuna watu wanatumia chasis no kufany boda boda hii sio fair, jan waliua kijana wa bunju pale mpiji darajani na kumtupa kisa pikipiki
 
Hakika inasikitisha, uchochoroni wanachinjwa saana. Nimeyashuhudia maeneo ya Kitunda, kinyerezi mh!!
 
nasikia masaki nako kuna mtaa unaitwa uganda avenue nao unatumika saana kuwapora boda boda vijana . jamaa yangu anakaa mitaa hiyo anadema watu wanakodiwa toka sehemu nyingine mpaka masaki kwa dau kubwa usiku jamaa akifika hapo anaomba ashushwe mara kundi la watu linatokea wanamkaba dereva wananyang'anya pikipiki
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom