Waliojenga nyumba hupenda kuwaogopesha wengine kuwa ujenzi ni gharama!

Nimejaribu kufuatilia kauli za waliojenga nyumba. Huwa wanapenda kuwaogopesha waliopanga kuwa ujenzi ni gharama.

Huwezi kutana na mtu akakutia moyo hata kidogo. Lengo la wengi waliojenga ni ku play god. Yani wanapenda waheshimike na kujionesha kuwa wana mawe marefu.

Mimi ninapopiga gharama za ujenzi, napata gharama za chini kama ambavyo Magufuli alifanya kwenye ujenzi wa hostel za UD. Tukienda kwa stail yake, mbona kila mtu atakuwa na ka mjengo!
Kweli mkuu
 
Labda niombe mwenye uzoefu anipigie hesabu rough, nyumba ya vyumba 4, sebule na jiko inakula tofali za kuchoma ngapi, bati za kawaida ngapi na simenti+ ufundi
 
Kwa uzoefu ua nashangaa watu wanaodai ukiwa na m20 nyumba ndo inakamilika!! Nyumba hata milioni 5 ipo sema unatka nyumba yenye nakshi zipi za gharama kiasi gani!! Kuna my class mate kamaliza kwa badget ya 16 milion but the quality of it unaezansema ni 50 milion!! Lakini itategemea unajenga wapi
Hakuna quality yoyote kwa 16 mln,sema nyumba hiyo Ina ukubwa gani na weka quantities na quality ya materials hapa tuone ,au kiwanda Cha kila kitu anachoyeye?
 
Mim najenga nyumba ya vyumba viwil sebule sitting room dining pamoja na jiko nimefikia hatua ya KUEZEKA ila bado sijazidi milioni kumi na tano na Mbao nshanunua pamoja na bati sitegemei nyumba izid m25 sasa izo gharama kubwa zipo wapi wasiwatishe bana wewe anza kujenga sema usiwe na haraka sana maana nyumba unakua unazika pesa waweza jikuta unadownfall bila hata kumaliza ujenzi unabaki kuona pagale tu bila kujua hatima ya hilo pagale
Sasa wewe kwa gharama hiyo afu kwa nyumba ya bedroom 2 huoni umeingiliwa,kwamba with the same cost ungeweza kujenga ya vyumba 3 ,unit cost ingekuwa ndogo
 
we umenena,mi nimejenga hata m7 haijafika na nikitaka kuhamia nahamiaaa nnitamalizia nikiwa humuhumu
 
Back
Top Bottom