Waliojenga nyumba hupenda kuwaogopesha wengine kuwa ujenzi ni gharama!

Usiogope mkuu ujenzi ni mpango WA muda utakaoupangilia wewe (hapa hela za pembeni hazihusiki! Mm nimejenga nyumba for just 72.5m. Kwa miaka mitatu to! Ni mipango tu ya saraly yako Hakuna uchawi hapa! Jenga nyumba kwa percentage yako ya mshahara mm nilikuwa nikiweka 30%ya salary jenga kwa kiwango cha kipato chako! Si kujenga kwa kujifanananisha na Fulani, hata ukijenga miaka kumi Nani WA kukuuliza!
Kwahiyo umetumia miezi 36 kwenye ujenzi,
Na ambapo kila mwezi ulikuwa unatumia 2000000 ambayo ni asilimia 30% ya mshahara wako, hivyo mshahara wako utakuwa ni 7000000...
(sijui kama nipo sahihi)
 
Nimejaribu kufuatilia kauli za waliojenga nyumba. Huwa wanapenda kuwaogopesha waliopanga kuwa ujenzi ni gharama.

Huwezi kutana na mtu akakutia moyo hata kidogo. Lengo la wengi waliojenga ni ku play god. Yani wanapenda waheshimike na kujionesha kuwa wana mawe marefu.

Mimi ninapopiga gharama za ujenzi, napata gharama za chini kama ambavyo Magufuli alifanya kwenye ujenzi wa hostel za UD. Tukienda kwa stail yake, mbona kila mtu atakuwa na ka mjengo!
Kama ni rahisi sasa mkuu mbona hujajenga?Anyway,mimi nimejenga nyumba wala sio moja na kiukweli nataka ujenge.Ila siwezi kukuficha.Ujenzi unahitaji kujinyima,uvumilivu na fedha,labda kama wewe ni mzee wa shortcuts(ngada,madili au fisadi).
 
Nimejaribu kufuatilia kauli za waliojenga nyumba. Huwa wanapenda kuwaogopesha waliopanga kuwa ujenzi ni gharama.

Huwezi kutana na mtu akakutia moyo hata kidogo. Lengo la wengi waliojenga ni ku play god. Yani wanapenda waheshimike na kujionesha kuwa wana mawe marefu.

Mimi ninapopiga gharama za ujenzi, napata gharama za chini kama ambavyo Magufuli alifanya kwenye ujenzi wa hostel za UD. Tukienda kwa stail yake, mbona kila mtu atakuwa na ka mjengo!
Sio kweli, mbona mimi huwatia moyo sana?
Ujenzi ni rahisi mno hasa ukiwa na kiwanja. Ukiwa hata na 300,000 inafanya kazi, unajenga kwa awamu sawa na nguvu yako hatimaye unaingia kwako.
Watu wasiogope kujenga
 
Kwa uzoefu ua nashangaa watu wanaodai ukiwa na m20 nyumba ndo inakamilika!! Nyumba hata milioni 5 ipo sema unatka nyumba yenye nakshi zipi za gharama kiasi gani!! Kuna my class mate kamaliza kwa badget ya 16 milion but the quality of it unaezansema ni 50 milion!! Lakini itategemea unajenga wapi

Hiyo ni gharama ya msingi na ukuta tu mkuu
 
Siyo nyumba peke yake, chochote binadamu anachofanya hupenda kujikweza nacho, na kuwakatisha wengine tamaa...

cc: mahondaw
 
Tatizo vijana wanapiga pesa za fastafasta alafu hapo hapo wanataka kununua kiwanja na kujenga, kwanini usione ujenzi ni ghali?

Ukipata hela yako tulia kama huna kitu then tafuta taarifa sahihi kwa unachotaka kukijenga, onana na mafundi wa kila aina yaani wale wa mtaani na wale waliokwenda shule, usiache kuwasikiliza watu ambao wameshajenga pia.

Zunguka kujua bei za material na bei zake, pia usiache kutafuta mbadala wa material kwa mfano badala ya kuweka matofali kwenye msingi uweke mawe kutokana na urahisi/upatikanaji wake.

Usishindane na wenzako ambao wameshajenga, kuwa mvumilivu, jenga kwa hatua, usijidai boss!

Usisahau kubariki eneo lako la ujenzi kabla maana sehemu nyingine ni makao ya Ibilisi au yamezindikwa huwezi kujua.

Mtangulize Mungu.

Ushauri wako huu ndio ambao nimekuwa naufanyia kazi. Sasa mimi nafanya tu survey ya maeneo yanayofaa kwa mimi kujenga, huku nikifuatilia gharama ya ujenzi na alternatives.

Mfano kuna jamaa mmoja aliniambia yeye amejenga nyumba yake kwa kutumia mafundi aliowatoa kijijini, hii yote ilikuwa ni kuepuka mafundi wa mjini ambao ujanja ni mwingi ukichanganyikana na wizi. Nyumba imejengwa vizuri utadhani hao mafundi wana degree za ujenzi kutoka Holland.
 
Nimejaribu kufuatilia kauli za waliojenga nyumba. Huwa wanapenda kuwaogopesha waliopanga kuwa ujenzi ni gharama.

Huwezi kutana na mtu akakutia moyo hata kidogo. Lengo la wengi waliojenga ni ku play god. Yani wanapenda waheshimike na kujionesha kuwa wana mawe marefu.

Mimi ninapopiga gharama za ujenzi, napata gharama za chini kama ambavyo Magufuli alifanya kwenye ujenzi wa hostel za UD. Tukienda kwa stail yake, mbona kila mtu atakuwa na ka mjengo!
Jenga tu mjengo wako mkuu, hakuna anayekuzuia
 
Nimekusoma mkuu hapo sasa kikubwa nilichokiona ni kila mtu ajenge kutokana na uwezo wake na si kulalamika kuwa ujenzi si gharama au ujenzi ni gharama.
Mkuu hapo sio tu kujenga kutokana na uwezo, ameonyesha pia kwa sababu fulanifulani, mfano kutokuwa na taarifa sahihi na kutokufanya uchunguzi wa kina, unaweza kutumia mil 100 kujenga nyumba ambayo mtu mwingine ameijenga katika eneo hilohilo ulipojenga wewe na factors zingine kubaki constant kwa mil 50 tu.
 
Ukiwa na kiwanja, gharama ya nyumba ya vyumba vitatu, kwa basic finishing ni around 20M. With the same house some one will mention kuwa ametumia milioni mia! Utadhani kajengea mchanga wa makinikia.
Eti? Wapi huko tuhamie? Vyumba vya size gani? Kwa materials gani? Weka BoQ mezani.
 
Ushauri wako huu ndio ambao nimekuwa naufanyia kazi. Sasa mimi nafanya tu survey ya maeneo yanayofaa kwa mimi kujenga, huku nikifuatilia gharama ya ujenzi na alternatives.

Mfano kuna jamaa mmoja aliniambia yeye amejenga nyumba yake kwa kutumia mafundi aliowatoa kijijini, hii yote ilikuwa ni kuepuka mafundi wa mjini ambao ujanja ni mwingi ukichanganyikana na wizi. Nyumba imejengwa vizuri utadhani hao mafundi wana degree za ujenzi kutoka Holland.
Hongera sana mkuu!

Mimi naamini sana katika kuwa mvumilivu, kusaka taarifa sahihi ikiwemo kuwasikiliza watu wote haijalishi wanakufurahisha ama lah! Kwani kwa kila mmoja kuna kitu utapata kujifunza.
 
Ndio nyie tunaowazungumzia.
Nyumba ya mabati sabini kwa elfu kumi na tano bati moja ni milioni moja hiyo.
Mbao za milioni na nusu zinatosha kupaua.
Matofali elfu mbili na mia tano ni milioni tatu hiyo, cement ya kujengea mifuko mia ni sh milioni moja hiyo.. Fundi wa kujenga na kupaua, milioni nne hiyo.. Hizo gharama unazozungumza, unajenga shule?
duh hizi hesabu zako sijui
 
Weka pamba masikio, halafu cheza muziki...usiogope maneno ya watu.
Utageuka KIBWEKA... Kucheza Muziki usio sikiliza sauti na ALA...

Umekwisha weka PAMBA Masikioni..

Unategemea nini...!!?
Unamaanisha hutaki kusikia hata USHAURI wa Mafundi...!!
 
Ina maana mpaka unaogopa maana yake hujachukua uamuzi wa kujenga hivyo unapokwenda kuuliza kwa jirani akakuambia kujenga nyumba ni gharama unachukulia kama anakutisha kumbe anakueleza ukweli ili sasa wewe mwenyewe unatakiwa uumuulize alifanyaje mpaka akajenga ndipo na yeye atakuambia njia alizopitia ikiwepo na kununua vifaa duka moja kuanzia msingi mpaka kufikia hatua ya kujenga urafiki na kuanza kuchukua vifaa na kulipa mwisho wa mwezi pamoja na kuchagua fundi mzuri.

Lakini kingine pia ujenzi ni hatua hasa kwetu wenye maisha ya kuunga unga maana kuna wengine anataka akinunua kiwanja na ajenge palepale (ndo pale unapokuta mtu anasubiri zifike 20million ndo anunue kiwanja kumbe hata kama huna mpango wa kujenga kiwanja kununua iwe ni lazima ili siku ukiona wakati umefika au ela zimekutembelea ni kufanya utekelezaji

Kwa ujumla hakuna anaetishwa ila ni kuelezana ukweli though ni ngumu mtu kukupa figure zote hasa kama sio rafiki maana kuna wengine sio wajenzi zaidi ya kupekuapekua mambo ya watu......mtu mwenye nia ya kujenga huwa haulizi gharama ya kujenga nyumba ni kiasi gani bali huuliza idadi ya vifaa vinavyohitajika kujenga nyumba pamoja na ufundi ili mwenyewe sasa akapige hesabu kulingana na aina ya material anayotaka maana kuna bati la 12,000 mpaka 50,000 na yote ni mazuri na size ni moja
 
Back
Top Bottom