Waliojenga nyumba hupenda kuwaogopesha wengine kuwa ujenzi ni gharama!

bitimkongwe

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
3,896
2,000
Acha kudanganya watu labda kama unajenga kibanda kijijini ila ujenzi ni gharama, take it from me.

Sent from my VFD 300 using JamiiForums mobile app
Ni gharama hasaaaa lakini ukimwambia mtu ukweli anadhani unamdanganya au unajisifia.

Kabla ya kuanza ujenzi, jaribu kununua daftari na uweke gharama zote za ujenzi ambazo utazitumia. Pale utapomaliza basi piga hesabu ya matumizi yako.

Kwa kweli hutaamini kwamba ulitumia fedha zote zile kwenye ujenzi.

Shida yetu sisi huwa tunajenga pole pole, leo laki mbili kesho laki nne kadiri unavyopata fedha na kuliendeleza jengo pole pole. Lakini piga gharama zote uone huo mchezo wake.
 
bitimkongwe

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
3,896
2,000
Jenga na wewe alafu ulete hizo gharama za chini ili uwatie moyo wengine!

Gharama za ujenzi zinategemea na eneo ulipo, nature ya kiwanja, materials unazotumia na aina ya wajenzi unaotumia na ukubwa na hadhi ya nyumba unayotaka jenga... Mtu akikutisha gharama wala zisikutikise, hamuwezi fanana!

Wengine wamejenga nyumba ya kawaida tu, sio ghorofa na millioni 150 TZS zimekatika na bado nyumba haina finishing nje!
Ni kweli, mfano huwezi kulinganisha tiles za mchina za Sh. 8,000 kwa square meter na za muitaliano za sh. 50,000 kwa square meter, au masinki ya sh. 80,000 na yale ya 400,000 kila moja. Milango na madirisha ndiyo hayasemeki, mengine ukienda kwenye nyumba mpaka unaona huruma lakini unanyamaza.

Vitu vinavyojumliisha gharama ya nyumba ni vingi, na hasa vile vya ndani vinavyohusu finishing.

Lakini ukijenga nyumba ya umeme phase moja na vifeni vyako kila chumba na taa moja moja basi hapo utaona hakuna gharama.
 
mkaamweusi

JF-Expert Member
Feb 19, 2013
546
1,000
Kuwa na nyumba nakufananisha na kuwa digrii.Unaweza kuwa na digrii ya kiswahili, ualimu, sayansi ya kompyuta au udaktari.

Haya tukiingia kwenye vigezo vingine kuna wenye pass, lower second, upper na first class.

Ujenzi sio kazi kama una kipato cha siku cha uhakika.

Na itakuchkua miaka mingi kumaliza kama kipato hicho ni kidogo sana say 5000 per day.Mpaka kumaliza nyumba walau ya mil5_7.

Pia kuna mikoa ambayo ujenzi wake ni nafuu mfano mbeya na iringa kule ukiwa na kiwanja tu unaita watu wafyatue tofali au ununue moja sh100 mpaka 200.

Hata million 3 unaweza pata mahali pa kuegesha mbavu zako.
 
Keyser Söze

JF-Expert Member
Mar 12, 2013
324
500
Top View

top_view.jpg
 
t blj

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
3,639
2,000
Huu si msingi wa kawaida na kiukweli hata sijui kwa nini umeamua kujenga hapo, inaonekana ni eneo amabalo bado halijajengwa sana kwa nini ujenge structure ya gharama hivi wakati ungeweza hata kuhamisha mahali pa kukaa nyumba hapo ukaacha kwa matumizi mengine?

Ni kweli kwa msingi huo , kwa mtu asiye jua mambo ya ujenzi anaweza akaogopa sana, ila hukuwa na sababu ya kujenga eneo hilo ,zaidi ya kutaka tu kuchoma pesa zako
 
Hivi mkuu kichwa chako kina akili kweli? Yaani huo msingi unauona mkubwa? Yaan kuongezeka kama tofali 300 ndio kunakufanya utoe povu kiasi hicho?
 
t blj

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
3,639
2,000
Hivi mkuu kichwa chako kina akili kweli? Yaani huo msingi unauona mkubwa? Yaan kuongezeka kama tofali 300 ndio kunakufanya utoe povu kiasi hicho?
Kichwa changu kimetimia kabisa , hivyo vijumba vya chumba tatu , nimejenga kadhaa, hapa nilipo najenga nyingine kibaha huko. For fun though maana napenda sana kuhamia nyumba mpya ,kuna feeling zake

Nashangaa tu unavyotumia pesa zako bila huruma na siwezi kutoa povu kwa msingi kama huo

Mada inasema waliojenga wanapenda kutishia wasiojenga , nashangaa ulicho present ndo hicho hicho, kama msingi tu unalazimisha ule 6 millions plus , unatuma salamu gani kwa wanaotaka kuanza ujenzi?
 
Unapoambiwa kichwa chako hakina akili unatakiwa ujitathmini! Aliyekwambia nimetumia 6 Millions plus nani? Hiyo list niliyoweka hapo juu ni BOQ, Hizo ndio estimates(Makadirio) nilizopewa na mchora ramani, Na wala haikufika hiyo gharama, Pia kama unayosema sijui unajenga wapi huko na ni mzoefu ungejua kabisa katika ujenzi gharama kubwa si tofali. Usipende kurukia vitu tu usivyoelewa. Mfano kwenye list kuna gharama za mbao(1.35M), Unafikiri nilienda kununua mbao wakati za kukodi zipo?
 
Kulikuwa na sababu gani ya kuweka ile list hapa wakati unajua kuwa utatumia less than that?
Umeelewa maana ya huu uzi kweli?
 
Keyser Söze

JF-Expert Member
Mar 12, 2013
324
500
Kulikuwa na sababu gani ya kuweka ile list hapa wakati unajua kuwa utatumia less than that?
Umeelewa maana ya huu uzi kweli?
Picha imeambatana na maelezo kuwa ni mkadirio ya msingi kutoka kwa mchora ramani, Kama zilikuwani gharama halisi zilizotumika kwenye ujenzi isingekuwa makadirio
 
t blj

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
3,639
2,000
Picha imeambatana na maelezo kuwa ni mkadirio ya msingi kutoka kwa mchora ramani, Kama zilikuwani gharama halisi zilizotumika kwenye ujenzi isingekuwa makadirio
Inaonekana huu ni ujenzi wako wa kwanza mr akili nyingi,
Ili usaidie watu andika kile ulichotumia , na si kile unachoambiwa utatumia , kuna tofauti kubwa sana kwenye makadirio na gharama halisi,
Si lazima iwe smart edited print outs kama ulivyoileta hapa unaweza kuandika tu na peni hata kwenye daftari dogo

Lengo la uzi ni kuelezea waliojenga wanavyowatisha wasiojenga nyumba , hukuwa na sababu ya kuleta makadirio yale ya 6.4 mil , ilhali hadi ulipofikia unajua gharama halisi ya msingi wako kuwa ni chini ya zile figures .
 
Nyumba Nafuuu

JF-Expert Member
Nov 29, 2016
323
500
Nimejaribu kufuatilia kauli za waliojenga nyumba. Huwa wanapenda kuwaogopesha waliopanga kuwa ujenzi ni gharama.

Huwezi kutana na mtu akakutia moyo hata kidogo. Lengo la wengi waliojenga ni ku play god. Yani wanapenda waheshimike na kujionesha kuwa wana mawe marefu.

Mimi ninapopiga gharama za ujenzi, napata gharama za chini kama ambavyo Magufuli alifanya kwenye ujenzi wa hostel za UD. Tukienda kwa stail yake, mbona kila mtu atakuwa na ka mjengo!
FAHAMU MAKISIO YA GHARAMA ZA UJENZI WA NYUMBA YAKO (+255-657-685-268)

Fahamu gharama ujenzi wa nyumba yako kwa kila steji kama MSINGI, KUTA, PAA, RANGI, DARI, MAJI, UMEME... ili uweze fanya tathimini ya uwezo wako kama upo chini au juu sanaaa na uanze kuweka mipango mikakati vyema ya kuweza kufanikisha ujenzi wa nyumba yako!
20210529_124307.jpg
 
dimple

Member
Dec 6, 2016
47
125
Usishangae sana kuna watu wanapigwa sana ktk ujenzi ila take it from me ujenzi sio garama kiivyo gharama ni finishing na finishing inategemea na uwezo wako mm nimejenga ya kupangisha yenye kila kitu ila vyuma 2 vyote vina vyoo ndani pia public toilet,jiko,sebule,dining tena raman ya kisasa tu imeenda 7M hadi juuu na shimo la choo na hapo kiwanja kina slope sana upande mmoja ulibeba tofali nyingi sanaaa ndo imefika hiyo 7M now navuta nguvu kidogo nianze finishing.
nilikosea bora ningepiga underground sabab ni nyumba za kupangisha eneo lililobaki nitajenga underground zingatia

Unapotaka kujenga usiulize sana ushauri kqa watu utavunjika moyo kila mtu ktk ujenzi kapitia changamoto zake wewe jilipue tu pia kuna wale wa kukusanya pesa hadi zifike milions ndo anaanza while mwingine akipata hata laki tano anaenda ongeza kozi hata round 2 we jenga tu utaweza kulingana na mfuko wako hata wauza mchicha wanajenga kwan wanamamilioni jilipue bhana
Nimejaribu kufuatilia kauli za waliojenga nyumba. Huwa wanapenda kuwaogopesha waliopanga kuwa ujenzi ni gharama.

Huwezi kutana na mtu akakutia moyo hata kidogo. Lengo la wengi waliojenga ni ku play god. Yani wanapenda waheshimike na kujionesha kuwa wana mawe marefu.

Mimi ninapopiga gharama za ujenzi, napata gharama za chini kama ambavyo Magufuli alifanya kwenye ujenzi wa hostel za UD. Tukienda kwa stail yake, mbona kila mtu atakuwa na ka mjengo!
 
kidunula1

JF-Expert Member
Apr 2, 2016
6,056
2,000
Ujenzi ni gharama ila tusiogope kujenga, tuanze tu kidogo kidogo hata kama ni miaka kumi ndio itaisha sawa tu!
 
A.Ngindo

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
213
225
usishangae sana kuna watu wanapigwa sana ktk ujenzi ila take it from me ujenzi sio garama kiivyo gharama ni finishing na finishing inategemea na uwezo wako mm nimejenga ya kupangisha yenye kila kitu ila vyuma 2 vyote vina vyoo ndani pia public toilet,jiko,sebule,dining tena raman ya kisasa tu imeenda 7M hadi juuu na shimo la choo na hapo kiwanja kina slope sana upande mmoja ulibeba tofali nyingi sanaaa ndo imefika hiyo 7M now navuta nguvu kidogo nianze finishing.
nilikosea bora ningepiga underground sabab ni nyumba za kupangisha eneo lililobaki nitajenga underground

zingatia

unapotaka kujenga usiulize sana ushauri kqa watu utavunjika moyo kila mtu ktk ujenzi kapitia changamoto zake wewe jilipue tu pia kuna wale wa kukusanya pesa hadi zifike milions ndo anaanza while mwingine akipata hata laki tano anaenda ongeza kozi hata round 2 we jenga tu utaweza kulingana na mfuko wako hata wauza mchicha wanajenga kwan wanamamilioni jilipue bhana
Unajenga mkoa gani kiongzi?
 
CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
5,729
2,000
Huwa sikatishi mtu tamaa hata siku 1 ukiniuliza bei ya mali yangu yyte siwezi kwambia gharama za juuu, huwa nashushaga bei nasema bei ndogoooo...

Najua utashangaa how this possible kitu hiki kiwe bei chini hivi, nitakuelewesha kwa utaalamu ili kukuthbtshia kweli ni bei Ndogo.

kasheshe utaenda kukutana nalo ukiingia kufanya kwa vitendo vile vitu nilivyokua nikikwambia ni bei ndogooo kama n dukani utakutana na bei husika Kama ni Fundi atakupa bei kamili.

Next time mtu akirudi namwambia ukweli kuwa "nlimwambia vile makusudi ili akafanye" maana ngemwambia ukweli asingefanya au angeniona namtambia au namtisha.

sasa ili tusitishane au usione nakutambia Ukija home ukiona chochote cha gharama ujue bei nakutajia isiyozidi 50k ili uone simple.

Reality show utakutana nayo siku unafanya kwa vitendo we mwenyewe.
 
Nas Jr

JF-Expert Member
May 15, 2018
4,736
2,000
Ujenzi sio gharama,, ujenzi ni Bure..

Wabongo tunafeli sana kwakusikiliza sana,,, Ideas nyingi huwa zinakufa kwa sababu ya kusikiliza watu...

Nunua kiwanja mkuu halafu kajenge bure..
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom