bitimkongwe
JF-Expert Member
- Oct 21, 2009
- 7,285
- 6,675
Ni kweli, mfano huwezi kulinganisha tiles za mchina za Sh. 8,000 kwa square meter na za muitaliano za sh. 50,000 kwa square meter, au masinki ya sh. 80,000 na yale ya 400,000 kila moja. Milango na madirisha ndiyo hayasemeki, mengine ukienda kwenye nyumba mpaka unaona huruma lakini unanyamaza.Jenga na wewe alafu ulete hizo gharama za chini ili uwatie moyo wengine!
Gharama za ujenzi zinategemea na eneo ulipo, nature ya kiwanja, materials unazotumia na aina ya wajenzi unaotumia na ukubwa na hadhi ya nyumba unayotaka jenga... Mtu akikutisha gharama wala zisikutikise, hamuwezi fanana!
Wengine wamejenga nyumba ya kawaida tu, sio ghorofa na millioni 150 TZS zimekatika na bado nyumba haina finishing nje!
Vitu vinavyojumliisha gharama ya nyumba ni vingi, na hasa vile vya ndani vinavyohusu finishing.
Lakini ukijenga nyumba ya umeme phase moja na vifeni vyako kila chumba na taa moja moja basi hapo utaona hakuna gharama.