Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,181
IPTL imekuwa na mkataba wa kifisadi na Tanesco kwa kuiuzia Tanesco umeme kwa bei ya juu zaidi ya soko na kuifanya Tanesco iendeshwe kwa hasara kwa sababu tozo zake ziko chini ya bei ya umeme Tanesco walizozinunulia!
Tusiukwepe ukweli ya kuwa waliowaongezea IPTL mkataba kwa masharti yale yale ya kifisadi na la ajabu hadi leo waliowaongezea mkataba IPTL hawajachukuliwa hatua kwa makosa ya jinai ya kuuhujumu uchumi.
Baada ya kuwaongezea IPTL mkataba wa kuendelea kuifilisi Tanesco bila kuishirikisha EWURA na kuigeuza EWURA rubber stamp ni wazi waliingilia majukumu ya kisheria ya EWURA.
Bila kuwachukulia hatua wahusika hawa na EWURA kugoma kuwaongezea muda wa leseni IPTL hadi watakapokubali kuwauzia Tanesco umeme bei chini ya bei Tanesco inawauzia wateja wake na kufuta capacity charges ambazo sisi ni kati ya nchi chache sana zina mikataba na wawekezaji ya kipumbavu kama hii.
Tumbua tumbua majipu hewa huku tunalinda saratani ni utapeli wa kutisha wa kisiasa ambao wakati tu ndiyo utawaumbua wasanii hawa.
Waliowaongezea mkataba IPTL ni baraza la mawaziri la JK ambalo mtumbua majipu ni Mjumbe sasa ni nani wa kumfunga paka kengele?