Walioibua ukweli ni waandishi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walioibua ukweli ni waandishi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Wazalendo halis, Nov 1, 2009.

 1. W

  Wazalendo halis Member

  #1
  Nov 1, 2009
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naona wote mmechangia kuhusu milioni 400 - kama zilikuwa na tij au la.

  Swali muhimu ni kwamba,kwanini walificha vielelezo wakati ule, jambo ambalo lingerahisisha maamuzi yakichukuliwa kwa wakati mmoja na ya uhakika. Issue ni kwamba walitumia pesa za umma and then wakaficha vielelezo vingine ambayo ilikuwa so unprofessional.

  Na kwanini wanatoa vielelezo hivyo now kwa vyombo binafsi vya habari?
  Pia swali lingine muhimu ni kuhusu hitimisho la kazi. Kazi waliyopewa ni ile ya kutuambia Richmond ni ya nani ili wahusika moja kwa moja wachukuliwe hatua badala yale kamati ilimumunya maneno na kusema wana vielelezo ambavyo wamevihifadhi kwa kuogopa kuiacha uchi serikalini.
  Kwani wao walitumwa kuprotect serikali au kuchunguza kwa ukamilifu saga la Richmond kwa niaba ya watanzania?
  Pia, mnasema pesa ziliweza kuokoa mali zetu kwa kuifungia Richmond. Ikumbukwe kuwa Richmond ilishafungiwa wakati Mwakyembe anawasilisha ripoti yake. Jasho la waandishi wa habari ndilo lililosababisha kutimuliwa kwa richmond.
  Kamati zikitumia pesa nyingi na kujibu maswali yote, hapo angalau inakubalika. Lakini, kamati iliyotumwa kutuchinguzia richmond ni ya nani, mpaka leo imeshindwa kutuambia.
  Instead, eti wao waliotumwa kujibu hilo swali, sasa wanauliza serikali kwamba richmond ni nani na wahusika wake halisi ni nani na walihusika vipi moja kwa moja? Ujinga gani huo?
  Shida yetu ni kwamba, kwanini kamati walihold evidence ambayo inawezekana ikarahisisha watuhumiwa halisi kufikishwa mahakamani. Hakuna anawetetewa hapa. Hapa ni kuuliza, mbona wote wapiganaji na watuhumiwa wa ufisadi, wote wanafanana?
  Watanzania tunashindwa kuelewa, miaka miwili baada ya serikali kuanguka kwa swala la umeme, bado tuko gizani? Anayetutetea na kutushughulikia sisi wananchi ni nani? Mbona tofauti haionekani?
  Hizo documents kwa nini hazikutolewa wakati wa kuwasilisha ripoti?
  Na bunge zimetupatia alternative gani kuhusiana na swala la umeme -- au ndiyo tuwaachie wabunge walumbane wakati sisi tuendelee kutafuta magenereta yetu binafsi ya kuongeza kelele mijini mpaka watanzania hata hatusikilizani?
  Kamati zote zinatumia pesa, lakini tunapima kwa matokeo yao. Matokeo yakifichwa, tunapima vipi?
   
 2. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #2
  Nov 1, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,083
  Likes Received: 4,031
  Trophy Points: 280
  Kwa vile wanajua kamati nyingi huundwa na report zake huwa huifadhiwa makabatini kujaa vumbi badala ya kuwekwa hadharani kupatiwa ufumbuzi au utekelzaji wa maagizo! Kwa sababu hiyo wazalendo wameamua kubaki na walichogundua ili wailipue serikali ya CCM kwa vile walijua utekelezaji utakuwa na utata wamechoka na mazoea! kaa mkao wa kula wataumbuliwa wengi soon!
   
Loading...