Walioiba mkia wa Simba kusakwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walioiba mkia wa Simba kusakwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Mar 14, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  WIZARA ya Maliasili na Utalii, imewataka wakazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam, waliokata mkia wa Simba na kung’oa kucha zake, kuvirejesha vinginevyo watasakwa ili kuchukuliwa hatua za kisheria.

  Taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana na Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Felician Kilahama, alisema Simba huyo aliyeuawa alikutwa bila mkia wala kucha.

  Wiki moja iliyopita, Simba jike aliuawa na mgambo eneo la Mbagala Kimbangulile, baada ya kumjeruhi mtu mmoja ambaye bado amelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

  “Imethibitika kuna watu waling’oa kucha 10 na kukata mkia wa Simba na kuondoka navyo, Wizara inamtaka aliyehusika kurudisha nyara hizo kituo chochote cha maliasili au polisi, kuendelea kukaa na nyara hizo ni kwenda kinyume na sheria za nchi,” alisema Dk Kilahama.

  Pia, Dk Kilahama alitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa vituo vya maliasili watakapomuona mnyamapori yoyote akizagaa mitaani.

  Hatua hiyo inafuatia uvumi ulioenea mwishoni mwa wiki kwamba, kulikuwa na Simba wengine waliokuwa wakizurura na kuunguruma eneo hilo.

  “Askari wa wanyamapori wanaendelea kufanya msako wa Simba hao wanaohofiwa kuwapo jijini, lakini bado hawajamuona na juhudi za kuwatafuta zinaendelea,” alisema Dk Kilahama.
   
 2. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Pia nimesikia korodani za simba ni dawa ya nguvu za kiume so sijui kama korodani zake wadau waliziacha unless kama alikuwa ni simba jike.
   
 3. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Vipi nyongo ipo salama?
   
 4. L

  Leornado JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  mbona walioiba mabilion ya noti mpya uwanja wa ndege wa mwalimu nyerere wasisakwe??

  mambo mengine ukifuatilia ni kujidhalilisha, i wish kumuona polisi aliepewa jukumu hili.
   
 5. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  unachoma unakula au unazichemsha?
   
Loading...