John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,373
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimelaani tukio la mauaji ya Juma Ramadhan (35) kupigwa risasi na askari wakati Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma likidhibiti vurugu, Machi 14, 2022 katika Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
LHRC imetoa wito hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya afisa wa Polisi waliohusika katika tukio hilo, iundwe Tume Huru ya kijaji kufanya uchunguzi wa kifo hicho na kuanzisha chombo huru kwa ajili ya kupokea na kuchunguza matukio dhidi ya Jeshi la Polisi.
Wamesema Jeshi la Polisi linatakiwa kuzingatia mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Matumizi ya Nguvu na Silaha wa Mwaka 1990 pamoja na Mwongozo wa Utendaji kazi wa Jeshi la Polisi (PGO marejeo ya mwaka 2021).