Waliohusika na mauaji ya watu 17 wahukumiwa kunyongwa hadi kufa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Musoma imewahukumu kunyongwa hadi kufa Watuhumiwa 6 kati ya 9, baada ya kukutwa na hatia ya mauaji ya watu 17 wa familia moja yaliyotokea Februari 10 mwaka 2010 katika eneo la Mgaranjabo lililoko kwenye manispaa ya Musoma mkoani Mara.

Mahakama hiyo pia imewaachia huru Watuhumiwa wengine 3 wa kesi hiyo, baada ya kujiridhisha kuwa hawana hatia katika makosa waliyoshtakiwa.

Washtakiwa waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa ni Juma Mgaya, Aloyce Nyakumu, Nyakangara Biraso, Marwa Mgaya, Wambura na Sadock Ikaka ambao kwa pamoja wanadaiwa kushiriki mauaji hayo ambayo chanzo chake ni kulipiza kisasi.

Akitoa hukumu hiyo hii leo Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Musoma Mustapher Siyani amesema kuwa, mahakama imeridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa Jamhuri juu ya watu hao kuhusika na tukio hilo la kinyama.

Amesema kutokana na ushahidi na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo, Watu hao sita walikuwa na nia ya dhati ya kuwaondolea uhai watu hao ambao miili yao ilikutwa na majeraha makubwa sehemu za kichwani, shingoni na mgongoni.

Chanzo: TBC
 
Mauaji ya Kulipiza Kisasi haya.
EPISODE I.
Picha ilianza hivi.
Katika Eneo la Mgarajabho walijitokeza Vijana Wawili tokea Maeneo ya Zanaki waliokuwa wamebeba Nyama za Wanyama "NUNGUNUNGU" waliowawinda kwenye Vilima vinavyozunguka eneo hilo.
Baada ya kuonekana na Nyama hizo Mkazi mmoja wa Eneo hilo akawashuku kwamba watu hao Vijana kuwa si wawindaji bali ni wezi wa Mifugo yao inayopotea ovyo ovyo. Vijana wakatoa maelezo na kujitetea wakasisitiza wao siyo wezi bali ni wawindaji wa siku nyingi na Nyama wakazifungua kwenye viroba wakamwonyesha. Mkazi huyo hakuridhika na utetezi wao akapandwa na Munkari na kukataa utetezi wa Vijana hao ikifuatiwa na Kupiga mwano wa Weziiiiiiiiiiiiiii kwa sauti ile ya juuu.
Wakafika Akina Murra na Mikuki na Mapanga. Ndani ya dakika 5 wale Vijana Wawindaji wakawa mchanganyiko na zile nyama zao haikutambulika Nyama ya Nungu Nungu wala ya wale Vijana Wazanaki hata zile Baiskeli zao haikujulikana hii ni pedal na hii ni spoket.
Kwa hakika wale Vijana walipoteza Maisha Ugenini kwa Udhalimu wa Hali ya Juuu. Ingekuwa miaka ya Nyuma kidoogo tukio hili lingeleta Vita ya Ukabila.
Baaada ya tukio kufanyika na Akina Murra wakiwa pale wanaendelea kukata kata ile miili ya Vijana Wawindaji akatokea Msema Ukweli mmoja jirani yake na Mpiga Mwano ambaye tutakuja kuona huko mbeleni alivyoshiriki mauaji ya watu 10 kulipiza kisasi... na kunyoosha Lugha kwamba waliouwawa ni Wawindaji na sio wezi.... Kimbembe kilianzia hapa

Episode II na EPISODE III zitafuata.
 
Leta episode 2 mkuu
 
Back
Top Bottom