Waliohusika kifo cha mama mzazi wa Hoyce Temu Hospitali ya KCMC waondolewe

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
52,883
25,250
HUU MSIBA UMEHUZUNISHA WENGI SANA MKOANI MOSHI

NA PENGINE WENGI WANAKUFA HAPO HOSPT BILA KUPEWA MSAADA

WAZIRI WA AFYA WALIOCHANGIA KIFO CHA HUYU MAMA WAONDOLEWE KABISA HAPO HOSPT WATATUMALIZIA WAZAZI WETU

MAPOKEZI MASAA MAWILI BILA HUDUMA??KWELI AISEE

=====

MAMA MGHWIRA-KULIKUWA NA UZEMBE KCMC,KIFO CHA MAMA WA HOYCE TEMU​

By Alex Sonna
1.JPGAAAAAAA-1.jpg

Mkuu wa Mkoa mstaafu wa Kilimanjaro, Mama Anna Mghwira akizungumza na waombolezaji wakati wa ibada ya mazishi ya mama mzazi wa mtangazaji wa kipindi cha Tanzania Yetu, Bi. Hoyce Temu iliyofanyika mwishoni mwa wiki nyumbani kwa marehemu Sion Temu iliyopo Mnazi Mmoja, mkoani Kilimanjaro.
2.JPGAAAAAAAAA-1.jpg

Mkuu wa Mkoa mstaafu wa Kilimanjaro, Mama Anna Mghwira akisalimia familia ya marehemu wakati wa ibada ya mazishi ya mama mzazi wa mtangazaji wa kipindi cha Tanzania Yetu, Bi. Hoyce Temu iliyofanyika mwishoni mwa wiki nyumbani kwa marehemu Sion Temu iliyopo Mnazi Mmoja, mkoani Kilimanjaro.
3.JPGAAA-8.jpg

Familia ya marehemu ikiomboleza wakati wa ibada ya mazishi ya mama mzazi wa mtangazaji wa kipindi cha Tanzania Yetu, Bi. Hoyce Temu iliyofanyika mwishoni mwa wiki nyumbani kwa marehemu Sion Temu iliyopo Mnazi Mmoja, mkoani Kilimanjaro.
……………………………………………………………….
NA MWANDISHI WETU

Mkuu wa Mkoa mstaafu wa Kilimanjaro, Mama Anna Mghwira amesema watoa huduma wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC wamefanya uzembe katika tukio la kifo cha mama mzazi wa mtangazaji wa kipindi cha Tanzania Yetu, Bi. Hoyce Temu baada ya eneo la mapokezi kushindwa kuchukua hatua za haraka kuokoa uhai wake.

Akitoa kauli hiyo wakati wa ibada maalum ya mazishi kama rafiki wa karibu sana wa marehemu iliyofanyika nyumbani kwa marehemu, Mnazi Mmoja Mkoani Kilimanjaro, Mama Mghwira alitoa kauli hiyo wakati akitoa neno la shukrani kwa maisha ya marehemu Sion Temu na kuwaasa watoa huduma wa KCMC kuzingatia utu na uadilifu katika kazi zao.

“Niseme neno moja kwa watoa huduma wetu katika nyanja mbalimbali kila kazi unayopewa, unayojipa, unayotumwa tuifanye kwa weledi, upendo na kwa uaminifu sana, hatuna baraka zingine za kuokota huku duniani isipokuwa kuhudumia watu kwa upendo. Alisema Mama Anna Mghwira.

Mama Anna Mghwira aliongeza kuwa kulikuwa na uzembe baada ya mgonjwa kufika hapo na kukaa kwa zaidi ya masaa mawili bila kupokelewa katika mapokezi hiyo ya wagonjwa KCMC.

Akielezea tukio hilo ambapo ulifanyika uzembe kwa mapokezi kushindwa kumpokea marehemu Sion Temu kwa wakati:

“Hatutaki kulaumu lakini kwa kweli kulikuwa na aina ya uzembe ambao tunaweza kuuzungumza ni kwamba mtu ameletwa kwenye kituo cha Hospitali mahali anategemewa apokelewe, hakupokelewa nimemshusha mwenyewe kwenye gari baada ya masaa mawili.

Hilo halikuwa sahihi awe alikuwa mzima awe alikuwa ameumia awe alikuwa ameshafariki hakuna sababu.

Katika hilo niwaombe sana ndugu zangu Hospitali yetu ya KCMC tuwe makini sana na jinsi tunavyopokea, tunavyohudumia na tunavyowaacha wagonjwa wetu hata wafu wetu, wote ni wa kwetu walio hai ni wetu na wasio hai ni wetu na ndio maana tunawalilia, tunawafurahia tunawashangilia na tunawasheherekea, kama yupo mwana KCMC hapaapeleke ujumbe dhidi ya mapokezi hiyo ya wagonjwa haitendi kwa weledi, naomba sana hilo lizingatiwe na sisi wote mahala pale popote tulipo tunapotoa huduma.” Alisema Mama Anna Mghwira.

Aidha, akitoa pole kwa familia alibainisha namna alivyomfahamu marehemu
“Namshukuru tena mama Sion kwa maisha yake. Kama mnavyoona uso huu tu unaongea mengi sana. Picha inamuonyesha mtu mwenye furaha, mwenye upendo, mwenye amani sana sana kwa muonekano kwa ndani kama familia ilivyotushuhudia.” Alisema Mama Anna Mghwira

Aidha, Mama Anna Mghwira alitumia wasaha huo kwa wana kilimanjaro kujiandaa kumpokea Mkuu wa Mkoa mpya kama walivyompokea yeye na kukaa kwa miaka minne ndani ya Mkoa huo.

“Mama … nimekaa nae kwa miaka hii minne na sasa siku yake ya mwisho ya maisha na mimi ni siku ya mwisho ya kazi, ni jambo jema sana…

wakati naingia hapa niliingia tulikuwa tunamzika Mzee Ndesamburo, Mzee ambaye pia alikuwa rafiki yangu nimetengeneza marafiki wengi sana japokuwa nimeishi kwa muda mfupi sana hata uhusiano wangu na Hoyce Temu umeimarika zaidi kwa kweli baada ya kuja hapa” alieleza Mama Anna Mghwira.
Na kuongeza kuwa:

“Namshukuru Mungu kwa haya yote na nawaahidi kabisa popote pale ninapoenda nyumbani kwetu nilipotoka, kwangu ninapoishi karibuni nitaendelea kuwaombea, kuwakumbuka na kuwaenzi sana sana. Asanteni Wachungaji kwa ibada njema na mafundisho mazuri Mungu atubariki sote, Amina” Alimalizia Mama Anna Mgwira.
Marehemu mama Sion Temu alifariki dunia Jumapili ya siku ya Mama duniani (Mother’s Day) dakika chache baada ya kuongea na binti zake kwa simu na kuwatakia heri ya siku hiyo na kuzikwa siku ya Jumamosi tarehe 15/5/2021 nyumbani kwake Moshi Mnazi Mmoja mkoani Kilimanjaro.

Mbona haya mambo yapo sana huko mahospitalini? Hamjui au kisa mtu wenu yamemkuta!!!...mkome tu mradi wote ni maccm mie sijali na i dont care
Tusipende kulaumu watumishi wa kada nyingine na kumbe nasi kwenye kada na ofisi zetu kumejaa madudu.

Watumishi wa afya ni sawa na watumishi wengine wowote wale Tanzania. Hawakuzaliwa wala kukulia kwenye mazingira tofauti kama mimi na wewe ili kuwaandaa kuwa watumishi wa Afya. Watumishi hawa wanafanana na wale walioko Tanesco, DART, BOT, Mahakama, Takukuru, Polisi, Ujenzi, Ardhi n.k.

Kabla ya kulaumu kila mtu ajitathmini pale alipo, anafanya nini kumhudumia mteja? Tujitathmini kama Taifa.
 
Mkuu sisi humu JF tuko perfect kwenye Kada zetu hakuna makandokando yoyote.
 
Leo Muhimbili nusura jamaa akate roho mikononi mwangu! Yaani mimi naumwa ila nikajikuta mimi ndio mzima.
POLE!
Sometimes tunalaumu, tu, unakuta wahudumu wachache na emergency ni nyingi, na kila mtu ana haki ya kuhudumiwa, eti. Siyo kwa sababu ni fulani basi hoehae tuachwe wakimbiliwe wao.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Tusipende kulaumu watumishi wa kada nyingine na kumbe nasi kwenye kada na ofisi zetu kumejaa madudu.

Watumishi wa afya ni sawa na watumishi wengine wowote wale Tanzania. Hawakuzaliwa wala kukulia kwenye mazingira tofauti kama mimi na wewe ili kuwaandaa kuwa watumishi wa Afya. Watumishi hawa wanafanana na wale walioko Tanesco, DART, BOT, Mahakama, Takukuru, Polisi, Ujenzi, Ardhi n.k.

Kabla ya kulaumu kila mtu ajitathmini pale alipo, anafanya nini kumhudumia mteja? Tujitathmini kama Taifa.
Kwahyo emergence kama hizo nan alaumiwe mkuu..tuendelee kushangilia tu au?au hujawah kwenda hosp ukaona maajabu mapokez?..nenda bas labor huko ukaone wamama wanavyonyanyasika..ptu
 
Tatizo Hawa wanashughulika na roho za watu. Kosa linaenda na roho ya mtu
 
Kwahyo emergence kama hizo nan alaumiwe mkuu..tuendelee kushangilia tu au?au hujawah kwenda hosp ukaona maajabu mapokez?..nenda bas labor huko ukaone wamama wanavyonyanyasika..ptu
Mkuu kulaumu hakusaidii ila ni kutotaka kutambua madhaifu yetu pia. Kulaumu hakusaidii wafiwa, wala aliyefanya kosa.

Kutopata huduma unayostahili popote pale huumiza.

Usipotibiwa vyema hospitali, bila kujali matokeo yake kama utapona au utakufa huumiza. Ukiporwa uwanja utaumia. Ukifungwa kwa kusingiziwa utaumia. Ukibambikiwa kesi ya uhujumu uchumi vivyo hivyo utaumia. Bahati mbaya yote hayo yanaweza sababisha kifo.

Binafsi nikiona matukio kama haya, hutumia muda huo kujitafakari jinsi ninavyotoa huduma kwa wateja wangu, maana nami ningependa nikienda sehemu fulani kupata huduma, nihudumiwe vizuri na kwa haki.
 
Back
Top Bottom