Waliohudhuria Kongamano/fursa wizara y mambo ya nje

geek01

Senior Member
Jul 11, 2017
143
267
Habari wanajukwaa, waliohudhuria hii kitu hapa chini tunaomba watupe updates kwani wengine tulikuwa mbali, je yapi yalifanyika?


TAARIFA KWA VIJANA

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inatoa mwaliko kwa Wajasiriamali, tafadhari wenye nafasi wahudhurie hasa Vijana:

Tukio: Uzinduzi wa kampeni ya Kuhamasisha Vijana wa Kitanzania kutumia Fursa za Biashara zilizopo katika soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki

Tarehe: 14/7/2017
Muda: 02:00 asubuhi hadi 08:00 Mchana
Kauli Mbiu: "Jumuiya ya Afrika ya mashariki inakuletea Fursa lukuki za Biashara na masoko"

Mgeni Rasmi; Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika ya Mashariki

Mahali: Ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIC), Posta, Dar es salaam

Washiriki: Vijana wote wa kitanzania wanafunzi, wafanyabiashara na wanaotaka kuingia kwenye biashara)

Kumbuka: Hakuna kiingilio, Chai, Chakula cha mchana na vinywaji vitapatikana kwenye Ukumbi wa mkutano. Kwa wale wenye bidhaa, nenda na sampuli za bidhaa zako. Ukipata ujumbe huu mwambie na mwingine.

Kila la kheri

"Masoko ya uhakika kwa Maendeleo ya viwanda na kukuza Ajira kwa Vijana"
 
Back
Top Bottom