Wanafunzi waliomaliza la saba mwaka jana walikuwa 943,318 na waliofaulu form six 2019 wako 79,770 hivyo basi watoto wanaomaliza la saba ni chini ya 8% ndio hufaulu form six, kama ni kweli tunahitaji kuangalia hawa waliokomea njiani wako wapi na wanafanya nini kwani hii ndio nguvu kazi ya taifa.
kutokana na matokeo yaliyotangazwa tarehe 20 December 2012 na waziri wa elimu Dr. Shukuru Kawambwa waliofanya mtihani walikuwa 865,534 na waliofaulu kujiunga kidato cha kwanza walikuwa 560,706. Kumbuka hawa ndio waliofanya mtihani kwa utaratibu wa Optical Mark Reader (OMR) maarufu kama mtihani wa kusigina. utaratibu huu ulilalamikiwa kwani wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika waliweza kupata daraja za juu.