Tetesi: Waliohamia CCM kuunga juhudi za hayati Rais Magufuli sasa kurejea kwa kishindo CHADEMA kudai katiba mpya!

Wanatajwa wengi tu kwamba wako mbioni kurejea Chadema baada ya mbeleko waliyoitegemea kukatika

Inasemekana wenye chama hawataki uchotara wanataka kuirudisha CCM katika misingi yake ndiposa makamanda waliofuata vyeo Lumumba wameanza kunyanyapaliwa kuanzia wizarani, Bomani, Mjengoni hadi Chamani.

Kwa kuwa hamna namna makamanda wanawaomba wana chadema wawapokee kama yule mwana " Mpotevu" wa kwenye Biblia.

Mungu wa mbinguni awabariki nyote!

Wana njaa hao wafie huko huko
 
Sijui kama jjmnyika atatoa hiyo nafasi ya wasaliti kurudi cdm
Mkuu ni hivi:

Mboa walimpokea Lowassa waliyem-brand #fisadipapa? Politics are never certain.

Inapofika kwenye critical issues za kimkakati Secretary General is nothing tena hashirikishwi bali anapewa order kusubiria mbali huko maamuzi ya vikao nyeti vya siri ili ayatekeleze kama yatakavyomfikia.

Kumbuka kuja kwa Lowassa Chadema Dr. Wilbroad Slaa aliwekwa kando, Mbowe alipanda ndege usiku kwenda Arusha kwenye kikao cha siri usiku wa manane na Edwin Mtei, kesho yake Katibu Mkuu akapewa tu order.

Mnyika na Slaa who is heavyweight? Slaa ni asset kwasababu amewahi kucheza kwenye timu zote mbili za upinzani na chama tawala, Mnyika hana sifa hiyo, hivyo Slaa ni heavyweight over Mnyika. Slaa ana international recognition kwa status yake ya VIP/Diplomat ukiachilia ile nafasi yake ya zamani ya TEC. Ni vivyo hivyo kwa Maalim, ni heavyweight kuliko the novice Mnyika, lakini Lipumba amewahi kufanya vikao nyeti bila kumuhusisha. Horace Kolimba alikuwa sidelined na CCM na ukawa ndiyo mwisho wake. Dr. Bashiru Ally bado Political Odyssey yake iko fresh kwenye kumbukumbu zetu. Dr. Mashinji yuko wapi? Ameenda alikoenda Dr. Slaa na huenda Mnyika naye akawafuata huko kama mambo yakikorogeka Chadema. Hivyo Secretary General wa chama ni Political Martyr kuliko any post kwenye chama.

Lakini Mkuu, ukumbuke hao migrants wanapokuja kwenye vyama huwa wako extremely strategic, wanafanya ujasusi na utafiti kwanza wa kutosha kubaini viongozi wakuu na mabaraza ya wadhamini ya vyama hivyo wanavyotaka kuhamia wana udhaifu na uhitaji kwenye maeneo gani? Yaani chama kina njaa ya nini: Wafuasi? Mgeni anayeweza kukivusha chama? Au Pesa?

Mrema alienda TLP na mamia ya wafuasi na NCCR kikapinduka chali kama mende. Lowassa alipeleka Chadema maelfu ya wafuasi na ofisi ya chama, Sumaye na Mahanga walipeleka Chadema pesa za kutosha, Maalim alipeleka ACT Wazalendo maelfu ya wafuasi na ofisi za chama Znz nzima.

Economics of Politics matter than anything else!
 
Back
Top Bottom