Waliogombea uhuru wangekuwa na mawazo haya!!!! Tungekuwa bado Tanganyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waliogombea uhuru wangekuwa na mawazo haya!!!! Tungekuwa bado Tanganyika

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ngambo Ngali, Sep 5, 2010.

 1. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  [​IMG]







  Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Jakaya Kikwete ameshangazwa na Wapinzani kwa kushindwa kuishukuru serikali ya CCM hata kwa jinsi ilivyowasomesha na badala yake wamekuwa wakiiponda kuwa haijafanya kitu tangu nchi ipate uhuru.
  Alitoa kauli hiyo jana wilayani Morogoro Vijijini katika jimbo la Morogoro Kusini alipowahutubia maelfu ya wananchi waliofika kumsikiliza.
  Alisema hawajawahi kuona wapinzani wasiokuwa na shukrani hapa nchini na kwamba kila kitu kilichofanywa na CCM kwao wanakiponda na kushindwa kutoa asante kidogo.
  Alisema serikali ya CCM wanayoiponda imewajengea barabara za lami katika majimbo yao lakini kitu cha ajabu hawalioni hilo na kwamba wanachojua ni kuponda kila kitu. “Hawa wapinzani ni watu wa ajabu wao kila kitu wanaponda hata vile ambavyo vinaonekana kwa macho,” alisema.


  Source:Nipashe Jumapili


  Kwa sababu wamesomeshwa basi wasiseme ukweli????? Kukaa kimya ni usaliti, kwenye mapungufu lazima waseme. Na anayesema ukweli ni wa kupongezwa sio kubezwa.



  kadri miaka inavyokwenda utakuja ona kuwa wengi wa watu wanaosomama majukwaani hawakusomeshwa na CCM bali ni kizazi cha kwanza cha shule za St. ...........
   
Loading...