Waliofukuzwa Udiwani Arusha Wawa Kivutio Mkutano Wa RC


PakaJimmy

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Messages
16,231
Likes
351
Points
180
PakaJimmy

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2009
16,231 351 180
Madiwani watatu kati ya wa5 waliofukuzwa uanachama kutokana na mgogoro wa uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Arusha, jana walikuwa kivutio katika mkutano wa Utambulisho wa Mkuu Mpya wa Mkoa wa Arusha Magessa Mulongo, uliofanyika katika bwalo la Polisi jijini Arusha, baada ya kujitambulisha kwa Nyadhifa zao licha ya kutoalikwa.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha Estomih Chang'a alisema ofisi yake haikuwaalika madiwani waliofukuzwa kutokana na uamuzi wa mahakama.
"Tayari nimemwagiza Mwanasheria wa Manispaa kufuatilia nakala ya hukumu hiyo ili nimwandikie Waziri husika kuomba maelekezo ya kinachofuata.
Leo sijawaalika na hata kwenye kikao cha Baraza kilichofanyika baada ya hukumu ya mahakama sikuwaruhusu kuhudhuria, labda wamekuja kama wananchi wa kawaida na wadau wa maendeleo"
alisema Chang'a.

Aisema ofisi yake haiwezi kuendelea kuwakumbatia au kuwatambua baada ya uamuzi wa mahakama iliyokataa kuwarejeshea uanachama wa Chadema.

Awali, Madiwani hao watatu walijitambulisha mkutanoni hapo bila kutarajiwa, ambapo Estomih Malla alijitambulisha kuwa ni Diwani wa kata ya Kimandolu, na Rehema Mohamed Diwani wa viti Maalum, akimalizia John Bayo ambaye alisema kuwa ni Mwenyekiti wa serikali ya mtaa kwenye kata yake.

SOURCE: Gazeti la Mwananchi Alhamisi, Sept 29, 2011.

My take:
Aibu kubwa hii!
Kwanini kujidhalilisha?...Kwa nini unaruhusu masikio yakue na kukipita kichwa, wakati unajua mbele giza?...Pole zao!
 
Raia Fulani

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Messages
10,217
Likes
110
Points
145
Raia Fulani

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2009
10,217 110 145
nadhana mwandishi alikosea taito. Walikuwa kichekesho
 
Mlachake

Mlachake

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2009
Messages
3,416
Likes
1,324
Points
280
Mlachake

Mlachake

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2009
3,416 1,324 280
kwa wale wapenda coomedies kama mimi, Nafikiri mtakua mmewatch Sinema ya Mr. Bean by the tittle ''JOHN ENGLISH''

You remember what were mr. bean (John English) on agent ones' Status?

Thats tells all.
 
Filipo

Filipo

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2011
Messages
9,322
Likes
226
Points
160
Filipo

Filipo

JF-Expert Member
Joined Jan 6, 2011
9,322 226 160
Hao jamaa kuna thread hapa ilisema wameamua kugombea tena kupitia nccr. Kwahiyo watakuwa wanauzauza sura maana wanaelekea kupotea kwenye ulingo wa siasa.
Othewise ni ulevi wa madaraka. Hawaamini kama walishavuliwa uongozi!

Aibu iliyowapata ni malipo ya ubaya. Siku zote mwisho wa ubaya ni aibu!
 
Mzee

Mzee

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Messages
13,430
Likes
3,484
Points
280
Mzee

Mzee

JF-Expert Member
Joined Feb 2, 2011
13,430 3,484 280
Tatizo la viongozi wenye IQ ndogo. Wanashindwa kufikiri kabla ya kutenda, wanatenda ndipo wanafikiri. Shame on them.
 
Angel Msoffe

Angel Msoffe

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2011
Messages
6,796
Likes
87
Points
145
Angel Msoffe

Angel Msoffe

JF-Expert Member
Joined Jun 21, 2011
6,796 87 145
Kweli aisee hawa jamaa walifanya mambo mema sn mpaka wanakuwa kivutio kwa jamii.
 
MVUMBUZI

MVUMBUZI

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2011
Messages
5,074
Likes
806
Points
280
MVUMBUZI

MVUMBUZI

JF-Expert Member
Joined Jan 8, 2011
5,074 806 280
Nimeambiwa juzi kwamba Estomihi Mallah anataka kuhama anakoishi Kimandolu baada ya kushindwa kupita mitaani mchana.
Sisi wa kimandolu mbona huyo diwani aliyejitambusha hatambuliwi kabisa sisi tunasubiri uchaguzi wa madiwani. Ni huyu huyu kwenye sikukuu ya mashujaa alijitambulisha kama Naibu meya wa manispaa ya arusha na kupiga picha ili awepo katika kumbukumbu za historia ya manispaa ya Arusha.
 
J

jigoku

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2011
Messages
2,397
Likes
127
Points
160
J

jigoku

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2011
2,397 127 160
Njaa haina adabu,kwani huko nikijidhalilisha,ni kwanini wanalazisha kuongoza?nadhani hiyo ni kushindwa kuikakbili njaa,na hii ndo imetufikisha hapa watanzania,kwani Mibunge yetu mingi huwa inapayuka ndio ili tu isije enguliwa kwa kuonekana wanakwend kinyume na matakwa ya wakubwa,hivyo utakutana na Ndioooo, nyingi kule Dodoma.na ndio hizi hata kama zinawakandamiza wapiga kura bado huwa hawaangalii,mfano huu ni dhahiri hata kwa hawa madiwani walioenguliwa,wanaendelea kujipendekeza kama waheshimiwa madiwani wakati wala watu hawana mpango nao,nadhani waliingia Chadema bila kujua uongozi uko imara kiasi gani,walidhani unafiki wa CCM uko hata Chadema,hivyo walidhani kupoteza madiwani watano itakuwa ni vigumu,kumbe kwenye ukombozi wa kweli hata kama ni wote bado wangeenguliwa.Hao ni njaa jamani kwani hawafikirii hata damu na roho za watu zilipotea Arusha,angalia leo wanabaki kujipendekeza mara kujionyesha onyesha.
Ushauri wa bure waende CCM,na wajiandae kugombea tena,si hata kilanja mkuu alikuwa anawatetea pamoja na Mkuchika?
Wanakula unafiki wao sasa wajifunze kuvumilia.
 
PakaJimmy

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Messages
16,231
Likes
351
Points
180
PakaJimmy

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2009
16,231 351 180
Kweli aisee hawa jamaa walifanya mambo mema sn mpaka wanakuwa kivutio kwa jamii.
Una mfano wa mambo hayo ututajie?

Kilichobaki kwa hawa jamaa kwa sasa ni kujichomeka mahala popote penye kusanyiko , ili watu wawaonee huruma.
Nasikia wakazi wa kata za huko watokako hata wakiwa na Ubarikio madiwani hao wanahudhuria, hata bila kualikwa...Ni kama wamepagawa, na wanatia huruma sana!
Ama kweli Majuto ni mjukuu!
 
MAGEUZI KWELI

MAGEUZI KWELI

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2011
Messages
1,946
Likes
25
Points
145
MAGEUZI KWELI

MAGEUZI KWELI

JF-Expert Member
Joined Jul 16, 2011
1,946 25 145
Njia ni nyembamba wapitao ni wachache wenye nia safi na wanao ogopa Hukumu ya mwisho. Waliiona Chadema kama Daladala ya Kwenda Mbagala Siyo....????
 
K

Kingu Victor EL

Member
Joined
Aug 21, 2011
Messages
26
Likes
0
Points
0
K

Kingu Victor EL

Member
Joined Aug 21, 2011
26 0 0
Uchaguzi mdogo unakuja. Hawa walipendwa sana na ccm na serikali yake. Nadhani itakuwa busara kwa ccm na serikali yao kuwachukuwa hawa na kuwasimamisha kwenye uchaguzi kwa tiketi ya ccm ili wajipatie ushindi wa kishindo. Waziri ------------ upo hapo?
 

Forum statistics

Threads 1,249,419
Members 480,661
Posts 29,697,547