abudist
JF-Expert Member
- Oct 25, 2009
- 850
- 780
Rais anawachanganya watu kwa kauli zake za kinafiki.
1) Hotuba ya Rais September 26, 2016 bandarini Dar es salaam, na-nukuu ''Yule mwenye vyeti vya forgery ataondolewa kwenye nafasi yake. Wewe uliyepeleka cheti chako ukasema mimi ni kuli nilimaliza darasa la saba unabaki na kazi yako'' Mwisho wa kunukuu.
2) Hotuba ya Rais leo tarehe 03 October, 2017. Na-nukuu ''Na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam alivyojaribu kuzungumza kidogo, vita ikawa kubwa kwake, hajasoma hajafanya nini...mimi hata hajui 'Aaa' mradi anashika madawa ya kulevya huyo ni msomi mzuri. Kwani wenyeviti mliopo hapa wote mmesoma?'' Mwisho wa kunukuu.
Sasa wale wafanyakazi wote waliofukuzwa kazi kwa kughushi vyeti ingawaje walikuwa wanafanya kazi zao kwa ufasaha waende mahakamani. Kwa kauli hii ya leo ya Rais Magufuli ina maana wanaweza kurudishwa kazini kwa kifungu cha kubaguliwa na kutotendewa haki. Kwa sababu makosa hayo hayo waliyokutwa nayo sheria imepindwa kumlinda RC wa Dar, kwa kutumia amri ya Rais na siyo ya sheria ya nchi. Wanasheria angalieni hili wasaidieni waliofukuzwa kazi kwa ushahidi huu wa kauli za Rais mwenyewe kesi mtashinda.