Waliofariki mkasa wa moto London wafika 30

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
_96512710_040077081-1.jpg

Polisi wamethibitisha kwamba idadi ya watu waliofariki kutokana na mkasa wa moto katika jumba la Grenfell Tower magharibi mwa London imefikia 30.

Bado kuna watu wengi ambao hawajulikani walipo.

Kamanda wa polisi Stuart Cundy amesema inaaminika kwamba idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka, lakini kwa sasa ni vigumu sana kubaini ni watu wangapi ambao hawajulikani walipo.

Hii ni kwa sababu huenda jamaa wamepiga ripoti mara kadha, kila mmoja kivyake, kuhusu jamaa zao ambao hawajui waliko.

Amesema polisi watachunguza kubaini iwapo kulitendwa makosa ya jinai.

Malkia Elizabeth na Mwanamfalme William walitembelea kituo cha misaada ambacho kinawasaidia manusura wa mkasa huo wa moto.

Waziri Mkuu Theresa May naye amezungumza na majeruhi hospitalini, baada yake kukosolewa kwamba hakuzungumza na wakazi alipozuru eneo la mkasa Alhamisi.

Moto huo ulizuka mwendo wa saa moja usiku, usiku wa kuamkia Jumatano.

_96512710_040077081-1.jpg
Haki miliki ya pichaEPA
Image captionMaafisa wamesema hawatarajii kuwapata manusura
Mada zinazohusiana

Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako
Rejea mwanzo wa ukurasa
Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii
Habari kuu
Trump akiri kwamba anachunguzwa Marekani
Rais wa Marekani Trump amethibitisha kwamba anachunguzwa yeye binafsi kutokana na hatua yake ya kumfuta kazi mkuu wa Shirika la Uchunguzi wa Jinai la Marekani FBI James Comey.

16 Juni 2017

Urusi yadai kumuua kiongozi wa IS Abu Bakr al-Baghdad
16 Juni 2017

Mji wa kale wa ‘majitu’ yagunduliwa Ethiopia
16 Juni 2017

Gumzo mitandaoni

Je uko tayari kuambukizwa ugonjwa kwa malipo ya pauni 3,526?


Waziri mkuu Australia amkejeli rais wa marekani Donald Trump


China kupanda viazi kwenye Mwezi


Gari lenye kasi zaidi duniani kujaribiwa Oktoba

http://www.bbc.com/swahili/habari-40246200
 
Pole zao sana ,ingekuwa India au Uarabuni wanakozaliana kama mchwa wangekufa wengi sana katika hilo jengo moja
 
Mimi nimejifunza kuwa kama kwa wenzetu ambapo kuna sheria lukuki za usalama hili limetokea, hapa kwetu ukitokea moto twafa. Ni kazi ya Mungu tu halafu basi!
Ni kweli mkuu...pia nilitegemea mpaka sasa watu wa fire department wawe wameshatoa muongozo kwa wamiliki wa majengo warefu wafanye majaribio tena ya fire detectors zao na kuhakikisha mifumo yote inafanya kazi vizuri..
 
Back
Top Bottom