Waliofariki dunia Loliondo wafikia 78 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waliofariki dunia Loliondo wafikia 78

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Saint Ivuga, Apr 5, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,270
  Likes Received: 19,413
  Trophy Points: 280
  Waliofariki dunia Loliondo wafikia 78 Send to a friend Monday, 04 April 2011 22:40 0diggsdigg

  Neville Meena na Mussa Juma, Samunge
  IDADI ya watu waliopoteza maisha wakienda kupata tiba ya magonjwa sugu kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapila katika Kijiji cha Samunge, Loliondo Wilaya ya Ngorongoro, mkoani Arusha imefikia 78.Habari ambazo Mwananchi limezipata na kuthibitishwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Dominick Lusasi jana zinasema idadi ya vifo hivyo ni ile iliyorekodiwa kuanzia Machi 11, mwaka huu.
  "Kati ya Machi 11, mwaka huu tulipoanza kuchukua rekodi za waliokufa na Machi 29, watu 74 walikuwa wamethibitishwa kufariki dunia, lakini hivi karibuni nilipata taarifa kwamba watu wengine wanne wamefariki," alisema Lusasi.
  Hata hivyo, idadi hiyo inaweza kuwa ndogo kuliko uhalisia kwani upo uwezekano mkubwa kwamba wapo waliofariki dunia na vifo vyao havikurekodiwa tangu watu walipoanza kufurika Samunge mwishoni wa Januari ,mwaka huu hadi Machi 11, 2011 utunzaji wa kumbukumbu ulipoanza.

  Kwa mujibu wa uongozi wa Kijiji cha Samunge, watu 19 wamelazimika kuzikwa kijijini hapo kutokana na ama maiti kukosa ndugu au ndugu kutokuwa na uwezo wa kusafirisha maiti hivyo kuomba msaada wa Serikali.

  Majina ya waliofariki Miongoni mwa waliopoteza maisha ni mke wa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mama Parceko Vincent Kone (55), watoto saba akiwamo mtoto wa miaka miwili, Bokye Mwilenyi Magoli, mkazi wa Kyang'ombe, Wilaya ya Rorya, mkoani Mara aliyefariki dunia Machi 25, 2011 sambamba na wagonjwa wengine 10 waliofariki dunia siku hiyohiyo.

  Taarifa ya Idara ya Afya ya Halmashauri ya Ngorongoro inawataja watoto wengine waliofariki dunia wakiwa Loliondo kuwa ni Fatma Hussein (5), mkazi wa Msambi - Kileche, Mwanga, Kilimanjaro; Athumani Omari (7), mkazi wa Ntiko, Singida; Tumaini Samson (10), mkazi wa Sengerema, Mwanza; Lesian Yuton (12) mkazi wa Dodoma Mjini na Jescar John (16) wa Dar es Salaam.

  Mtoto mwingine aliyefariki dunia ni raia wa Kenya, Maximilian Shuku (12), mkazi wa Narok na raia mwingine wa nchi hiyo, Nori Makati (46) ambaye ni mkazi wa Usupuko.Kwa mujibu wa taarifa hiyo, siku inayoongoza kwa vifo vingi ni Machi 24, 2011 ambayo watu 15 walipoteza maisha, ikifuatiwa na Machi 25 ambayo ilishuhudia wagonjwa kumi na moja wakifariki dunia hivyo kufanya jumla ya waliopoteza maisha kwa siku hizo mbili tu kufikia 26.
  Majina ya watu wengine waliofariki dunia, umri na wanakotoka katika mabano ni Hassan Ally Tarimo (38- Moshi Mjini), Agness Costantine (43-Singida Mjini), Alex Godii (45 - Mererani, Manyara), Masinyari Nuhu (80 - Engaruka, Monduli), Daudi Shanu (31 -Moshi), na Holo
  Nigha (40 - Kishapu, Shinyanga).

  Wengine ni Grace Somi (59 -Moshi Mjini), Eva Sumaye (65 - Lekamba, Arusha), Hadija Wambura (30 - Tarime, Mara), Juma Ally (45 - Tanga), Fatuma Shaban (54 - Ngara, Kagera), Mrs Moshi (60 - Msagara, Moshi), Donald Msele (47 - Misungwi, Mwanza) na Mama Ndossi (70 - Bomang'ombe, Moshi). Wengine ni Okonbo Oguyi (78 - Musoma Vijijini), Stella Hagai (43 - Dar es Salaam), Diana Munisi (20 -Hai, Moshi), Flora Assenga (42 - Chumbageni, Tanga), Steward Mgosingwa (86 -Muheza, Tanga), Shanuel Mushi (22 - Lyamungo, Hai), Penina Wiga (38 - Shirati, Rorya) na Mwajuma Ramadhani (72 - Dodoma Mjini).

  Margaret (35 - Rorya, Mara), Eliashenya Bilingi (78 - Meru), Steven Haule (53-Majengo, Tabora), Mary Sindani (38 - Manyoni, Singida), Ngangi Nana (70-Milima Meru), Kabula Kazungu (24 - Nyanguge, Magu), Elizabeth Emmanuel (74 - Arusha) na Jaston Kusoma (35 - Katesh).

  Norbert Kudome (33 - Moshi), Philipo Jalo (35 - Mwanza), Stella Mwanyemba (42 -Busali, Kyela), Haikaeli Msocha (62 -Mlalo, Lushoto), Joy Rose (36 - Msanga, Chamwino), Hamis Kazyoba (70 - Kahama, Shinyanga), Mjaledi Munka (65 - Makete, Iringa), Esther Rutainyu (49 - Biharamulo) na Mwanahamis Rajabu (32 - Tabora Mjini).
  Katika orodha hiyo pia wamo, Mwanaisha Isaka (70 - Dodoma Mjini), Rehema Sadalla (30 - Kiteto, Manyara), Emmanuel Napengwa (68 - Ilala, Dar es Salaam), Amina Kimweri (62 - Makanara, Korogwe), Butondo Mbuje (26 - Manyoni, Singida), Elise Mandari (76 - Mamba Kusini, Moshi), Jonathan Mnyiremi (Sorya, Manyoni) na Elisaria Urio (50 - King'ori Arumeru).

  Wengine ni Shafu Muya (30 -Korongoni, Moshi), Paschal Shaghembe (47 - Geita Mjini), Bertha Muro (78-Machame, Hai), Lucas Machimo (56 - Ugogoni, Korogwe), Magdalena Kalole (35- Kimara, Dar es Salaam), Charya Mashishi (45 - Usanga, Maswa), Josephine Robert (34-Murukurazo, Ngara), Asha Nkinda (65 -Tanga Mjini) na Lyidia Msuya (78 - Kimara, Dar es Salaam).

  Wagonjwa wengine waliofariki ni Paulina Portea (65 - Ganako, Karatu), Alemwene Mwakatobe (69 - Mwanjelwa, Mbeya), Marieta Mandwa (56 - Shinyanga), Masalu Nhelegani (65-Nyangokolo, Bariadi), Emmanuel Mang'arai (56 - Arusha), Amina Chuwa (86 - Uru, Moshi), Eliadi Mariki (40 - Mwika, Moshi Vijijini) na Mmoja Juma (25 - Bukumbi, Tabora).

  Mwishoni mwa wiki iliyopita, Mwananchi lilishuhudia baadhi ya watu katika Kijiji cha Samunge wakiwa wamebeba maiti ya mwanamke aliyetambuliwa kwa jina la Rukia Rajab, Mkazi wa Kondoa wakati majina ya watu wengine wanne waliofariki dunia bado hayajatambuliwa.Kadhalika, mmoja wa maiti ambazo majina yake hayakutambuliwa alifahamika kuwa ni mkazi wa Biharamulo, mkoani Kagera.

  Sababu za vifo
  Lusasi alisema kwa mujibu wa taarifa za madaktari, vifo vingi vimesababishwa na magonjwa ya kisukari, pumu na shinikizo la damu. "Wagonjwa wengine walikuwa wakifika Samunge unamwangalia na kumwona kuwa huyu alikuwa amewekewa drip, lakini yuko pale akiwa kwenye foleni akisubiri kwenda kwa Mchungaji kunywa dawa," alisema Lusasi na kuongeza:
  "Sasa katika hali hiyo kama mgonjwa ni wa kisukari, wengi walipoteza maisha kwani hata vyakula walivyokuwa wakila pengine havikuwa vikikidhi matakwa ya ugonjwa husika."Alisema katika kukabiliana na hali hiyo, waliimarisha huduma za afya katika Zahanati ya Kijiji cha Samunge kwa kuongeza watumishi wa afya na dawa za magonjwa hayo lakini akasema watu walikuwa hawajitokezi hadi pale hali zao zilipozidi kuwa mbaya.

  Alisema zahanati hiyo pia imekuwa ikipewa mgawo mkubwa wa dawa nyingine kutokana na kuongezeka kwa mahitaji na idadi ya wagonjwa kuongezeka.Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi kwa siku kadhaa umebaini kuwa baadhi ya wagonjwa walichukua dawa za siku chache wakitaraji kwamba wangetumia muda mfupi kupata kikombe cha Babu, lakini kinyume chake walijikuta wakikaa kwenye foleni kwa muda wa kati ya siku saba na kumi na moja.

  Kutokana na kuwapo kwa dalili za tiba ya Mchungaji Mwasapila kuendelea kwa muda mrefu, Lusasi alisema Halmashauri ya Ngorongoro inakusudia kujenga chumba kidogo cha kuhifadhia maiti katika Zahanati ya Samunge ili kukabiliana na tatizo la maiti kuzikwa kabla ya ndugu zao kufika kuwachukua.

  Alisema sababu nyingine iliyochangia vifo hivyo ni kuzibwa kwa barabara kiasi kwamba gari la wagonjwa lililopelekwa na halmashauri kushindwa kuwasadia wale waliokuwa wamezidiwa."Gari lile mara kadhaa lilijaribu kupenya, lakini lilishindwa kutokana na watu kukataa kulipa nafasi, tulijaribu kila njia, kuweka mabango kwenye gari, kuweka bendera na hata kutumia kipaza sauti kutangaza lakini ilishindikana," alisema Lusasi
   
 2. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2011
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,366
  Likes Received: 661
  Trophy Points: 280
  Asante kwa taarifa!!
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,270
  Likes Received: 19,413
  Trophy Points: 280
  sourrce:
  mwananchi.co.tz
  washukuru wao
   
 4. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  There oughta be regulations against this nonsense.
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,270
  Likes Received: 19,413
  Trophy Points: 280
  who gonna impose those regulations?Maghufuli,Lowasa,Pinda,or KKT
   
 6. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  na wangapi hufa kila siku kabla ya kumuona daktari?
   
 7. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Wangapi hufa kwa siku kutokana na ajari au uzazi???
   
 8. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,930
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo unapigana kuhalalisha vifo vya Samunge?
   
 9. s

  sawabho JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Katika Tanzania nzima ni wangapi hufa wakiwa njiani kwenda hospitali? Maana hapa tatzizo sio watu kufa baada ya kunywa dawa ila wakiwa katika harakati za kwenda. Na mbona hatujiulizi ni kwa nini wanenda Samunge hata kama wanasikia barabara haipitiki, kwa mawazo yangu ni kwamba wamekata tamaa, hawana imani na huduma ya huko watokako.
   
 10. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  tena hasa hospital ya taifa muhimbili............
   
 11. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #11
  Apr 5, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Toa data ya wanaokufa kila siku Muhimbili...
   
 12. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #12
  Apr 5, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Regulations are in place.
   
 13. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #13
  Apr 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Wagonjwa 50 hufariki kila siku Muhimbili Hospitali kabla ya kumuona daktari...
   
 14. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #14
  Apr 5, 2011
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,648
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Nia ya kumruhusu "babu" aendelee kugawa dozi ni kupunguza msongamano wa wagonjwa mahospitalini na maambukizi ya magonjwa hatari kama ukimwi na kwa ujumla gharama kubwa za kuhudumia Wagonjwa, ambazo ni mzigo kwa Serikali na hata Wanandugu. Kwa mantiki hii, wakifa watu wengi zaidi, the better.

  Ndiyo maana mnaona Serikali inaruhusu moronic scam kama hizi. How else would otherwise very rational, well-learned big shots in the Govt flock to Loliondo kila kukicha na picha zao kutolewa waziwazi? Obviously, wanategemea maelfu ya watu wafuate mkumbo na wazidi kwenda ile waangamie wengi zaidi. In the meantime, "babu" keshakuwa millionaire wa Tshs many-times over, and there's apparently no end in sight to this madness. Ndiyo kwanza Magufuli ana-pledge Tshs Bilioni moja kutengeneza barabara ya kwenda kwa "babu".
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Apr 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,270
  Likes Received: 19,413
  Trophy Points: 280
  kila siku au kila saa?
   
 16. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #16
  Apr 5, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  hapo haijajumlishwa wale wanaokufa baada ya kurudi majumbani mwao na illusion kuwa wamepona na kusitisha dawa.

  huyu babu KISHAMFUNIKA KIBWETERE kwa mauaji ya watu wasio na hatia waliomkimbilia kwa kutoijua kweli
   
 17. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #17
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Iwe Loliondo, Barabarani au Hospitali, iwe wanakufa kwa kisukari, uzazi au malaria, maisha ya Watanzania yanapotea kwa wingi kila siku na tumeshindwa kuandaa sera ya kuwapatia matibabu.
  Pengine wapo watakaodai kuwa kifo ni kazi ya Mungu, hivi Mungu yupo katika nchi zinazoendelea tu? Kwa nini wastani wa kuishi nchi zilizoendelea (miaka 80) ni mkubwa kuliko nchi masikini miaka 45?
   
 18. LD

  LD JF-Expert Member

  #18
  Apr 5, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mmmmh, Mungu saidia, afadhali kufia hospitalini, au kwa ajali, kuliko porini Samunge. Hata kuwapa wajukuu historia, babu yenu alifia Samunge kwa mganga wa jadi anayetumia kikombe kutibu, haileti, bora hata nikafia kanisani kuliko huko.....ni mm tu najiwazia hivo.
   
 19. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #19
  Apr 5, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  ...Watanzania tuna tabia ya usahaulifu kama KUKU (actually ni utamaduni wa uzembe tu).
  Tukumbuke jambo la msingi kwamba Babu anapokea wagonjwa kutoka TANZANIA NZIMA. Kwa hiyo, kabla ya 'kudai kwamba eti watu wengi wanakufa kwa Babu tujiulize:

  1. Tanzania kuna hospitali, vituo vya afya na zahanati ngapi?
  2. Je, watu wangapi wanakufa katika hizi zahanati, hospitali, vituo vya afya na majumbani KILA SIKU? - Hiyo zahanati ya mtaani kwako hapo je?
  3. Ni wagonjwa wangapi NA WENYE HALI GANI wanaokwenda kwa Babu?
  4. Je, hao wagonjwa wote (wengi wao mahututi, or with terminal illnesses) wangepona kama wangebaki kwenye zahanati na hospitali zisizo na dawa, na zenye huduma mbovu? au kwa sababu kila mtu anafiwa na mtu wake mmoja, basi inakuwa siyo ishu?

  Survey ndogo tu kwenye mortuary za hospitali za Mikoa na Wilaya inatosha kufichua hali halisi ilivyo mbaya katika zahanati na hospitali za Tanzania.
   
 20. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #20
  Apr 5, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Pale Muhimbili wafu 78 kwa siku si ajabu tena wengine kwa uzembe kabisa. Hata kama hiyo dawa ya babu haiponyi basi itasaidia kuweka wazi uozo wa huduma za afya za Tanzania ya CCM. Nani angeenda huko loliondo kama kungekuwa na huduma makini za afya?
   
Loading...