Waliochota Stanbic hawa: Mke wa kigogo Ikulu atajwa

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
14,880
2,000
MAJINA ya baadhi ya watu walionufaika na fedha za akaunti ya Escrow zilizowekwa katika akaunti ya Benki ya Stanbic jijini Dar es Salaam yameanza kutajwa, Raia Mwema linafahamu.

Miongoni mwa majina ambayo vyanzo vya gazeti hili vimethibitisha kwamba yapo ni lile la mke wa mmoja wa vigogo wa ngazi za juu Ikulu (jina tunalihifadhi kwa sasa) ambaye anaelezwa kuchukua kiasi cha dola za Marekani milioni tatu (Sh. bilioni tano).

"Tayari tunalo jina la mwanamke mmoja ambaye amefahamika kama mke wa mmoja wa watu wenye vyeo vikubwa Ikulu. Kwa sababu bado mapema kukupa jina kamili, vumilia kidogo hadi kila kitu kitakapokamilika," kilisema chanzo cha kuaminika cha gazeti hili kinachoshiriki kwenye uchunguzi wa suala la namna fedha za akaunti ya Escrow zilivyolipwa kwa watu.

Raia Mwema linahifadhi jina la mwanamama huyo pamoja na mumewe kwa sasa kwa vile kuwataja majina kunaweza kuingilia upelelezi.

Wakati majina ya baadhi ya mawaziri, wanasiasa, majaji na viongozi wa dini yakionekana kulipwa fedha za mgao kutoka katika akaunti moja ya Benki ya Mkombozi, kumekuwa na kitendawili kuhusu ni akina nani hasa walilipwa fedha zilizokuwapo katika Benki ya Stanbic.

Wafaidikaji wengine wa akaunti hiyo ambao gazeti hili limefanikiwa kuwapata kwa sasa ni mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Rajiv Bharat Bhesania, anayetajwa kuwa mojawapo wa wasaidizi muhimu wa mmiliki wa kampuni ya Pan African Power (PAP), Harbinder Seth Singh.

Katika mojawapo ya miamala katika akaunti ya Stanbic iliyofunguliwa na PAP ambayo inaonekana katika ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Bhesania anaonekana kuchukua kiasi cha dola milioni moja (shilingi bilioni 1.6).

Mtu mwingine ambaye inaonyesha amefaidi fedha za akaunti ya PAP ni Mwanasheria wa PAP, Joseph Makandege, ambaye kampuni yake ya sheria ya Bulwark Associates imeonekana kupata malipo yakiwamo ya zaidi ya shilingi milioni 500 kwa nyakati tofauti.

Gazeti hili limefanya mawasiliano na mmoja wa wafanyakazi wa zamani wa IPTL aliyedai kwamba Rajiv pengine ndiye mtu anayefahamu vizuri zaidi mienendo na biashara nyingi zaidi za Sethi na kama Serikali inataka taarifa za mfanyabiashara huyo mtata; basi inapo pa kuanzia.

Ingawa PAC ilipendekeza Sethi akamatwe na kuhojiwa kutokana na tuhuma mbalimbali kama vile utakatishaji wa fedha, kukwepa kulipa kodi na udanganyifu, Raia Mwema limeambiwa kuwa mmiliki huyo wa PAP hayupo nchini kwa sasa.

"Kama Serikali inataka kupata chochote kutoka kwa Sethi inabidi wambane huyuhuyu Rajiv Bhesania. Yeye ndiye kila kitu kwa Sethi hapa Tanzania. Hata akitaka mambo yake yanyooke mahali huwa anamtumia huyu.

"Nafahamu si rahisi kusema kila kitu lakini nafahamu kwamba kama vyombo vya ulinzi vitambana kisawasawa, anaweza kutoa siri zote za Sethi na hatimaye Watanzania wakapata wanachokitaka," alisema mfanyakazi huyo wa IPTL.

Malipo hayo yote yalifanyika katika kupitia katika akaunti namba 912 0000 12 52 94 ambayo ilifunguliwa tarehe 28 Novemba mwaka 2013 na kufungwa tarehe 14 Septemba 2014.

Ni katika benki hii ndiko ambako muamala wenye thamani ya shilingi bilioni 73.5 ulifanyika siku ya Januari 23 mwaka huu; muamala ambao sasa ndio unachunguzwa na vyombo vya ulinzi.

Ni katika siku hii ambapo ripoti za Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na ile ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), zilieleza kwamba kuna watu waliondoka katika ofisi za benki hiyo wakiwa na magunia yaliyojaa fedha.

"Kwa mujibu wa Takukuru baadhi ya watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa (Stanbic) wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi, maboksi, magunia na lumbesa," ilisema sehemu ya ripoti iliyowasilishwa bungeni na PAC.

Muamala huo unachunguzwa vikali na Takukuru pamoja na ule wa Februari, 2014 katika Benki ya Mkombozi jijini Dar es Salaam ambapo kiasi cha shilingi bilioni 3.3 zinadaiwa pia kuchukuliwa kwa siku moja.

Habari za mke wa mmoja wa maofisa wa ngazi za juu wa Ikulu kuhusishwa na uchotaji wa fedha za Escrow inakuja katika kipindi ambacho Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, akidai bungeni kwamba ofisi hiyo ya juu nchini ina mkono katika utolewaji wa fedha hizo kutoka Benki Kuu ya Tanzania.

Wakati akizungumza bungeni, Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, alimtaja Prosper Mbena ambaye ni Katibu wa Ofisi ya Rais (Ikulu), kuwa ndiye aliyeandika barua ya kuruhusu fedha zilizokuwa zimehifadhiwa zitolewe katika akaunti hiyo.

Habari hizi za Stanbic kuhusishwa na fedha za Escrow zimesababisha benki hiyo kumpa uhamisho aliyekuwa Meneja wake, Paul Omara, ambaye sasa anadaiwa kurejeshwa nchini Uganda.

Omara anaelezwa kuitumikia benki hiyo kwa muda wa miaka zaidi ya 11 na Raia Mwema limeelezwa kwamba ofisa huyo tayari amehojiwa na Takukuru kuhusu suala hilo kabla hajaondoka.

Mmoja wa maofisa wa Takukuru aliyezungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa jina kwa maelezo kwamba uchunguzi unaendelea, alisema wamepata ushirikiano mzuri kutoka Stanbic na kuna uwezekano kwamba " watu watakula Krismasi wakati tayari Takukuru ikiwa imemaliza kazi".

Suala la fedha za Escrow lililiteka Taifa wiki iliyopita na sasa wananchi wanasubiri kwa hamu hatua itakayochukuliwa na serikali kuhusu vigogo wanaotajwa kusaidia kutokea kwa kashfa hii.

Chanzo:Raiamwema

Huyu mwanamke ni nani? Na Mumewe ni nani huko ikulu
 
frema120

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
5,099
1,195
MAJINA ya baadhi ya watu walionufaika na fedha za akaunti ya Escrow zilizowekwa katika akaunti ya Benki ya Stanbic jijini Dar es Salaam yameanza kutajwa, Raia Mwema linafahamu.
Miongoni mwa majina ambayo vyanzo vya gazeti hili vimethibitisha kwamba yapo ni lile la mke wa mmoja wa vigogo wa ngazi za juu Ikulu

- See more at: Raia Mwema - Waliochota Stanbic hawa

Huyu mwanamke ni nani? Na Mumewe ni nani huko ikulu

mbona naona hakuna majina au.
 
babagodi

Senior Member
Sep 16, 2014
147
195
MAJINA ya baadhi ya watu walionufaika na fedha za akaunti ya Escrow zilizowekwa katika akaunti ya Benki ya Stanbic jijini Dar es Salaam yameanza kutajwa, Raia Mwema linafahamu.
Miongoni mwa majina ambayo vyanzo vya gazeti hili vimethibitisha kwamba yapo ni lile la mke wa mmoja wa vigogo wa ngazi za juu Ikulu

- See more at: Raia Mwema - Waliochota Stanbic hawa

Huyu mwanamke ni nani? Na Mumewe ni nani huko ikulu

Huu uandishi wenu haufai.utafikiri magazeti ya udaku, uhusiano Wa heading na contents ni asilimia 0-10.haaaag mnaboa.
 
MESTOD

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
4,787
2,000
Kwa nini wasipate uhakika Nipo wariport? Hata mimi ningesema hayo hayo, si sijataja jina?
 
Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
2,000
Mawio hawajafikia weledi wa kiuchunguzi wa -----------.
----------- wangeshatujuza A-Z
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,599
2,000
MAJINA ya baadhi ya watu walionufaika na fedha za akaunti ya Escrow zilizowekwa katika akaunti ya Benki ya Stanbic jijini Dar es Salaam yameanza kutajwa, Raia Mwema linafahamu.
Miongoni mwa majina ambayo vyanzo vya gazeti hili vimethibitisha kwamba yapo ni lile la mke wa mmoja wa vigogo wa ngazi za juu Ikulu

- See more at: Raia Mwema - Waliochota Stanbic hawa

Huyu mwanamke ni nani? Na Mumewe ni nani huko ikulu

Wajameni namjua huyu Mwanamke aliychota Bilioni 3 za Escrow jinsi alivyo, na pia namjua mumewe wa Ikulu, jinsi alivyo!.
Jee niwatajie ?.

.....
Huyo Mwanamke ni jinsia ya kike na mumewe ni wa jinsia ya kiume!.
asanteni.
Pasco
 
KASHOROBANA

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
3,244
1,500

kumbe pasco sometimes uwa unajifanyaga mpuuzi. ok endelea lkn ujue unajishushia heshima
 
KASHOROBANA

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
3,244
1,500
si nilisema naijua jinsia ya alivyo?!.
Pasco.

DUH HAYA BHANA ILA NLIKUKUBALI SANA PASCO MIDA FULANI. LKN NAONA TANGU UJIUNGE NA KAMBI YA CCM HUSOMEKI KABISA. TUNAKUONA KM UNATUMIWA NA MAFISADI KUYAPAMBA. I THINK BORA UCHANGE ILI TUJIKITE KT OPERATION TOKOMEZA MIccm POPOTE YALIPO
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,004
2,000
Huyu jamaa alishajidharaulisha siku nyingi kwa pumba zake anazoandika. Halafu anajiita eti mzalendo halisi!!

kumbe pasco sometimes uwa unajifanyaga mpuuzi. ok endelea lkn ujue unajishushia heshima
 
Jungumawe

JF-Expert Member
May 2, 2009
248
225
Wajameni namjua huyu Mwanamke aliychota Bilioni 3 za Escrow jinsi alivyo, na pia namjua mumewe wa Ikulu, jinsi alivyo!.
Jee niwatajie ?

.....
Huyo Mwanamke ni jinsia ya kike na mumewe ni wa jinsia ya kiume!.
asanteni.
Pasco

Kweli umepatiaje? huyu mke ana nywele ndefu na mumewe ana ndevu
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
43,088
2,000
Uandishi wa aina hii ni wa kushawishi rushwa ili muhusika asije tajwa kabisa.

Anyway,labda ni mashariti kutoka chanzo cha habari yenyewe.
 
Ng'wale

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
3,827
2,000
Wajameni namjua huyu Mwanamke aliychota Bilioni 3 za Escrow jinsi alivyo, na pia namjua mumewe wa Ikulu, jinsi alivyo!.
Jee niwatajie ?.

.....
Huyo Mwanamke ni jinsia ya kike na mumewe ni wa jinsia ya kiume!.
asanteni.
Pasco

Kuna wakati nikiona jina Pasco nilikua navutiwa kusoma comments zako, lakini hivi karibuni kila nikipitia nimekua sioni cha maana. Hii ya leo ndo nimechoka kabisa!!! Hivi mtu unajiita GT unaweza kuandika hayo uliyoandika? Ukikaa kimya sometimes inapendeza na bado watu watatambua uwepo wako. Unless kuna mtu kaingilia ID yako na ameamua kukuchafua.
 
Mtumpole

JF-Expert Member
Aug 30, 2010
2,187
2,000
Wajameni namjua huyu Mwanamke aliychota Bilioni 3 za Escrow jinsi alivyo, na pia namjua mumewe wa Ikulu, jinsi alivyo!.
Jee niwatajie ?.

.....
Huyo Mwanamke ni jinsia ya kike na mumewe ni wa jinsia ya kiume!.
asanteni.
Pasco

Si bora uwe kimya ili ufiche upumbavu wako!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom