Waliochapwa na DC Arusha na kulazimishwa kulipa fedha bila kufikishwa mahakamani waombe msaada wa kisheria kumshtaki DC

Wakienda tu mahakamani wanafunguliwa kesi ya kuhujumu uchumi na mdhamana hawapewi. DPP anahakikisha kesi yao haiishu mpaka watakapokilli makosa yao.
 
Nawaza tu hivi katika wale waliochapwa na mzazi wqngu angekua mmoja wao sijui ningemfanyaje yule mbwa.........kwa kwelii ningefungwa tu jela
Kwangu mimi chaguo la risasi ya polisi lingekuwa bora kuliko kiboko cha dc. Ni pale angelazimisha kunipiga nami ningemsurubu na polisi wake wangenipiga risasi. Maumivu ya risasi ni ya muda mfupi kabla sijakata roho, maumivu ya kunidhalilisha ni ya kudumu mpaka naondoka duniani.
 
Kura???nan kakwambia wanategemea kura kubaki madarakan???
Watu Kama hawa Bwn.DC wanakipa tabu Sana Chama kuomba kura kwa wananchi kipindi cha Uchaguzi.

You can imagine unamchapa mtu halafu huyo huyo unategemea kwenda kumuomba kura 2025.

Hizi ni hujuma kwa Chama na Serikali.

Mamlaka za uteuzi zikemee mambo kama haya.
 
Hao wakaushe tu wakienda mahakamani watageuziwa kibao ohoooo
Na hakuna mtu akataye tokea kuwatetea

Ova
 
Ni miaka karibia mitano sasa viongozi wamekuwa wakijichukulia sheria mikononi na hakuna kiongozi wa kisiasa wa juu anayekemea Jambo linaloashiria wahusika wanatekeleza msimamo wa serikali.

Wahanga wa tukio la Arusha wamelazimishwa kupigwa na kisha kulipishwa fedha zaidi ya milioni tano ambazo taarifa zinadai wamelazimishwa kuuza baadhi ya Mali zao pamoja na ndugu kuwachangia kutokana na vitisho na shinikizo lililotolewa na uongozi wa wilaya dhidi yao.

Uongozi huo ulienda mbali zaidi nakushinikiza kuwafungulia kesi zisizo na dhamana ikiwemo uhujumu uchumi wakiambiwa wamehujumu Mali ya umma na wasipotii nakulipa watawekwa ndani bila dhamana kwa kipindi kisichojulikana. Baada ya vitisho hivyo ambavyo hata vyombo vya habari vimehoji nakujiridhisha kuwepo kwa uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu hakuna chombo kiliripoti ukubwa wa kadhia hii badala yake vyombo vyote vya habari vimesimama na DC na kumfanya DC aonekane kuwa yupo sahihi.

Rai inayotolewa na familia za wahanga nikupata uwakilishi wa kisheria waweze kwenda mahakamani kuomba tafsiri ya kisheria ya kile ambacho wametendewa ikiwa Ni pamoja na kuangalia njia yakupata fidia kwa madhara waliyopata.

Ikumbukwe hata watumwa baada Uhuru kwenye baadhi ya Mataifa walikuja kufungua kesi na mahakama za Dunia wakatoa maamuzi lengo likiwa nikuheshimu utu na haki za binadamu.

Kwa upande wa pili, mkuu wa wilaya kutamka adharani kuwa mchakato wa kisheria dhidi ya watuhumiwa ni kupoteza muda inaleta tafsiri kwamba serikali haiamini Kama muhimili wa mahakama una heshima yake. Kitendo Cha mahakama wakati wote kudharaulika wakakaa kimya nacho kinatia ukakasi.

Niwaombe watu wa haki za binadamu waache kukaa ofisini na kutuletea taarifa za uvunjifu wa haki za binadamu waingie kwenye vyombo vya kisheria nakuwatetea wanaoumia, atutaki takwimu za uvunjifu wa haki tunataka kusikia wamefungua kesi ngapi kutetea wananchi wanaoumizwa na ngapi wameshinda, fidia kiasi gani nk
Kwanza, kwa vile wewe umeona uchungu na kuwatetea wezi, kwa nini usiwe mstari wa mbele kufungua kesi ya kuwatetea? Kesi siyo lazima wafungue wao, hata wewe mkereketwa wa kutetea haki za wezi wizi unaweza kufungua kesi. Pili, huwezi kulinganisha wezi na watumwa. Mwizi ametenda hicho kitendo kwa hiari yake. Hakuna aliyemlazimisha. Mtumwa haamui kuwa mtumwa. Tukiendelea kulea majizi hatutafika. Wewe unadai haki ya ya majizi, je haki ya watoto kupata elimu wewe unaiona vipi. Je, wewe mwizi akikuingilia nyumbani kwako, ukatoka na mkuki, fimbo, mishale, au bunduki utaanza kwanza kufikiria haki ya mwizi kupelekwa mahakamani na si kumtungua kwa mkuki. Mwizi siyo wa kutetewa, maana ukimkurupusha ni ama wewe au yeye. Mimi sina huruma na majizi, hasa pale yanapokuwa yamekamatwa na ushahidi. Ukiyabembeleza majizi yataendelea kukuibia. Kama sera ya CHADEMA ni kubembeleza wezi na mafisadi, sioni kama mna huruma na maskini wa TZ.
 
Bwana wako mzalendo namba moja amemchukulia andrew chenge yule aliyepiga pesa za rada hatua gani!? Kweli wendawazimu nyie mnachagua wa kuwashughulikia! Usafi wenu uko wapi zaidi ya unafiki!?
 
Wewe wadanganye watingishe kiberiti,
Ni kama wamesamehewa, maana wangefunguliwa kesi ya uhujumu uchumi!!
Kumbuka hiyo kesi haina dhamana
Hizo kesi za uhujumu uchumi zinafunguliwa kwa kufuata na kuzingatia sheria za nchi?Mbona inavyoelekea mnawafungulia wale wanaowakosoa?CCM imejisahaulisha misingi yake(Imani) ya inayosema Binadamu wote ni sawa,Kusema kweli daima,kutetea wanyonge na Utu wa binadamu ni zaidi ya Mali.
 
Kwanza, kwa vile wewe umeona uchungu na kuwatetea wezi, kwa nini usiwe mstari wa mbele kufungua kesi ya kuwatetea? Kesi siyo lazima wafungue wao, hata wewe mkereketwa wa kutetea haki za wezi wizi unaweza kufungua kesi. Pili, huwezi kulinganisha wezi na watumwa. Mwizi ametenda hicho kitendo kwa hiari yake. Hakuna aliyemlazimisha. Mtumwa haamui kuwa mtumwa. Tukiendelea kulea majizi hatutafika. Wewe unadai haki ya ya majizi, je haki ya watoto kupata elimu wewe unaiona vipi. Je, wewe mwizi akikuingilia nyumbani kwako, ukatoka na mkuki, fimbo, mishale, au bunduki utaanza kwanza kufikiria haki ya mwizi kupelekwa mahakamani na si kumtungua kwa mkuki. Mwizi siyo wa kutetewa, maana ukimkurupusha ni ama wewe au yeye. Mimi sina huruma na majizi, hasa pale yanapokuwa yamekamatwa na ushahidi. Ukiyabembeleza majizi yataendelea kukuibia. Kama sera ya CHADEMA ni kubembeleza wezi na mafisadi, sioni kama mna huruma na maskini wa TZ.
CHADEMA imwehi lini kuiongoza Tanganyika+Zanzibar?Tusitafute pa kuficha kichwa ilhali tukifahamu fika kuwa kiwiliwili chote kipo nje peupe?CCM kama zao la TANU+ASP ndiyo watawala,mnashindwa kuwashughulikia wezi waliojaa pomoni ndani mwenu na kuanza kuwasingizia NCCR 1995,CUF 2000&2005 na CDM 2010,2015&2020 kwa wimbo ule ule!
Mnawaibia wapinzani kura halafu mnawalaumu mnaposhindwa kufikia matarajio/mahitaji ya Wananchi?
 
Ccm wanafikiri Watanzania ni mazuzu
Sheria ifate mkondo,DC aburuzwe mahakamani akajibu huko uzalendo wake.
 
Ni miaka karibia mitano sasa viongozi wamekuwa wakijichukulia sheria mikononi na hakuna kiongozi wa kisiasa wa juu anayekemea Jambo linaloashiria wahusika wanatekeleza msimamo wa serikali.

Wahanga wa tukio la Arusha wamelazimishwa kupigwa na kisha kulipishwa fedha zaidi ya milioni tano ambazo taarifa zinadai wamelazimishwa kuuza baadhi ya Mali zao pamoja na ndugu kuwachangia kutokana na vitisho na shinikizo lililotolewa na uongozi wa wilaya dhidi yao.

Uongozi huo ulienda mbali zaidi nakushinikiza kuwafungulia kesi zisizo na dhamana ikiwemo uhujumu uchumi wakiambiwa wamehujumu Mali ya umma na wasipotii nakulipa watawekwa ndani bila dhamana kwa kipindi kisichojulikana. Baada ya vitisho hivyo ambavyo hata vyombo vya habari vimehoji nakujiridhisha kuwepo kwa uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu hakuna chombo kiliripoti ukubwa wa kadhia hii badala yake vyombo vyote vya habari vimesimama na DC na kumfanya DC aonekane kuwa yupo sahihi.

Rai inayotolewa na familia za wahanga nikupata uwakilishi wa kisheria waweze kwenda mahakamani kuomba tafsiri ya kisheria ya kile ambacho wametendewa ikiwa Ni pamoja na kuangalia njia yakupata fidia kwa madhara waliyopata.

Ikumbukwe hata watumwa baada Uhuru kwenye baadhi ya Mataifa walikuja kufungua kesi na mahakama za Dunia wakatoa maamuzi lengo likiwa nikuheshimu utu na haki za binadamu.

Kwa upande wa pili, mkuu wa wilaya kutamka adharani kuwa mchakato wa kisheria dhidi ya watuhumiwa ni kupoteza muda inaleta tafsiri kwamba serikali haiamini Kama muhimili wa mahakama una heshima yake. Kitendo Cha mahakama wakati wote kudharaulika wakakaa kimya nacho kinatia ukakasi.

Niwaombe watu wa haki za binadamu waache kukaa ofisini na kutuletea taarifa za uvunjifu wa haki za binadamu waingie kwenye vyombo vya kisheria nakuwatetea wanaoumia, atutaki takwimu za uvunjifu wa haki tunataka kusikia wamefungua kesi ngapi kutetea wananchi wanaoumizwa na ngapi wameshinda, fidia kiasi gani nk
Hao jamaa waachane na "wajuaji" wa JF. Wameishawapotosha wengi wakajikuta pabaya. Mange, Lowassa, Mdude, Membe na Lissu kutaja wachache!
 
Back
Top Bottom