kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Ni miaka karibia mitano sasa viongozi wamekuwa wakijichukulia sheria mikononi na hakuna kiongozi wa kisiasa wa juu anayekemea Jambo linaloashiria wahusika wanatekeleza msimamo wa serikali.
Wahanga wa tukio la Arusha wamelazimishwa kupigwa na kisha kulipishwa fedha zaidi ya milioni tano ambazo taarifa zinadai wamelazimishwa kuuza baadhi ya Mali zao pamoja na ndugu kuwachangia kutokana na vitisho na shinikizo lililotolewa na uongozi wa wilaya dhidi yao.
Uongozi huo ulienda mbali zaidi nakushinikiza kuwafungulia kesi zisizo na dhamana ikiwemo uhujumu uchumi wakiambiwa wamehujumu Mali ya umma na wasipotii nakulipa watawekwa ndani bila dhamana kwa kipindi kisichojulikana. Baada ya vitisho hivyo ambavyo hata vyombo vya habari vimehoji nakujiridhisha kuwepo kwa uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu hakuna chombo kiliripoti ukubwa wa kadhia hii badala yake vyombo vyote vya habari vimesimama na DC na kumfanya DC aonekane kuwa yupo sahihi.
Rai inayotolewa na familia za wahanga nikupata uwakilishi wa kisheria waweze kwenda mahakamani kuomba tafsiri ya kisheria ya kile ambacho wametendewa ikiwa Ni pamoja na kuangalia njia yakupata fidia kwa madhara waliyopata.
Ikumbukwe hata watumwa baada Uhuru kwenye baadhi ya Mataifa walikuja kufungua kesi na mahakama za Dunia wakatoa maamuzi lengo likiwa nikuheshimu utu na haki za binadamu.
Kwa upande wa pili, mkuu wa wilaya kutamka adharani kuwa mchakato wa kisheria dhidi ya watuhumiwa ni kupoteza muda inaleta tafsiri kwamba serikali haiamini Kama muhimili wa mahakama una heshima yake. Kitendo Cha mahakama wakati wote kudharaulika wakakaa kimya nacho kinatia ukakasi.
Niwaombe watu wa haki za binadamu waache kukaa ofisini na kutuletea taarifa za uvunjifu wa haki za binadamu waingie kwenye vyombo vya kisheria nakuwatetea wanaoumia, atutaki takwimu za uvunjifu wa haki tunataka kusikia wamefungua kesi ngapi kutetea wananchi wanaoumizwa na ngapi wameshinda, fidia kiasi gani nk