Waliochaguliwa kwenda kidato cha tano 2021 hawa hapa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,873
Idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano kwa shule za Serikali na vyuo vya elimu na mafunzo ya ufundi mwaka 2021 imeongezeka kwa asilimia 14.

Ongezeko hilo linakuja baada ya jumla ya watahiniwa waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwa shule za Serikali na vyuo vya elimu na mafunzo ya ufundi mwaka 2021 kufikia 148,127 kutoka 129,854 mwaka 2020.

Hayo yamesemwa leo Jumanne Juni Mosi, 2021 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.

Alisema uchaguzi huo umefanyika kwa kuzingatia Takwimu za wanafunzi waliofanya mtihani mwaka 2020 kutoka Tanzania Bara ambapo watahiniwa waliopata daraja la kwanza hadi la tatu walikuwa 153,464 ikiwa wasichana 67,135 na wavulana 86,329, sawa na asilimia 35.06 ya watahiniwa wote.

Alisema kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea waliomaliza kidato cha nne mwaka 2020 wakiwa chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ambao walipata daraja la kwanza hadi la tatu walikuwa 479 ikiwa wasichana ni 289 na wavulana 190.

Hata hivyo Waziri Ummy alisema katika kufanya uchaguzi huo hawakuwaweka nyuma wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika kujiunga na udahili huo.

“Idadi hiyo ya wanafunzi wenye sifa za kujiunga na udahili huo pia imejumuisha wanafunzi wenye mahitaji maalumu 288 wakiwemo wasichana 123 na wavulana 165,” alisema.

Tazama au fungu link hii ya Awamu ya kwanza ya majina ya waliochaguliwa kidato cha tano 2021
1622559686660.png
1622559728645.png

1622559769281.png

1622559794678.png

1622559819801.png
 
Back
Top Bottom