Waliobomolewa nyumba wawastukia, wawaambia...

KadaMpinzani

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
3,715
86
Waathirika wa bomoabomoa waishitukia CHADEMA
na julian msacky

WAATHIRIKA zaidi ya 90 waliovunjiwa nyumba zao Tabata Dampo, wamesema watashiriki maandamano yatakayoongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ikiwa lengo ni kufikisha kilio chao Ikulu.

Wamedai kuwa, kama lengo la chama hicho ni kutangaza sera zake kwa maslahi ya chama, hawatakuwa tayari kushiriki maandamano hayo.

Tamko hilo lilitolewa na Mwenyekiti wa waathirika hao, Masoud Said, jijini Dar es Salaam jana, alipoulizwa kama watashiriki maandamano hayo, yaliyotangazwa na chama hicho, Machi 24, mwaka huu, Tabata Dampo.

“Tutashiriki maandamano hayo kama agenda ya chama hicho itakuwa kupeleka malalamiko yetu serikalini, kulaani tukio la kuvunjiwa nyumba zetu, lakini si kinyume chake,” alisema Said.

Machi 24, mwaka huu, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Chacha Wangwe, akizungumza na wananchi hao, alisema leo wataandaa maandamano makubwa kwenda Ikulu, ili kudai waliovunjiwa wapewe haki zao.

Kwa mujibu wa Wangwe, ambaye ni Mbunge wa Tarime kupitia chama hicho, moja ya agenda ya kwenda Ikulu, ni wananchi kupewa haki ya kuishi, kurejeshewa nyumba zao walizovunjiwa hapo hapo, ili waweze kupata huduma zao za msingi.

Mbali na hilo, katika mkutano huo, chama hicho kilimtaka Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Stephen Wasira, kujiuzulu.

Wakati hali ikiwa hivyo, ripoti ya Tume ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na wahanga hao kutolewa Machi 23, mwaka huu, tarehe hiyo imesogezwa tena mbele.

Machi 12, mwaka huu, Waziri huyo aliunda Tume ya watu wanne ikiongozwa na Celestine Nchimbi kutoka Kitengo cha Sheria, Ofisi ya Waziri Mkuu, Abraham Shamimoyo kutoka TAMISEMI, Salum Chima kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, na Joseph Shewiyo, ambaye ni Naibu Kamishina Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi.
 
chadema kwa kuwapandisha wenzao mkenge hawajachacha.

waliwapandisha wale waliokuwa wanafunzi ukraine wakatumia shida zao kisiasa, mara madini kisiasa na mengi leo wameshtukiwa heko wananchi
 
Siyo vizuri kutumia siasa katika janga.

Lakini pamoja na hayo Wananchi wa Tabata dampo wanaweza kusubiri maandamano yatakayo andaliwa na CCM nafikiri wanaweza kujipatia kadi na wakasamehewa kiingilio kwa sababu ya kuvunjiwa nyuma zao.
 
chadema kwa kuwapandisha wenzao mkenge hawajachacha.

waliwapandisha wale waliokuwa wanafunzi ukraine wakatumia shida zao kisiasa, mara madini kisiasa na mengi leo wameshtukiwa heko wananchi

lakini hadi sasa nina shaka juu ya hawa wananchi, hata najiuliza sijui niseme au nikae kimya ! inawezekana wakawa...............
 
lakini hadi sasa nina shaka juu ya hawa wananchi, hata najiuliza sijui niseme au nikae kimya ! inawezekana wakawa...............

Posted Date::3/27/2008
Polisi wazuia maandamano ya Chadema kufika kwa mkuu wa mkoa
Na Muhibu Said

MAANDAMANO yaliyoandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuishinikiza serikali iwalipe fidia wakazi wa Tabata Dampo, jijini Dar es Salaam waliovunjiwa nyumba zao kiholela, jana yalifanyika chini ya ulinzi mkali wa polisi.

Hata hivyo maandamano hayo hayakuwa na mafanikio baada ya waandamaji walioongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe kuzuiwa kuingia katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Abba Kandoro.

Ulinzi huo uliowekwa katika maandamano hayo yaliyofanywa na watu wasiozidi 200, wengi wakiwa vijana wadogo, ulihusisha askari polisi wa kawaida, makachero na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).

Askari hao waliokuwa kwenye magari aina ya Land Rover takriban sita na gari maalum la polisi la maji yanayowasha, walibeba silaha mbalimbali, vikiwamo virungu, mabomu ya machozi na bunduki za risasi za moto.

Maandamano hayo yaliyoongozwa na Wangwe, yaliwashirikisha pia baadhi ya viongozi wa makao makuu ya chama hicho na waathirika wa uvunjwaji wa nyumba hizo, walioongozwa na Mwenyekiti wao, Said Masoud.

Yalianzia katika eneo la Tabata Dampo saa 8:00 mchana na kupita katika Barabara za Mandela, Uhuru na kuishia katika viwanja vya Soko la Mchikichini ambako viongozi hao walihutubia mkutano wa hadhara.

Baadhi ya askari, waliyosindikiza maandamano hayo baadhi yao waliweka doria katika soko hilo na katika Kituo cha Polisi cha Karume wakiwa ndani ya Londrover na gari la kurusha maji yanayowasha.

Waandamanaji walibeba mabango yenye ujumbe mbalimbali, baadhi yakihoji sera ya ardhi, iliko sheria, kuapa kutoondoka Tabata Dampo na mengine yakiipongeza Chadema na kumkejeli Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

"Sera ya ardhi inaua wanyonge", "Sheria ipo wapi?", "Kandoro Dar es Salaam imekushinda", "75% ya wakazi wa Dar es Salaam watabomolewa", "Hatuondoka kamwe bora tufe" na "Tunawapongeza Chadema".

Mbali na mabango hayo, waandamanaji hao walipita katika barabara hizo kwa mwendo wa mchakamchaka, huku wakiimba: "Tunataka nyumba zetu".

Waandamanaji hao walipofika katika makutano ya Barabara za Uhuru na Kawawa, walikwenda katika ofisi za Mkuu wa Mkoa, lakini hawakuweza kuingia baada ya polisi wa kawaida na wale wa FFU waliokuwa na bunduki za risasi za moto na mabomu ya machozi, kuwazuia katika lango kuu.

Kutokana na hali hiyo, Wangwe aliwaamuru waandamanaji hao kuondoka katika eneo hilo, ndipo walikwenda moja kwa moja katika viwanja vya soko hilo na kufanya mkutano wa hadhara.

Akihutubia mkutano huo, Wangwe alisema mbali na kushinikiza waathirika hao walipwe fidia, maandamano hayo yameandaliwa pia kwa lengo la kuitangazia Jumuiya ya Kimataifa kwamba kuna matendo ya kinyama yaliyofanyika Tanzania dhidi ya raia.

"Kazi yetu pia ni kuikosoa serikali iliyoko madarakani na kuwaelimisha wananchi kuhusu haki zao za ardhi," alisema Wangwe.

Wangwe alisema sababu nyingine iliyowafanya wafanye maandamano hayo, ni baada ya kuona tangu serikali iunde tume kuchunguza uvunjwaji wa nyumba hizo, hadi sasa hakuna kinachoeleweka kuhusu hatma ya haki za waathirika wa kadhia hiyo.

"Tunataka wananchi wapewe haki zao na si misaada, kwani kinachofanyika hivi sasa ni kuwafanya waathirika kama wakimbizi," alisema Wangwe.

Alisema wataendelea na maandamano kama hayo katika maeneo yenye migogoro ya ardhi nchini kwa kushirikisha asasi za kiraia, wakiwamo wafanyabiashara na wakulima.

Alisema wataendelea kuungana na waathirika kwa kuishi nao katika mahema katika eneo hilo hadi hapo watakapopata haki zao. Alisema yeye na wenzake walianza kuishi katika eneo hilo kuanzia jana.

Naye Masoud alisema wanaunga mkono maandamano hayo kwani yamewapa fursa Watanzania kufahamu yaliyowapata na jinsi viongozi wachache wa serikali wanavyotumia vibaya madaraka yao kuwaangamiza raia wadogo.

Masoud alisema tangu mvua zianze juzi jijini Dar es Salaam, baadhi ya waathirika wamekuwa wakijihifadhi katika nyumba nane zilizonusurika kuvunjwa na wengine wanajihifadhi katika msikiti ulioko katika eneo hilo.

Wakazi hao walivunjiwa nyumba zao Februari 29, mwaka huu kwa amri ya baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kinyume na taratibu.

Kutokana na hatua hiyo, Mkurugenzi, John Lubuva na Mhandisi wa Manispaa hiyo, Iddi Kisisa walisimamishwa kazi na serikali iliunda tume kuchunguza kadhia hiyo.

Tuma maoni kwa Mhariri
 
hivi hawa chadema hawana kazi nyengine ya kufanya zaidi ya fitna na uchonganishi?

inanisikitisha sana kila nikisoma habari za chadema ni kuwachochea wananchi wapingane na sheria au kuwajaza fitna hii inanisikitisha mno.

hivi hamuwezi kutoa rai mbadala kwa njia za amani, serikali iliopo tukubali si ya kibabe tumekiri wenyewe hata baadhi ya mawazo wanapita humu ambapo hata mwakabwela wanaandika mawazo yao na kuyachukua na kuyafanyia kazi.

chadema mnakutana na watendaji wA serikali kila saa kwa nn msiombe kukaa nao na kutoa ushauri wenu ktk kutatua matatizo ya wananchi badala yake mnangojea patokee uchochoro mjenge fitna na chuki.

taireni wakuu, taireni huo mwendo sio.
 
Mimi si mwanasiasa lakini nilidhani siasa katika demokrasia ni kuonyesha pale mwenzako anapoteleza? Na kama huyo mwenzako amekalia kiti kuitumia nafasi hiyo kikamilifu ili waliowaweka wamuone hafai na wewe uchukue nafasi yake? Wakati wa Katrina sikuwaona demokrats wakimtetea Bush bali walitumia kila nafasi kuushusha huo mzigo kwake na chama chake! Hakuna cha kushangaza katika kile ambacho Chadema wanafanya!
 
hivi hawa chadema hawana kazi nyengine ya kufanya zaidi ya fitna na uchonganishi?

inanisikitisha sana kila nikisoma habari za chadema ni kuwachochea wananchi wapingane na sheria au kuwajaza fitna hii inanisikitisha mno.

hivi hamuwezi kutoa rai mbadala kwa njia za amani, serikali iliopo tukubali si ya kibabe tumekiri wenyewe hata baadhi ya mawazo wanapita humu ambapo hata mwakabwela wanaandika mawazo yao na kuyachukua na kuyafanyia kazi.

chadema mnakutana na watendaji wA serikali kila saa kwa nn msiombe kukaa nao na kutoa ushauri wenu ktk kutatua matatizo ya wananchi badala yake mnangojea patokee uchochoro mjenge fitna na chuki.

taireni wakuu, taireni huo mwendo sio.

well, naona imeanza kuback fire ! MNYIKA mwenyewe hana pa kuonekana. Alikusanya wamachinga ( ili watoe ripoti, maana MNYIKA ni mzee wa maripoti tu, hana solutions) na sasa sijui ameishia wapi, kimyaaaaaaaaaaa !
 
Hivi KadaMpinzani,

Mnyika kakufanyaje lakini, unaenda naye sambamba tu mwaka huu hehehehe...
 
Nusa nusa ya kipaparazi inaonyesha kwamba baadhi ya viongozi ndani ya CHADEMA hawakubaliana na mtindo wa Chacha Wangwe na matamshi yake ya kukurupuka. Inaelekea mmmoja wa viongozi hao ni Bwana Mnyika ambaye hakuwepo mara zote tabata na mpaka sasa haiujulikani amejificha wapi. Lakini kuhusu hii ripoti ya wamachinga si walitoa solutions na wakata serikali itekeleze mambo fulani ndani ya mwezi mmoja? Kuna mtu mwenye nakala ya ripoti nzima ambayo ilizinduliwa siku hiyo tuzione pumba za CHADEMA? Nilitoa ushauri hapa kwamba CHADEMA hawana serikali, wamachinga wawapuuze

PM
 
Hivi KadaMpinzani,

Mnyika kakufanyaje lakini, unaenda naye sambamba tu mwaka huu hehehehe...

Yeye ni kijana wa kuigwa maana yupo mstari wa mbele akiona kuna soo atasema chadema watafanya hivi na hivi na vile, lakini pakitibuka HUMUONI ! Anayemtibulia ni mwenzake wangwe !
Nafikiri raia pia tunaweza kuiga mfano wake,
 
Nusa nusa ya kipaparazi inaonyesha kwamba baadhi ya viongozi ndani ya CHADEMA hawakubaliana na mtindo wa Chacha Wangwe na matamshi yake ya kukurupuka. Inaelekea mmmoja wa viongozi hao ni Bwana Mnyika ambaye hakuwepo mara zote tabata na mpaka sasa haiujulikani amejificha wapi. Lakini kuhusu hii ripoti ya wamachinga si walitoa solutions na wakata serikali itekeleze mambo fulani ndani ya mwezi mmoja? Kuna mtu mwenye nakala ya ripoti nzima ambayo ilizinduliwa siku hiyo tuzione pumba za CHADEMA? Nilitoa ushauri hapa kwamba CHADEMA hawana serikali, wamachinga wawapuuze

PM

wewe umetumwa na mafisadi ! Muone kwanza, lol !
Endelea tu kutetea mafisadi, na wewe ushakuwa fisadi eeh'.(nakutania mzazi)!
 
Huyo Bw. Chacha Wangwe si alisema nae atahamia huko kwa waliovunjiwa nyumba? hadi pale watakapolipwa fidia... vp tena ameshindwa kulala kwenye mkeka..
 
Huyo Bw. Chacha Wangwe si alisema nae atahamia huko kwa waliovunjiwa nyumba? hadi pale watakapolipwa fidia... vp tena ameshindwa kulala kwenye mkeka..

nafikiri alipitiwa na kauli nyiiingi zikamjaa ! Si ndio pale wananchi wakasema kama amekuja kwa ajili ya chama chake watamtimua, sasa sijui ndio wamemtimua au vipi ! kulala kwenye mkeka mchezo !
 
Back
Top Bottom