KadaMpinzani
JF-Expert Member
- Jan 31, 2007
- 3,716
- 86
Waathirika wa bomoabomoa waishitukia CHADEMA
na julian msacky
WAATHIRIKA zaidi ya 90 waliovunjiwa nyumba zao Tabata Dampo, wamesema watashiriki maandamano yatakayoongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ikiwa lengo ni kufikisha kilio chao Ikulu.
Wamedai kuwa, kama lengo la chama hicho ni kutangaza sera zake kwa maslahi ya chama, hawatakuwa tayari kushiriki maandamano hayo.
Tamko hilo lilitolewa na Mwenyekiti wa waathirika hao, Masoud Said, jijini Dar es Salaam jana, alipoulizwa kama watashiriki maandamano hayo, yaliyotangazwa na chama hicho, Machi 24, mwaka huu, Tabata Dampo.
Tutashiriki maandamano hayo kama agenda ya chama hicho itakuwa kupeleka malalamiko yetu serikalini, kulaani tukio la kuvunjiwa nyumba zetu, lakini si kinyume chake, alisema Said.
Machi 24, mwaka huu, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Chacha Wangwe, akizungumza na wananchi hao, alisema leo wataandaa maandamano makubwa kwenda Ikulu, ili kudai waliovunjiwa wapewe haki zao.
Kwa mujibu wa Wangwe, ambaye ni Mbunge wa Tarime kupitia chama hicho, moja ya agenda ya kwenda Ikulu, ni wananchi kupewa haki ya kuishi, kurejeshewa nyumba zao walizovunjiwa hapo hapo, ili waweze kupata huduma zao za msingi.
Mbali na hilo, katika mkutano huo, chama hicho kilimtaka Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Stephen Wasira, kujiuzulu.
Wakati hali ikiwa hivyo, ripoti ya Tume ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na wahanga hao kutolewa Machi 23, mwaka huu, tarehe hiyo imesogezwa tena mbele.
Machi 12, mwaka huu, Waziri huyo aliunda Tume ya watu wanne ikiongozwa na Celestine Nchimbi kutoka Kitengo cha Sheria, Ofisi ya Waziri Mkuu, Abraham Shamimoyo kutoka TAMISEMI, Salum Chima kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, na Joseph Shewiyo, ambaye ni Naibu Kamishina Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi.