Walio wengi tulidhani Magufuli atafanya haya, kadri muda unavyopita tunakata tamaa, hata huo uchumi wa kati yaweza kuwa ndoto tu!

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Naendelea kukiri kwamba Magufuli ni miongoni mwa marais wachache sana wanaofanya kazi ya uhakika hapa Afrika hilo halipingiki kabisa

Ukiangalia Marais 5 wa mwanzo kwa uchapakazi yeye kama hashiki namba moja basi namba mbili au tatu,
Lakin pamoja nana kwamba hao marais wanafanya kazi sana ndani ya Afrika bado hawajawa na ari ya kuyaleta mabadiriko sahihi ya kuwanufaisha wananchi wanaowaongoza,

TEGEMEO AU MATEGEMEO YA WENGI TANZANIA JUU YA UONGOZI WA MAGUFULI ILIKUWA KAMA IFUATAVYO

UCHUMI
Sisi wasomi na waelewa wa masuala ya uchumi tulidhani magufuli atazirejesha fedha zote ambazo mabeberu walikuwa wanazitumia kufanyia mambo yao, baada ya kuzirejesha hazina basi atakuja na mfumo thabiti wa kuzisambaza kwa wananchi kupitia miradi mbali mbali, sio kugawa kama cash, hapana kunaweza kuwepo mpango wa maendeleo ya jamii kupitia kuweka na kukopa, Au pia kuputia benki hizo hizo hela zingeletwa upya kwa utaratibu safi watu wakakopa , ila yeye alichofanya kaweka hela yote kwenye akaunt ya pamoja ya serikali (treasury account) na hela inakuwa controlled huko, badala ya decentralize utaratibu wa uingizaji wa fedha kwenye mzunguko, hivyo pesa kuongezeka kwenye mzunguko inategemea na furaha ya Magufuli ili aamue ,akinuna hamuipati,

VIWANDA
Nilitegemea yafuatayo
Kila balozi atapewa target ya kuleta mwekezaji Tanzania wa viwanda vidogo, vikubwa na vya kati,

Pia hata serikali ingefufua viwanda vile vile vya zaman ambavyo vinawezekanika , maana kuna ambavyo viko analogue sana mpaka kubadili mfumo wake wa uendeshaji,

Tulitegemea ,Viwanda vya nguo, ngozi, maji, samani, baiskeli, alafu tukaongeza hata vya redio,

Lakin magufuli anasema vyerehani vinne ni kiwanda,

USAFIRSHAJI
Tulitegemea kuona shughuli za kitaifa ambazo ziko sambamba na usafirishaji zikiendelea usiku na mchana , lakin ikifika saa 5 usiku unasikia kwamba hakuna kuendelea na safari usiku tunaogopa majambazi, unajiuliza serikali ndo ya kuogopa majambazi kweli??

ULINZI
Kwakweli suala la ulinzi Magufuli hii serikali yako imeshindwa kidogo kulihandle hundred percent au hata 70 percent, kuna mauaji , ukianza kule yaloendelea kibiti, ukaenda utekaji na kupotea kwa watu hiyo inaleta sintofahamu,

ELIMU
Hapa nakili mzee hujapatendea haki, wengi wanaoshangilia elimu bule hawajaangalia kwa ufasaha, tunakupongeza kwa kazi hiyo lakin kaa ukijua hakuna nchi ya kuweza kuingia uchumi wa kati kwa kusoma kinjekitile ngwale , Mangungo wa Musovelo au Chimurenga war, hapana Elimu iliyoleta mabadiliko ya kimfumo wa kiuchumi iliendana na mazingira halisi na uzalishaji wa moja kwa moja, elimu ya ufundi
Tulitegemea kwamba kila mkoa utaweka chuo cha ufundi , Mategemeo ya wanaoipenda Tanzania tukadhani unapunguza vyuo vikuu, unapungusha shule za kata nguvu kuzielekeza kwenye elimu ya sayansi ya ufundi, kumbe unaendelea na yale yale ya Jakaya,

VYUO VIKUU hapa tulitegemea watoto uwape mikopo, wote hawazidi 130,000 lakin mnaangaika nao , au hata hela ambayo wadaiwa wanarejesha mnafanyia mambo mengine??
AJIRA
Tangia umeingia ikulu ajira ulizotoa hazifikia elfu 10, inatisha na inasikitisha,
Tulidhani labda ukija sekta zote za serikali tutaimarisha ulinzi tufanye kazi kwa shift mpaka usiku, kwamba watu 120,000 wanafanya mpaka saa 8 mchana , alafu unatengeneza ajira mpya 120,000 nyingine wa kuingia shift za usiku lakin umeshindwa hata kuliona hilo, tulidhani utakomesha mazoea ya kufunga ofis saa kumi wakati uzalishaji unaendelea,

BIASHARA
Kodi Kodi Kodi mmefanya mahesabu mabaya kwenye kodi mpanga mnawatia umasikini watanzania, hakuna mfumo thabiti wa kutambua wafanyabiashara wote na aina ya biashara wanayofanya na mitaji yao ,ili mtu tozwe anachostahili, lakin hakuna mfumo mzuri, mnalala mbele na anayekatiza anafidia na za ambao hawakupatikana au ambao hawajalasimisha biashara, tulidhani MAGUFULI utafanya haya,

MFUMUKO WA BEI
Sukari imepanda, saruji, vifaa vya ujenzi, vifaa vya umeme na nakadhalika vimepanda bei, tulidhAni utatumia.mechanism ulotumia kwenye kushusha soda bei, (Government pegging) ili hata bidhaa nyingine zisipande bei, ila hatujaona,

IDLE AU WAZURURAJI
Hapa tulitegemea kila mkoa uweke makarandinga matano ambayo yao ni kupita kutafta wasio na kazi maalumu wanaozurura, alafu wanapelekwa kwenye kambi maalumu ambayo iko kwenye mkoa husika lakin maporini na kuna shughuli za uzalishaji zinaendelea huko,
Kuweko ufugaji,ufumaji, ufundi, na kilimo, alafu wanasimamiwa na JKT, wapewe chakula vizuri kabisa lakin waafanye kazi,

UFISADI NA RUSHWA
Hapa nilidhani kujinadi kwako kutaanza na watu wahusika wa EPA, KIWIRA, MCHUCHUMA, RICHMOND, NYUMBA ZA SERIKALI, kumbe wanaenda kufungwa fungwa watu wa chini wale wa bank ambao wamekula vi milioni 2 au 3 ndo unasikia kafungwa 15 years,
Wale wengine mmewafungulia kesi bila ushahidi naona wanaachiwa tu HAKUNA KITU KINAKERA MNATUITA KWENYE TV KUONESHA MNAVYOKAMATA WABADHIRIFU WA MALI ZA UMMA ALAFU UTASIKIA ETI DPP KUTUPILIA MBALI MASHTAKA, hii imetukatisha tamaa kabisa,

UHURU WA KUSEMA NA KUANDIKA
Kwanza Magufuli wewe siyo dikteta, hivo mtu akikuandika huko facebook au tweeter kwamba we dikteta hakuna haja ya kuhangaika naye, maana unajijua we si dikteta, sasa kwanini ikuume wakati wanakusingizia?
Tulitegemea utaruhusu kila mtu aandike anavyotaka ila wasivunje sheria ya nchi, lakin nashangaa wanazibwa,

USHIRIKIANO KIMATAIFA NA WATANZANIA KUTOKA NJE
Kuna ili ndo limewafanya watu waanze kukata tamaa kabisa maana wakiangalia hata upinzani hakuna wa kumpa kura wote wale wale,
Wewe na serikali yako mmeanza kuwabana watanzania kutoka nje, kwanin, mnaweka urasimu kwenye kutafuta hati za watu kusafiri, na ambao wanazo mnawasumbua wasitoke, hii imekatisha tamaa,

SERIKALI YA MTU MMOJA IMEZAA UNAFIKI NA UOGA BAINA YA WATENDAJI NA WEWE KAMA RAIS
Kwa sasa kazi hazifanyiki kwa weledi ni mashindano ya kwamba ngoja rais asikie kwamba namimi nawajibisha kumbe hakuna lolote wanakurupuka wanaharibu,

MWISHO HII NDO IMETUACHA MIDOMO WAZI KUTETEA USHOGA
Ni wazi serikali inautambua ushoga kiaina, kupitia kwa Kange Lugola waziri wa mambo ya ndani zile sentensi zake, na kupitia kwa wwaziri wa mambo ya nje mmetuumiza sana,
Sisi hatukuchagua serikali ya kuonea haya kukemea ushoga,
Tumekata tamaa sana

IKUMBUKWE HAYA NI MAWAZO YANGU NAWE LETA YAKO

Britannica
 
Ninyi ndo mabwege wa CHADEMA, ndo maana mnajiteka, mnajipiga risasi kwenye gari na kuudanganya umma, hatudanganyiki.tunajua CHADEMA wamekusajili kuisema serikali,
 
Back
Top Bottom