Walinzi waeleza mwanzo mwisho walivyomsaidia Mo Dewji usiku baada ya kuachiwa na watekaji

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
5,154
10,809
Mkurugenzi wa kampuni ya walinzi waliomsaidia Mo Dewji usiku baada ya kuachiwa na watekaji amsema ,siku hiyo walinzi wa kampuni yake wakiwa kwenye doria za kawaida maeneo ya viwanja vya Gymkhana ghafla waliona mtu anakuja mahali walipo huku akitoa sauti ya kuomba msaada.

=======

Dar es Salaam. Meneja mkuu wa kampuni ya ulinzi ya Ultimate, Eliuta Mwanjawike amesema mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji aliwafuata askari wao huku akitoa maneno ya kuomba msaada siku aliyoachiwa na watekaji.

Mwanjavike alikuwa akiielezea Mwananchi jinsi askari wake walivyomsaidia mfanyabiashara huyo tajiri aliyetekwa Oktoba 11 akiwa Hoteli ya Colosseum, Oysterbay na watekaji kumtelekeza saa 7:30 usiku ya Oktoba 20 kwenye viwanja vya Klabu ya Gymkhana jijini Dar es Salaam.

Askari hao usiku huo walimsindikiza Dewji, maarufu kwa jina la Mo Dewji, hadi hoteli ya Southern Sun alikopiga simu kwa baba yake mzazi ili amfuate na kumchukua.

Pamoja na maeneo jirani na Colosseum na Gymkhana kuzungukwa na majengo yenye ulinzi unaotumia vifaa vya kisasa, bado Jeshi la Polisi halijaweza kuwatia mikononi mwake watekaji hao, ambao wameelezewa kuwa ni watu wanaozungumza lugha yenye lafudhi za mataifa ya kusini mwa Afrika.

Akisimulia mkasa huo jana, Mwanjawike alisema askari wake watatu walimweleza kuwa wakati wakiwa kwenye doria yao ya kawaida nje ya jengo la Umoja House lililo karibu na Gymkhana, walimuona mtu akiwafuata huku akitamka maneno ya kuomba msaada.

“Walishtuka na hawakumjua kama ni ‘Mo’. Alipowakaribia ilibidi wamwimbie stop (simama),” alisema Mwanjawike.

“Akiwa katika hali isiyo ya kawaida, ilimbidi Mo Dewji ajitambulishe kwa kusema ‘jamani mimi ndiye Mo. Mohammed Dewji yule aliyetekwa. Naomba msaada nipo katika risk (hatari).”

Alisema vijana hao walimweleza kuwa baada ya Dewji kujitambulisha kwao, aliwaambia anahitaji msaada apelekwe Hoteli ya Holiday Inn akafanye mawasiliano na ndugu zake.

“Askari wangu akamjibu Holiday Inn ni mbali ila ngoja tukuitie usafiri wa ofisi ili tukupeleke kwenye hoteli hiyo’,” alisema Mwanjawike.

“Hata hivyo, Mo aliwaambia hadi asubiri gari itachukua muda mrefu badala yake aliwaomba wampeleke kwenye hoteli yoyote iliyo karibu na eneo hilo.”

Meneja huyo alisema walinzi wawili kati ya watatu walimpeleka Mo Dewji hadi Hoteli ya Southern Sun ambayo ipo mita chache kutoka jengo la Umoja House. Alisema baada ya kufika, aliomba apewe simu kwa ajili ya kufanya mawasiliano na ndugu zake na alifanikiwa na haikuchukua muda mrefu ndugu zake walimfuata.

“Vijana wangu walisubiria hadi ndugu zake Mo wafike hotelini kumchukua ndipo nao wakaondoka. Hiki ndicho ninachoweza kusema kwa sasa kuhusu msaada tuliotoa kwa mfanyabiashara huyo. Maelezo mengi nimewakabidhi polisi kwa hatua zaidi za upelelezi.”

Oktoba 20 akizungumza kwa sauti yenye kuashiria furaha, baba mzazi wa mfanyabiashara huyo, Gullam Hussein Dewji alisema alipokea simu iliyopigwa na mwanaye akimtaka amfuate kwenda kumchukua Hoteli ya Southen Sun iliyopo takriban mita 200 kutoka eneo aliloachwa.

Alisema baada ya mtendaji huyo mkuu wa kampuni za Mohammed Enteprises Limited (MeTL Group), kutelekezwa Gymkhana alitembea hadi hoteli hiyo alikoomba msaada wa simu na kumpigia baba yake.

“Namshukuru Mungu nimemkuta Mo akiwa salama na haraka nilimpeleka nyumbani, lakini tumemkuta na majeraha kidogo,” alisema Gullam.

Chanzo: Mwananchi
 
IVI WASIOJULIKANA NDIO WANASUBIRIWA WAMKWIDE MWINGINE ?
mh rais kauli yako ni ipi ?
masuala ya amani ya wananchi wako upo kimya au umekasimisha ?
kumbuka usalama wa wananchi ni muhimu zaidi kuliko tanzanite uliyoijengea hadi ukuta isiibiwe..
 
IVI WASIOJULIKANA NDIO WANASUBIRIWA WAMKWIDE MWINGINE ?
mh rais kauli yako ni ipi ?
masuala ya amani ya wananchi wako upo kimya au umekasimisha ?
kumbuka usalama wa wananchi ni muhimu zaidi kuliko tanzanite uliyoijengea hadi ukuta isiibiwe..
Haya mambo hayaishi kwa kutolewa kauli ,yanaisha kwa kuwanyang'anya bunduki haraka haraka
 
Hapo nani anastahili ile sh billion moja, ni walinzi waliokuwa wa kwanza kumuona au mtu wa hotelini aliyetoa simu?
 
Back
Top Bottom