Walinzi wa SUMA-JKT daraja la Nyerere (Kigamboni) ni kero

timeline

JF-Expert Member
May 19, 2015
458
2,403
Wadau,

Kwanza nipongeze hatua ya kuweka ulinzi eneo la daraja na kwenye barabara zinazotoka na kuelekea Nyerere Bridge. Naamini Lengo na madhumuni yalikuwa kwa manufaa ya watumuaji wa daraja.

Cha kushangaza walinzi wa SUMA JKT wamekuwa kero badala ya msaada.

Kwa mara kadhaa nimeshuhudia walinzi hawa wakisimamisha magari na pikipiki na kuanza kukagua. Kwa wanaoelewa huwaeleza kuwa hiyo si kazi yao na huwaachia bahati mbaya wapo wasiolewa, hawa huingia kwenye mtego.

Nimesaidia watu watatu baada ya kukamatwa na niliamua kusimama na kuuliza kinachoendelea, ndipo nikawaeleza walinzi hao kuwa wanachofanya sio sawa. Na niliamua kutoa taarifa kwa trafiki waliopo eneo la barabara ya Mandela, sijui hatua walizochukua.

Jana saa 12.20 jioni ndipo nikashihudia jambo baya zaidi, kijana mwendesha bodaboda akiwa anatokea Kurasini kuelekea darajani alikuwa anasimamishwa ghafla na mlinzi wa SUMA JKT na kwa kuwa Ilikuwa ghafla hakuweza kusimama na ndipo Mlinzi huyu alimfuta mwendesha pikipiki huyu aliposimama na kuaza kumpiga mateke akiwa juu ya pikipiki na hatimaye kijana huyu yeye na abiria wake wakaanguka.

Mlinzi huyu alikuwa akidai kwanini mwendesha pikipiki amesimama mbali. Nilishuka kwenye gari na kuamua kumzuia huyu mlinzi kumpiga Dereva wa bodaboda.

Niliamua kufikisha malalamiko yangu kituo cha Polisi Darajani Kama mita 150 kutoka eneo la tukio cha ajabu Polisi alinijibu kuwa hayo mambo Mimi hayanihusu niwaachie Wao watashughulikia.

Ninapoandika hapa, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa zaidi ya Dereva wa bodaboda kuambia aende akajitibie na kesi imeishia hapo.

Naona jambo moja hapa, hawa walinzi kuvaa sare zenye jina la SUMA -JKT inawafanya baadhi ya Wananchi wasiojua kudhani kwamba hawa ni askari wa Jeshi la Kujenga taifa hivyo kuheshimu kila wanachoambiwa hata Kama ni kinyume na taratibu.

Hili halitaishia hapa nina appointment na mmoja wa wakuu pale wizara ya mambo ya ndani Ili kufikisha malamiko yangu.
 
kweli mkuu ndugu yangu wiki mbili zilizopita alikamatwa.na gari la mzigo lenye uwezo wa kubeba tani kumi uzito ambao pale darajani unaoruhusiwa kupitisha gari.wakamzuia na kumuweka lock up na kumfungulia kesi ya kumbambikia kuhusiana na sheria za Tanroad kinyume na mabishano yao ya mwanzo
 
kwa kufanya ukaguzi kwenye magari sio jambo baya, watu waovu wanaweza kutupa hata maiti pale, ila kuwapiga na kuwatesa watu hiyo sio sawa haki isipopatikana duniani mbinguni itapatikana, watalipwa kadili ya matendo yao.
 
Design kama wanazingua vile maana Ni juzi Tu nilienda pale kushangaa Daraja , nkawa naona wale wamura wanafoka Sana na huku wameshikilia mashine duuu , Wakuu wao kikazi wawape maelekezo, miiko na mipaka ya Majukumu Yao.
 
Maaskari wemgi ni wale waliofeli darasa la saba na wachache kidato cha nne, sasa hapo unategemea nini? Kila askari anajifanya mbabe sana,yupo tayari kuvunja sheria maana anajua huna la kumfanya. Ni wapuuzi sana mimi huwa sina urafiki nao kabisa. Hawajui miiko ya kazi zao, wanachojua ni uonevu.

Askari wenye fani zao kama madaktari na wanasheria etc huwezi kuta anahangaika kutesa raia.

ELIMU ELIMU ELIMU
 
Huu unyanyasaji kwa raia unaofanywa na baadhi ya askari lazima ukemewe kwa nguvu zote.
 
hongera sana mkuu maana imekuwa bahati kila unyanyasaji unaotokea hapo na wewe unakuwa hapo hapo darajani unakwenda kusaidia
 
Nitalichukua na kukufanyanyia kazi kwa kweli hawa walinzi ni tatizo.
Nashukuru kwa kuweka ulinzi wa kueleweka lakini hawa vijana wa suma jkt ni pasua kichwa
 
So hapo tu ni polite wallop safari haha wa Suma -JKT kiukweli wanalidharirisha jeshi letu la kujenga Taifa. Nenda pale ofisi za TRA LONG ROOM. utachoka
 
Nina taarifa kwamba kwa wale wanaokwenda Kupiga picha hasa nyakati za usiku wamekuwa wakikamatwa na kutakiwa kutoa pesa kwa madai kuwa hairuhusiwi kupiga picha maeneo hayo.
 
Back
Top Bottom