Walinzi wa Rais Mobutu Sese Seko walivyomtorosha kwenda kuishi uhamishoni Morroco

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
11,544
2,000
Walinzi wa Rais Mobutu Sese Seko wakiongozwa na ma-bodyguard Colonel Motoko na Major Ngani walivyoweza kumuokoa Mobutu asikamatwe na askari waasi waliokuwa wameuzingira mjini mkuu wa Zaire wa Kinshasa.

Walipoona majeshi ya Mzee Laurent Desire Kabila yana elekea kwa kasi Kinshasa waliamua ndege rasmi ya Rais wa Zaire iende kwanza kuegesha nchi jirani ya Brazaville Congo ngambo ya mto Congo.

Cha ajabu wakati majeshi ya Laurent Kabila yanaukaribia mji mkuu wa Congo (Zaire ), wanausalama wa Zaire walipoomba ndege hiyo rasmi ya Rais Mobutu ifike Kinshasa haraka kumuokoa Mobutu, serikali ya Congo Brazzaville iligoma kuruhusu ndege hiyo iondoke. Ndipo hapo walinzi wa Mobutu wakaja na mpango wao wa pili ili kumnusuru Mobutu asiangukie mikononi mwa majeshi ya Mzee Laurent Kabila.

Mlinzi mwandamizi wa Mobutu kwa miaka 22 mfululizo akielezea operesheni yao ya kumtorosha Mobutu toka Kinshasa na kisha kufika Kijiji cha asili cha Gbadolite kujificha.

Na mipango ya mwisho ya wanausalama hao kumtorosha Mobutu Sese Seko toka kijijini hapo kwa kuilazimisha ndege ya mizigo ya Urusi aina ya Ilyushin iliyotua ktk uwanja wa ndege kijijini Gbadolite nchini Zaire (DR Congo) hadi mji mkuu wa Lome, Togo na hatimaye kufika uhamishoni nchini Morocco baada ya ushindi wa majeshi ya Mzee Laurent Kabila.

Video zote zina Sub-Titles in English pia kuna makamanda wa Rwanda na Uganda wanatumia lugha ya kiingereza


Source: Sefraus

INVASION OF CONGO 1996

Rais Museveni na Paul Kagame wakisimulia walivyokutana na Mzee Laurent Kabila na mtizamo wake Rais Museveni juu ya uwezo wa Mzee Laurent Kabila kutatua mgogoro wa nchi za Maziwa Makuu. Makamanda wa Jeshi la Rwanda na wale wafuasi wa Kabila wakisimulia uvamizi na vita kuelekea Kisangani mpaka Kinshasa kwa kutumia askari wa miguu.


Source: Sefraus

Rais wa Uganda Mh. Yoweri Kaguta Museveni akielezea kushangazwa na kasi kubwa ya majeshi ya Mzee Kabila kuelekea mji mkuu wa Kinshasa kumngoa Rais Mobutu Sese Seko wa Zaire. Major James Kaberebe aliyeongoza operesheni nzima ya uvamizi Zaire akiwa na umri wa miaka 29 tu anaelezea jinsi opresheni za kijeshi zilivyoweza kufikia malengo ya ushindi dhidi ya majeshi ya Mobutu. Pia Juhudi za jumuiya ya kimataifa za kidiplomasia kutatua uvamizi nchini Zaire ili kumuokoa Mobutu Sese Seko asingolewe madarakani.


Source: Sefraus

25 May 2020
Maisha ya Laurent Kabila tangu alipoanza mapigano hadi alipoapishwa mei 1997. Baada ya Mobutu Seseseko kukimbia| Mirathi ya siasa

Laurent Desire Kabila anakumbukwa kuwa rais wa tatu wa Jamhuri ya Demokrasi ya Kongo DRC baada ya kuutimua utawala wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Mobutu Seseseko. Katika makala ya mirathi ya siasa sehemu ya kwanza tunaangazia maisha ya Laurent Kabila tangu alipoanza mapigano hadi alipoapishwa mei 1997.
Source : KTN News Kenya
 

1954

JF-Expert Member
Nov 14, 2006
8,780
2,000
Napata picha watu wengi wa DRC, Burundi, Rwanda na Uganda huwa wanaingia humu JF
 

Lucas Mobutu

JF-Expert Member
Jul 29, 2017
15,067
2,000
Kuna kitu msichokijuwa Rwanda na Uganda walikuwa hawana uwezo wa kuichukuwa Congo kila kitu hadi uwezo wamepewa na wadhungu America na U.k
kweli kabisa kwa maana hata ukitoa nguvu ya kijeshi hata ki fedha congo ilikuwa mbali mno, mfano mara kadhaa zaire alituma wanajeshi wake rwanda kutuliza vurugu, wanajeshi wa kagame walichapwa sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom