Walinzi wa kampuni ya SUMA JKT GUARD wana matatizo ya kisaikolojia

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,701
36,119
Habari!

Ukichukua matukio machache yaliyofanywa na hawa vijana wa SUMA JKT GUARD utagundua kuna kitu hakiko sawa. Kuna upepo umepunguza akili zao.

Majuzi Jangwani walimpiga yule jamaa wa African sports na kupelekea kifo chake, tena tunapokea taarifa kuwa wamemuua mwananchi asiye na hatia aliyekuwa akilima shambani kwake karibu na msitu wanaoulinda.

Juzi jioni wakati natoka kazini narudi nyumbani njiani nikakutana na kijana wa suma kabeba Kirungu, manati, pingu na vikorokoro vingine anatembea akiekekea lindoni. Jinsi alivyojifanyia camouflage utadhani yupo vitani kumbe anakwenda kulinda kaeneo kadogo tu.

Wale vijana wa SUMA wengi wao ni vijana wa JKT waliomaliza mikataba yao na kurudi nyumbani bila mitaji. Marafiki zao wengi ni vijana waliokuwa nao JKT ambao sasa ni watumishi wa JWTZ, TISS, ZIMAMOTO , UHAMIAJI, MAGEREZA na POLISI.

Wenzao wanakopa wanajenga, wananunua magari na kusaidia ndugu huku wao vijana wa SUMA wakilipwa kitapeli na kampuni yao ya ulinzi. Take home yao haifiki hata 250k, hawakopesheki benki, ajira yao kufukuzwa ni rahisi, hawana uhakika wa maisha ya uzeeni.
Muda wa kazi ni mwingi.

Hawa vijana wa SUMA wasaidiwe .

Ni vijana waliokosa dira, sasa wamebaki kujitutumua tu ili nao wahesabike kama wanajeshi.

Unajua JKT mtiti wake ni mzito sana, miezi 6 unakula kozi ngumu huku ukiendelea kulima kwa bidii, then umemaliza unaendelea kulimishwa zaidi kila siku. Unavumilia ukijua utafanikiwa mwisho wa siku unapewa nauli tu urudi kwenu, lazima uchanganyikiwe.

Hakuna anayekwenda JKT eti akajitolee tu kisha arudi nyumbani. Basi serikali itoe mitaji kwa vijana wanaotoka JKT bila ajira ya uhakika ili wakaendeleze fani walizojifunza huko makambini. Wa kufuga samaki au kuku akafuge, wa kujenga akajenge n.k
 
...
Ni vijana waliokosa dira , sasa wamebaki kujitutumua tu ili nao wahesabike kama wanajeshi.
...
... kuna kamoja wiki iliyopita nilikashuhudia mahali kanataka kuingia kwenye public transport bila kulipa nauli kama kaka zao JW na Polisi kisa kamevaa magwanda ya SUMA! Kalisukumizwa kakadondoka kuleee! Huhitaji kumtamzama mara mbili kujua ni victim wa psychological problems.
 
... kuna kamoja wiki iliyopita nilikashuhudia mahali kanataka kuingia kwenye public transport bila kulipa nauli kama kaka zao JW na Polisi kisa kamevaa magwanda ya SUMA! Kalisukumizwa kakadondoka kuleee! Huhitaji kumtamzama mara mbili kujua ni victim wa psychological problems.
Kuna mmoja alifanikiwa kumtandika konda ngumi ya mdomo na kumchana mdomoni kisa mambo ya nauli ambayo ni sh.450.
 
Umeandika ukweli mtupu chief, hawa vijana walimezeshwa ndoto zenye mafanikio makubwa sana. Hivyo ilipelekea wakawekeza nguvu na akili zote kwenye kujitolea, then leo wamerudi kitaa wakiwa hawana mitaji, hawana ajira na wametoka mikono mitupu.

Wakiangalia wenzao waliokuanao mitaani, shuleni na JKT wamepiga hatua kubwa kimaendeleo....

Lazima wachanganyikiwe
 
Huwezi kuamini. Suma jkt guard kuna vijana wasomi wazuri tu.
Suma ya miezi hii sio ile Suma ya wakati wanaanza kuchukua tenda za malindo ya kwenye taasisi. Wale wa mwanzo walikua ni wakali sana halafu uelewa wa mambo ulikua ni mdogo sana.

Vijana wenzangu wa Suma JKT guard msikate tamaa ya maisha. Wote hamuwezi kuwa polisi, magereza au JW. Tumieni kipato kidogo mnachopata kujiendeleza kwa fani mbalimbali za stadi za maisha lakini kupata mitaji.

Wengi wenu bado ni vijana wadogo. Nawasihi muache umalaya sio mzuri, kuna ukimwi na homa ya ini. Kuweni makini sana vinginevyo mtakwisha.
 
Back
Top Bottom