Walinzi wa Area D (Dodoma) walikuwa wapi wakati Lissu akishambuliwa?

..Area D eneo aliposhambuliwa TL ni makazi ya Naibu Spika Dr.Tulia na Waziri wa Nishati Dr.Kalemani.

..Kwa kawaida makazi ya viongozi wa ngazi za juu kama hayo hulindwa na askari wenye silaha.

..Pia kiutaratibu askari hao huwa hawaruhusu mtu yeyote yule kuingia ktk maeneo wanayoishi viongozi bila kutambuliwa na kufanyiwa ukaguzi.

..Mh.Tundu Lissu alishambuliwa kwa silaha za kivita akiwa ndani ya eneo la makazi ya viongozi.

..Wananchi tunapaswa kuelezwa waliomshambulia Mh.Lissu waliingia ktk makazi hayo kwa utaratibu upi

..Walinzi walikuwa wapi na walichukua hatua gani baada ya kuona shambulizi lile.

..Walitoa taarifa wapi, kwa nani, na wakati gani.

..Lakini kama kulikuwa hakuna walinzi tunapaswa kuelezwa ni kwasababu gani. Na walinzi hawakuwepo wakati wa shambulizi tu au wakati wote. Pia ni nani alichukua uamuzi wa kuondoa au kutokuweka walinzi kabisa.

Cc Mwanahabari Huru, Mag3, Nzi, Zanika, MTAZAMO, masopakyindi, Nyani Ngabu
Hawakutumia akili Ilitakiwa walinzi wawepo apigwe Hata risasi moja. Mkononi Hata kupiga risasi juuu mradi purukushani za kivita "eti watu wasiojulikana" Hata akili za kuvukia barabara zinatosha kujua nini kilifanyika
 
Hivi kwa Polisi hilo faili ndio limefungwa hakuna wa kulichunguza tena
 
..hata mgonjwa naye ameanza kuhoji kuhusu ulinzi wa area D siku aliposhambuliwa.

..kwanini inachukua muda mrefu namna hii kupata majibu?

..walinzi walikuwa wapi? Au kwanini kulikuwa hakuna ulinzi?

Tunakaribia kufikisha mwaka toka tukio hili litokee. Inavyoelekea eneo la tukio lilikuwa "coincidentally deserted". Hata majirani ambao walisikia milio ya risasi wakaja kushangaa kama ilivyo kawaida ya Watanzania nao hawakuwepo!
 
..hata mgonjwa naye ameanza kuhoji kuhusu ulinzi wa area D siku aliposhambuliwa.

..kwanini inachukua muda mrefu namna hii kupata majibu?

..walinzi walikuwa wapi? Au kwanini kulikuwa hakuna ulinzi?

mkuu walinzi wanalinda kwa boss husika na sio barabara ya lami ukiuliza swqli la hivo ina maana ulitaka watoke kitengo walicho ajiriwa (bossi wao) wafate milio ya risasi badala ya kumuangalia boss wako km yupo salama au laa!!
 
Duuuh,hii kweli akili ya hapa na pale!
 
Tunakaribia kufikisha mwaka toka tukio hili litokee. Inavyoelekea eneo la tukio lilikuwa "coincidentally deserted". Hata majirani ambao walisikia milio ya risasi wakaja kushangaa kama ilivyo kawaida ya Watanzania nao hawakuwepo!

..kwa maelezo ya Lissu, alikuwa na fahamu muda wote mpaka walipomfikisha Dodoma Hospitali.

..pia yapo maelezo ya Tundu Lissu akieleza kwamba, baada ya shambulizi, watu wa kwanza kumpa msaada ni, dereva wake, mtumishi wake wa ndani, na dereva/mtumishi wa Naibu Spika Dr.Tulia.
 
Back
Top Bottom