Walinzi sita wa Makamu wa Rais wa Sudan Kusini, James Wani Igga wameuawa kwa kupigwa risasi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,866
Walinzi sita wa Makamu wa Rais wa Sudan Kusini, James Wani Igga wameuawa kwa kupigwa risasi na wengine wawili wamejeruhiwa baada ya msafara wao wa magari kuvamiwa na waasi mjini Juba. Kiongozi huyo hakuwa katika msafara huo wakati shambulio hilo lilipotokea.

Msemaji wa Kiongozi huyo, Kalisto Lado amesema magari ya msafara yalichomwa moto na kikundi cha kijeshi cha National Salvation Front (NAS) ambacho kilikataa kusaini mkataba wa amani 2018

Makamu wa Rais hakuwepo katika msafara huo wakati shambulio. Aidha Msemaji wa Makau wa Rais amesema ni kikundi hiko pia kilimua mpita njia

Sudan Kusini imekuwa na machafuko tangu mwaka 2013 na hivi karibuni wasemaji wa Benki Kuu walihusisha machafuko kuathiri uchumi wa nchi hiyo na kushusha thamani ya fedha yao
1597987540499.png

===

Six bodyguards for Vice-President James Wani Igga have been killed and two others injured after their convoy was attacked by rebels in Lobonok, his spokesperson Kalisto Lado said.

Igga is one of South Sudan’s five vice-presidents in the Revitalized Transitional Government of National Unity (R-TGoNU). He is in charge of the economic cluster.

Speaking to Radio Tamazuj on Thursday night, Kalisto said a vehicle the bodyguards were travelling in was destroyed and burnt by forces from the National Salvation Front (NAS), an armed group that refused to sign the September 2018 peace deal.

"The incident happened on Wednesday afternoon when the convoy was moving from the residence of the vice president in Lobonok to a nearby village. So the bodyguards were attacked by NAS forces on their way," he said.

"In the ambush by NAS forces, six bodyguards of the vice president died, two others were wounded, and one is still missing," he added.

Wani was not in the convoy when it came under attack in Lobonok, Lado said.

Lado condemned the killings and accused NAS forces of violating the cessation of hostilities deal signed in 2019 in Rome, Italy.

"Today (Thursday), the same NAS forces also killed a civilian who was coming from Pageri village in Lobonok to Yapa village. The civilian was killed in cold blood," said Lado.

NAS officers in Lobonok could not immediately be reached for comment.

Lobonok, the home village of Vice President James Wani Igga, is located about 30 kilometres south of the capital Juba on the east bank of the Nile.
 
waafrika wenye akili za kushikiwa..
Hapo ataambiwa beberu ndio chanzo!! Kumbe wakati mwingine ni ulafi tu wa viongozi wetu, kuendekeza ukabila tu, na Sudan kusini bila hao kina rick machali, na salva kirr, kuondolewa, kamwe haiwezi tulia, kipindi kile walisingizia sudan ya Khartoum kuwa ndio ilikuwa chanzo, huu ni mwaka wa ngapi wako pekee yao? Lakini hali ndio imekuwa mbaya zaidi?!! UKABILA NDIO TATIZO.
 
Nadhani ilo suluhisho pekeee
 
Yah wana ukabila sana na hawaelewani yani Dinka na Nuer hawapatani kabisa yani
 
Hivi Riek Machar si ndo makamu wa rais au kaendelea kugoma ili aendeleze Vita?.
South Sudan took new steps last week on its shaky path to peace, swearing in opposition leader Riek Machar as first vice president on February 22. Machar will serve in a unity government alongside his chief rival, President Salva Kiir, and three lower-ranking vice presidents, under the terms of the country’s current peace agreement.

Unity Government Rekindles Hopes for Peace in South Sudan
 
Sudan matatizo, hii nchi ina kila aina ya shida kuanzia ufisadi, ukabila , njaa mpaka matatizo ya kiuchumi.
 
Pamoja na hila za wazungu, tukubali tu waafrika ni shida. Ubinafsi na upumbavu ulipitiliza unatumaliza sana. Na sioni wa kumcheka mwenzake, sote ni walewale tunatofautiana viwango tu.
Na uwongo mwingi. Hats vitu vilivyofanywa na mkoloni, waliopo madarakani wanajinadi wamefanya wao ili wapige pesa.
 
Baada ya Sudan kusini kujitenga makabila makubwa mawili yakachomoza kila moja likijiona lina haki ya kutuo Rais.
Ni kama Zanzibar itakapojitoa kwenye muungano wapemba au waunguja mmojawapo ajione yeye ndo anahaki ya kutoa kiongozi mkuu wa nchi.
 
Back
Top Bottom