Walinda amani wasiwe chanzo cha wavunja amani

Yuco

New Member
Sep 10, 2021
2
5
Tanzania ni nchi ya Amani na Utulivu na hii ni tunu tuliorithi tangu vizazi na vizazi na sisi hatuna budi tuwalithishe vizazi vijavyo.

Amani ndio Chanzo na mafanikio ya kila kitu katika maisha ya kila siku kwa mwanadamu na anavyovimiliki mwanadamu huyo kuthibitisha hilo viongozi mbalimbali duniani kote wanahimiza Amani na Utulivu.

Nani mwenye jukumu la kulinda amani? Wengi wetu tunaamini Kuna watu maalumu ndio wenye jukumu la kulinda hiyo Amani tena tukiweka wazi wenyejukumu la kulinda raia na mali zao ni jeshi la polisi huo ni ukweli lakini isitupumbaze akili ifikie pahali tunaona uvunjifu wa amani wa dhahiri basi tukaacha kukemea tukiamini Kuna watu maalumu wenyekazi hiyo

Amani hujengwa kuanzia msingi yaani kwenye familia baba ,mama na watoto huko amani ikitengemaa basi itaonyesha matokeo chanya katika jamii kwa ujumla kwani majirani wataelewana hatimaye sisi sote tutatengemaa na kushirikiana na endapo kunashida itajitokeza basi ni rahisi kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo.

Pamoja na hayo yote uhalisia wa mwanadamu hauwezi kuacha kujitokeza kiasili mwanadamu ameumbwa, kuogopa,kuabudu,kuiga na kutegemea hapa nitagusia viwili tuu kutegemea na kuiga ,kila mwanadamu alipita katika utegemezi yaani tangu kutunga kwa mimba hadi anazaliwa mwanadamu alikuwa anamtegemea mama kwa kila kitu mpaka anapozaliwa na baba nae hutegemewa kwa kuleta chakula,mavazi ,ulinzi nk.huo ndio utegemezi wa mwanadamu na sifa ya kuiga mwanadamu pia anayo utakuta jambo linatokea sehemu fulani na sehemu nyingine watu huiga iko kitu Sasa kwenye kuiga hapo Kuna kuiga mazuri na kuiga mabaya Sasa hayo mabaya ndio Chanzo Cha uvunjifu wa amani utakuta watu wa sehemu fulani wamechoma moto jengo fulani hivyo watu wengine wanaiga hivyo hivyo hiyo ni sifa mbaya kabisa,kutokana na hayo mitaani kwetu matukio mabaya huongezeka kutokana na kuwepo watu wa aina hiyo na hiyo ndio imepelekea kuundwa kwa vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama pamoja na vyombo vya usuluhishi lakini je kuwepo kwa vyombo hivyo Kuna mabadiliko yeyote katika jamii?

Leo vituo vya polisi vinaonekana Kama sehemu ya kawaida kwa baadhi ya vijana wa mitaani Tena utawasikia wakisema ngoja nifanye msala niende nikapumzike juu wiki kadhaa Kisha nilejee kitaa yani wanaona polisi na mahabusu ni sehemu ya kupumzika tuu.

Je, ni kweli walinda Amani ndio chazo Cha uvunjifu amani?

Hilo swali Ni gumu Sana kulijibu moja kwa moja lakini Lina majibu sahihi kabisa, kuna baadhi ya walinda Amani wanasababisha uvunjifu wa Amani aidha kwa makusudi au kutotambua majukumu yao je nani wa kuwakumbusha majukumu yao? Kuthibitisha hayo fuatana nami.

Mwanzoni mwa mwezi wa saba kulitokea tukio wafugaji kulisha shamba la mazao ya mkulima wa mahindi na huyo mkulima akachukua hatua ya kwenda kuripoti polisi tena kituo kikubwa cha polisi cha mkoa huo kutokana na sababu zisizojulikana polisi hawakuweza kufika eneo hilo mkulima akaweka dolia anayoijua yeye mwenyewe siku nyingine wafugaji wakaingiza tena mifugo hivyo huyo mkulima alichokifanya akapiga picha mnato na akachukua video ikionyesha mifugo ikila mazao yake na akabahatika kumuhoji mchungaji wa hiyo mifugo alikili kosa na kuomba asamehewe kwani ni bahati mbaya baada ya kupatikana kielelezo hicho mkulima akaenda kwa mtendaji wa Kijiji wanapotoka hiyo mifugo kutokana na alama za mifugo hiyo mtendaji amekili kuwafahamu wa miliki wa mifugo kutokana na usajili na alama za mifugo hiyo kwa maana hiyo mtendaji yuko tayari kutoa ushahidi polisi ata mahakamani kwa kutambua alama za wanyama hao, mkulima akapeleka vile vielelezo polisi na wakaahidi kufanyia kazi baada ya wiki kadhaa kupita mkulima akaenda kufatilia muendelezo wa ufunguzi wa kesi yake jibu analopewa yeye aende kuwatafuta na kuwakamata hao wafugaji alafu atoe taarifa polisi Sasa unajuliza hivi mkulima anapoenda kumkamata masai bila ya silaha yeyote ile nini kitatokea Kama sio kukatwa mapanga ?

Mkulima ana uchungu na mazao yake leo unampa majibu Kama hayo unategemea anaweza fanya maamuzi gani?
Hivi kwa majibu ama utendaji kazi kwa wenye mamlaka hii migogoro itaisha kweli? Kwa ufikiri wa kawaida haitaji degree kukamilisha uchunguzi wa hii kesi ndani ya wiki moja tuu.
Hadi sasa mkulima huyo hajui afanyaje na haki yake itapatikanaje.
Na matukio Kama haya hupelekea watu kuchukua sheria mkononi wakiamini hakuna haki kwenye vyombo vilivyopewa mamlaka hayo
Nafikiri kungekuwa na ufatiliaji mzuri wa kesi Kama hizi na mwishoe anaekutwa na hatia anatakiwa apewe adhabu kali na fidia hii ingetoa funzo kwa watu Kama Hawa kwa hakika hili tatizo lingepungua Kama sio kuisha kabisa.

Tunaomba mamlaka zijifunze kuondoa mapema viashiria vya uvunjifu wa amani kuliko kusubiri huo uvunjifu utokee ndio kuunda tume kuchunguza maafa.Tuipende na tuilinde amani yetu.
 
Uko sahihi mkuu... naunga mkono hapa.

Serikali mwaka huu inatikisa sana kibiriti, bahati nzuri kibiriti chenyewe hakina kitu.

Sasa kama kikitikisika shuhuli itakua pevu na tutapoteza sana.

Tushukuru tu mitandao ya kijamii Ina-neutralize sana matukio.

Kunauwezekano serikali kuna kitu inakitaka ila wananchi hatuonyeshi ushilikiano.
 
Back
Top Bottom