Walinda amani wa MONUSCO wauawa DRC: Wamo Watanzania na Malawi

Ugiligili

JF-Expert Member
Jun 20, 2014
2,844
2,000
Umoja wa Mataifa umesema walinda wake amani wapatao 7 wameuawa katika mapigano yaliyozuka karibu na mji wa Beni kaskazini mwa Kivu, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Ni eneo lililoathiriwa zaidi na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini humo. Bado haijajulikana ni kundi gani la waasi limehusika na mashambulizi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya tukio hilo, msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema wanajeshi hao waliokufa, 6 ni kutoka Malawi na 1 Tanzania.

''..Walinda amani wameuawa wakati wa operesheni ya pamoja iliyokuwa ikifanywa na Kikosi cha Kulinda amani cha Umoja wa Mataifa na Jeshi la Congo dhidi ya kundi LA Allied Democratic Foirces linalojulikana kama ADF.

''Taarifa za awali zinaonesha kuwa walinda amani wengine 10 wamejeruhiwa na mmoja hajulikani alipo''. Amesema Dujarric

Walinda amani kadhaa wa jeshi la Congo pia wameripotiwa kuuawa ama kujeruhiwa katika operesheni hiyo.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya walinda amani waliouawa na serikali ya Jamhuri ya watu wa Malawi na ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Msemaji wa Umoja wa mataifa amesema pia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ameyasisistizia makundi yanayopigana kuacha kuacha mapigano, ambayo yanazidi kusababisha maafa kwa watu na pia ugumu katika kuudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini humo.

Wafanyakazi wa huduma za afya wanapata changamoto kuwapata na kuwahudumia wagonjwa walioambukizwa ugonjwa huo.

Mji wa Beni na vijiji vya jirani, umekuwa ukikabiliwa na mlipuko wa Ebola ambao umeshawaambukiza watu zaidi ya 300.

Mlipuko huu wa Ebola wa tatu kwa ubaya zaidi kuwahi kutokea baada ya ule uliotokea Afrika magharibi mwaka 2013 hadi 2016 ambako watu elfu 28 waliambukizwa na ule uliotokea Uganda mwaka 2000 ambako wagonjwa 425 waliripotiwa.

Makundi kadhaa ya wapiganaji likiwemo kundi la Ugandan Allied Democratic Forces, yanaendesha shughuli zake katika eneo hilo.

Umoja wa Mataifa umeongeza hali ya tahadhari kutokana na kuendelea kwa mapigano katika eneo hilo na kuonya kuwa ghasia zinaweza kuzuia uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao nchini humo.

Source:BBC SWAHILI
 

lwamu

JF-Expert Member
Apr 19, 2015
933
1,000
Ni wakati mwafaka sasa kwa serikali kuondoa majeshi yetu kwenye huo umoja wa mataifa,isitoshe sahz wana2bania misaada,kama mbwai mbwai 2...
 

mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
16,914
2,000
...Askari hafii kwenye maua, We lost our brothers and sisters. That is what is meant to be soldier!, Pumnzikeni kwa Amani makamanda Kifo chenu na kiwe ukombozi katika Ardhi ya Congo,
Unamshaurije askari anayefariki kwa ukimwi??
 

Nyanjomigire

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
6,171
2,000
Hawa ADF vipi? Kwa nini wasirudi kwao Uganda wakamng'oe Museveni aliyeng'ang'ania madarakani. Congo inawahusu nini, kazi kuvizia "Soft target tu na mali za Congo. They're really hopeless indeed.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom