Walimu wawasha moto mpya,Wataka mishahara ya 900,000/- | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walimu wawasha moto mpya,Wataka mishahara ya 900,000/-

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by palalisote, Feb 8, 2012.

 1. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0

  Wimbi la wafanyakazi wa umma kudai nyongeza ya mishahara, posho na marupurupu limechukua sura mpya baada ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kupendekeza viwango vipya vya mishahara wanavyopaswa kulipwa walimu. CWT kimesema mwaka wa fedha unaoanza Julai mwaka huu kinataka kuwe na ongezeko la asilimia 100 kwa walimu wote kulingana na viwango vya madaraja yao, ambapo wa Cheti (Daraja A), anatakiwa kulipwa sh laki tano, stashahada alipwe sh laki saba na nusu na yule wa shahada alipwe zaidi ya sh laki tisa.


  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kwa niaba ya Rais wa CWT, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Ezekiah Oluoch, alisema ongezeko hilo linatokana na kupanda kwa gharama za maisha. "Tumefanya tathmini na kujiridhisha kuwa mapendekezo yetu yanawezekana, serikali inaweza kutulipa fedha hizo kwa sababu ina rasilimali za kutosha," alisema. Oluoch alisema mapendekezo hayo yametokana na kikao cha Baraza la Taifa la chama hicho lenye wajumbe 163 wanaowakilisha walimu katika mikoa 21, kilichoketi Januari 31 hadi Februari mosi mjini Morogoro. Alibainisha kuwa baraza la taifa limeagiza kuwa majadiliano kuhusu nyongeza ya mishahara yaanze mara moja na yawe yamekamilika mwishoni mwa Machi mwaka huu. Alisema wanataka majadiliano hayo yafanywe mapema ili serikali iyaingize makubaliano kwenye bajeti yake ya mwaka huu. Oluoch alisema CWT inaamini kuwa majadiliano ni njia pekee ya kupata mwafaka wa ongezeko hilo la mishahara.


  CWT inahitaji kulipwa kwa posho za kufundishia na za mazingira magumu kwa walimu hao, kwa kuwa muda wa kazi zao ni tofauti na watumishi wengine wa umma.
  Kinataka walimu wote wapewe posho ya asilimia 55 kwa walimu wa masomo ya Sayansi na asilimia 50 wa Sanaa, na posho hizo zianze kulipwa kuanzia Julai.CWT kimesema kuwa nyongeza ya posho hizo si ngeni kwani Rais Jakaya Kikwete aliwapa ahadi hiyo Siku ya Walimu Duniani Oktoba 5, mwaka 2010.

  Chanzo: TANZANIA DAIMA
   
 2. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD] Walimu wawasha moto mpya

  • Wataka mishahara ya 900,000/-

  na Datus Bonif
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]WIMBI la wafanyakazi wa umma kudai nyongeza ya mishahara, posho na marupurupu limechukua sura mpya baada ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kupendekeza viwango vipya vya mishahara wanavyopaswa kulipwa walimu.

  CWT kimesema mwaka wa fedha unaoanza Julai mwaka huu kinataka kuwe na ongezeko la asilimia 100 kwa walimu wote kulingana na viwango vya madaraja yao, ambapo wa Cheti (Daraja A), anatakiwa kulipwa sh laki tano, stashahada alipwe sh laki saba na nusu na yule wa shahada alipwe zaidi ya sh laki tisa.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kwa niaba ya Rais wa CWT, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Ezekiah Oluoch, alisema ongezeko hilo linatokana na kupanda kwa gharama za maisha.

  "Tumefanya tathmini na kujiridhisha kuwa mapendekezo yetu yanawezekana, serikali inaweza kutulipa fedha hizo kwa sababu ina rasilimali za kutosha," alisema.

  Oluoch alisema mapendekezo hayo yametokana na kikao cha Baraza la Taifa la chama hicho lenye wajumbe 163 wanaowakilisha walimu katika mikoa 21, kilichoketi Januari 31 hadi Februari mosi mjini Morogoro.

  Alibainisha kuwa baraza la taifa limeagiza kuwa majadiliano kuhusu nyongeza ya mishahara yaanze mara moja na yawe yamekamilika mwishoni mwa Machi mwaka huu.
  Alisema wanataka majadiliano hayo yafanywe mapema ili serikali iyaingize makubaliano kwenye bajeti yake ya mwaka huu.
  Oluoch alisema CWT inaamini kuwa majadiliano ni njia pekee ya kupata mwafaka wa ongezeko hilo la mishahara.

  Malipo ya posho
  CWT inahitaji kulipwa kwa posho za kufundishia na za mazingira magumu kwa walimu hao, kwa kuwa muda wa kazi zao ni tofauti na watumishi wengine wa umma.
  Kinataka walimu wote wapewe posho ya asilimia 55 kwa walimu wa masomo ya Sayansi na asilimia 50 wa Sanaa, na posho hizo zianze kulipwa kuanzia Julai.

  CWT kimesema kuwa nyongeza ya posho hizo si ngeni kwani Rais Jakaya Kikwete aliwapa ahadi hiyo Siku ya Walimu Duniani Oktoba 5, mwaka 2010.
  Olouch alisema posho ya mazingira magumu, inatakiwa kulipwa kwa asilimia 70 kwa mwalimu anayefanya kazi maeneo ya vijijini, kama utekelezaji wa ahadi ya Rais Kikwete aliyoitoa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani Oktoba 2010.

  Madeni yasiyohusiana na mishahara

  CWT kimeitaka serikali kuwalipa walimu fedha zao za madeni yasiyohusiana na mishahara kabla ya Februari 15 na iwapo itashindwa kufanya hivyo, chama hicho kitachukua hatua dhidi ya waajiri waliokaidi makubaliano yaliyofikiwa.

  Oluoch aliongeza kuwa awali walikubaliana na serikali kuhusu utaratibu wa kulipa madeni hayo ambayo walihakiki kwa pamoja, wakishirikiana na viongozi wa serikali wa ngazi za wilaya, ambapo sh bilioni 22.5 zilitumwa kwenye halmashauri za wilaya na sh bilioni 3.5 zilitumwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

  Alibainisha kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha alitoa waraka ambao umetafsiriwa vibaya na baadhi ya watendaji wa serikali.
  Aliongeza kwamba, baadhi ya watendaji wametafsiri kinyume kuwa ni kuhakiki upya madai ya walimu badala ya kujiridhisha kama anayelipwa ndiye aliyehakikiwa.
  Alisema utata huo umechangia halmashauri 50 kutowalipa fedha walimu licha ya kuzipata fedha hizo.

  Kulipwa madeni ya mishahara

  CWT kinataka kufanyike marekebisho yote ya mishahara na malipo ya mapunjo yafanyike ndani ya mwezi huu bila kukosa.

  Oluoch alisema CWT ilifanya kikao na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Simfue Ombeni, Januari 13 mwaka huu na serikali ilitoa taarifa ya kulipwa kwa walimu 18,000 kiasi cha sh bilioni 18.
  Aliongeza kuwa CWT kupitia Baraza lake limesikitishwa na kauli ya serikali ya kukosa fomu hizo huku serikali ikificha ukweli, kwani tatizo linafahamika na kwamba walimu wengi hawajarekebishiwa mishahara yao baada ya kupanda madaraja.

  Chama hicho kimetaka kufutwa kwa waraka wa serikali wa kupunguza zoezi la upandishwaji wa madaraja kwa asilimia 50 kutokana na maelezo kuwa serikali haina pesa.
  SOURCE : TANZANIA DAIMA 08/02/2012 (Tanzania Daima - Sauti ya Watu)  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 3. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Safi sana. Polisi na nyinyi msibaki nyuma, mwendo ni KINDUGAI NDUGAI tu, kila mtu atangulize tumbo taifa baadaye
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,302
  Likes Received: 5,640
  Trophy Points: 280
  Mkuu p
  hao ni ma sharobaro tu hawana jipya viongozi wao utasikia wakhimiza migomo mwisho wanaitwa ikulu tena wanaenda kuchukuliwa na gari za state wakiingia na kile kiyoyozi ukiangalia gari zao azijawasha a//cmwaka wa tatu wakifika wanakamata cheki zao wanarudi turudini jamani tuwape miezi sita..usiamini hao hata mmoja ..wasanii watupu kama wakina tucta
   
 5. T

  Topical JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Watafanikiwa kwa majadiliano serikali haina tatizo na majadiliano
   
 6. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Wabunge na hizo sitting allowance wamechokoza moto!
   
 7. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mabehewa yameanza kuinga sasa. Hofu yangu yataunga mengine mengi tu hapo mbeleni kudai maslahi ya wafanyakazi. Bunge lilianza kujadili ongezeko lake, madaktari wakadai haki zao, sasa walimu kwanini wasidai yao? Hatari ni kwamba serikali haina fedha na wafanyakazi hawatakubali hilo.

  Watakubali vipi! wakati wawakilishi wao walithubutu kujibadilishia viwango vya maslahi kwakuwa wao ndio wawakilishi wa wananchi! Naam! ndio bwana wakubwa hao ni stahiki kuishi na hadhi ya wadhifa wako si ndio? Sasa wanowatumikia wananchi wafanye nini?

  Amini, si bunge wala Serikali itayoweza kupinga madai ya ongezeko la maslahi ya wafanyakazi itakuwa ni migogoro tu. Hapa Raisi hawezi kukwepa inabidi Serikali izungumzie kwa ujumla wake haya mamishaara yanapatikanaje patikanaje? Mzoa taka 10,000; housegirl 30,000; posho 300,000
   
 8. satellite

  satellite JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  weraweraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!bunge nalo litagoma?polisi je?baba Liz mwaka huu wako
   
 9. satellite

  satellite JF-Expert Member

  #9
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Maisha magumu kwa kila mtanzania.wahadhiri vipi na nyie hamgomi?maana mziki wa wanafunzi wahadhiri wakigoma pale magogoni patachimbika
   
 10. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #10
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,494
  Trophy Points: 280
  hata mimi naona toka mwaka 2010 ahadi yao imetekelezwa
   
 11. Eddy Love

  Eddy Love JF-Expert Member

  #11
  Feb 8, 2012
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 12,864
  Likes Received: 6,315
  Trophy Points: 280
  C wamelizuia hlo gazeti leo kutoka
   
 12. chubulunge

  chubulunge Senior Member

  #12
  Feb 8, 2012
  Joined: Dec 30, 2011
  Messages: 132
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbona serikali haikukubali kufanya majadiliao na dr waliofanya mgoma,serikali hii si sikivu na haiwezi kufanya majadiliano na walimu imekuwa ikiwapuzaa walimu siku nyingi kwa ubabe wao,so walimu they have to fallow wht dr do
   
 13. k

  kula kwa tindo JF-Expert Member

  #13
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,330
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ni ckivu kwa Mamy Kiroboto...
   
 14. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #14
  Feb 8, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hawa wameishiwa hela ya kula wanata kikao kiitwe cha muafaka kisha wapewe posho watoe matamko kuwa serikali imekubali kulipa kwa hiyo tuwe na subira ndefu

  hawana jipya kabisa hawa kumbuka Dec walitoa tamko kama hilo hilo
   
 15. T

  Topical JF-Expert Member

  #15
  Feb 8, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Majadiliano watafanikiwa, wakigoma kama dks hawatafanikiwa; madkts hawatafanikiwa trust me watarudi kazini wenye kupenda wasiopenda wajenga hospitali zao walipane wapendavyo..lol..

  JK anawabembeleza laiti ingekuwa mimi wangesharudi kazini after all, wanaotakiwa kuboresha sehemu ya kazi ni kanisa through MoU public funds hawakufanya hivyo wamekula pesa...kama kawaida makanisa kwa ufisadi..

  Naona vyombo vya habari hawataki kuandika kuhusu cssc (christian social services commision) walivyoshindwa kuboresha mazingara ya kazi KCMC, na Bugando wameanza kuisingizia serikali..lol
   
 16. S

  SINGOGO Member

  #16
  Feb 8, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa kutumia elimu yangu ya uchumi napendekeza yafuatayo: Serikali iboreshe maisha ya watu kupunguza madai maana watumishi wakidai nyongeza za mishahara mfumuko wa bei utakuwa juu na nyongeza nyingine itahitajika so kutakuwa na mzunguko wa kudai nyongeza za mishahara.
   
 17. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #17
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda hii na kubadilisha Sahihi yangu.

  Kama hujui kuomba chako basi KUFA. Muda ni sasa hivi, na wewe ongeza urefu wa kamba yako ili ule nyasi za mbali.

  TUMBO MBELEEEE, TAIFA LA TANZANIA NYUMAAAAAA. Asanteni
   
 18. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #18
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jamani wasaidizi wa maofisi ya serikali na makuli na wale wengine mnaofanya kazi za vibarua na kulipwa shillingi 1000 au 2000 kwa siku mdai nyongeza ya mishahara ya kima cha chini kwa mfanyakazi sekta zote binafsi na serikalini. Wafanyakazi wa taaluma zote sasa wajitokeze, huu ndio wakati muafaka wa kudai chenu, maana hili wimbi likipita ndo basi tena., asiyekuwepo......
   
 19. R

  RMA JF-Expert Member

  #19
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Polisi na ninyi je mishahara yenu inawatosha? Someni makala hii ili mpate akili!!!

  Waraka maalum kwa Askari wote - Na Samson Mwigamba


  MAKALA hii ilikuwa itoke Jumatano ya wiki iliyopita lakini kwa sababu za kiufundi ikashindikana. Imekuwa ni bahati nzuri kwamba inapotoka leo, ijibu swali la askari polisi dereva wa gari la maji ya kuwasha.

  Askari huyo alimweleza Mwalimu Mkuu wa watu jinsi roho inavyomuuma pale anapowamwagia Watanzania wenzake maji hayo ya kuwasha wakati wakidai haki yao. Askari uliyeuliza na wenzako wote someni makala hii kwa utulivu. Huu ni waraka maalumu kwa askari wote wa majeshi yote vikosi vyote Tanzania Bara na Visiwani.

  Kwa lugha ya wazi zaidi nazungumza na askari wa Jeshi la Polisi Tanzania, Askari wa Jeshi la Kujenga Taifa, askari wa Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo (KMKM), askari wa Jeshi la Magereza na wale wa Jeshi la Wananchi (JWTZ).
  Kuwa mwanajeshi lolote kati ya hayo niliyoyataja si dhambi na si kweli kwamba kuwa mwanajeshi kunakuondolea uwezo wa kufikiri na badala yake ukawa unafikiriwa na watu wengine.

  Wala haimaanishi kuwa askari kuwa kama robot ndio nidhamu bora kuliko zote duniani. La hasha! Mimi nilikataa utumwa huo!

  Mwaka 1999 nilihitimu elimu ya cheti cha ufundi mchundo, yaani Full Technician Certificate (FTC) katika uhandisi wa Elektroniki na Mawasiliano ya Anga, yaani Electronics & Telecommunications Engineering kutoka Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT).

  Nikiwa bado sijapata kazi ya maana, mwezi Aprili mwaka 2000 niliona tangazo la kazi ya Radio Technician katika Jeshi la Magereza. Nikatuma maombi na kuitwa kwenye usaili uliofanyika Chuo cha Maofisa wa Jeshi la Magereza Ukonga, Dar es Salaam mwezi Juni 2000.

  Wote tuliofaulu usaili tulipangiwa siku ya kuripoti Chuo cha Magereza Kiwira kule Tukuyu, Mbeya.

  Kufika kule nilishuhudia mambo ya ajabu. Ingawa wao hufurahia na kusema eti wanakutoa uraiani na kuwa mwanajeshi lakini baadhi ya matendo yanayofanyika wakati wa mafunzo ya jeshi ni ya kuwapumbaza askari wetu ili baadaye wakiwa kazini, watawala wawatumie watakavyo.

  Nilishindwa kuvumilia kaulimbiu ya wakufunzi wa jeshi pale walipoelekeza kwamba chochote kruta (askari mpya mafunzoni) unachoambiwa lazima uitikie "ndiyo afande". Nilishindwa kuitikia kwa mfano pale mkufunzi mmoja mwenye cheo cha koplo alipotutamkia mfululizo wa sentensi zifuatazo:
  Mkufunzi: Nyinyi makruta mbona wote hamkuja na majembe?
  Makruta: Ndiyo afande!
  Mkufunzi: Hamkuambiwa makao makuu ya jeshi kwamba lazima mje na majembe?
  Makruta: Ndiyo afande!
  Mkufunzi: Kwa hiyo kwa kuwa hamkuambiwa na nyinyi hamkuyabeba?
  Makruta: Ndiyo afande!
  Mkufunzi: Wote ni wapumbavu pamoja na mama zenu waliowazaa.
  Makruta: Ndiyo afande!

  Ni hayo pamoja na mambo mengine ya kulazimishwa kwenda kwenye kile kinachoitwa disko, ambapo pamoja na uchovu wa kutwa nzima wa kazi ngumu na nyingi bado ni lazima ukae hapo mpaka saa 4 usiku tena ukinyooshewa kidole tu na mwenzako lazima usimame na kuimbisha wimbo tena kwa tabasamu, wimbo mmoja wapo ukisema "Magereza ninavyokupenda nitakunywa sumu juu yako", ndiyo yaliyonifanya nikakataa kazi ya jeshi baada ya wiki moja tu ya mafunzo.

  Siku niliyokataa jeshi ilikuwa ni Jumatano asubuhi ambapo sikwenda mchakamchaka na wakati wenzako wanatawanyika kufanya usafi wa nje maeneo mbalimbali, mimi nilibeba begi langu na kuanza kuondoka chuoni majira ya saa moja na nusu hivi asubuhi.

  Nilikamatwa na mkufunzi mmoja wa jeshi na kupelekwa pamoja na begi langu kwa Ofisa Mafunzo wa chuo. Aliponiuliza sababu nilimtajia mbili, kwanza kwamba sifurahii mambo ya jeshi na kubwa zaidi kwamba mimi ni Msabato na nimeambiwa na wenzangu kwamba hapa hakuna kwenda kusali, siku zote za juma ni kazi.

  Kitu ambacho sitaweza maana Sabato takatifu lazima nipumzike! Bila kuuliza zaidi aliconclude kwa kuniambia kwamba, "Sijawahi kuona mtu anaacha kazi kwa ajili ya mambo ya dini.

  "Ni dhahiri wewe ulikuja kutupeleleza na hivyo kazi yako imeisha sasa unataka kurudi. Tutakuweka rumande, tena ile ya polisi kwa wiki mbili wakati tunafanya upelelezi juu yako."

  Askari aliyenileta alianza kunivuta ili kunipeleka rumande lakini nilikataa huku nikiendelea kujieleza kwa ofisa mafunzo ili ajue kwamba sikuwa na mpango huo aliousema.

  Baada ya kuelemewa na hoja zangu alinipeleka kwa makamu mkuu wa chuo ambaye yeye alitumia zaidi Biblia kunihubiri kwamba nakaidi amri ya mamlaka wakati hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu.

  Jibu langu lilikuwa fupi na lenye msimamo mzito kwamba ikiwa mamlaka ya wanadamu inafika mahali inanena tofauti na Mungu, Mtume Petro ametuandikia kwamba katika hali ya namna hiyo, "Imetupasa kumtii Mungu kuliko mwanadamu".

  Na yeye alinishindwa akanipeleka kwa mkuu wa chuo na wao wote wakiwapo. Ushauri waliokuwa wakimpa mkuu wa chuo ni kwamba mimi niwekwe rumande kwanza ili wafanye upelelezi. Lakini sikuyumba katika msimamo wangu.

  Nilimweleza mkuu wa chuo kwamba mimi ni raia na si mpelelezi. Nilizirudia rudia sababu zangu za kuacha jeshi tena kwa ujasiri mkubwa na kumhakikishia mkuu wa chuo kwamba akinipa hayo ninayoyataka niko tayari kubaki jeshini.
  Hatimaye kauli ya mwisho ya mkuu wa chuo ilikuwa ni hii: "Jeshi ni wito. Tunaweza kumlazimisha huyu kijana kuwa mwanajeshi lakini baadaye ikatuletea madhara makubwa sana." Akamalizia kwa kusema, "chukueni maelezo yake kwa maandishi kisha arudishe vifaa vya jeshi."

  Wakati naondoka nilimsikia ofisa mafunzo akitoa maelekezo kwa walio chini yake kwamba mwanafunzi mwingine wa jeshi akija kuripoti na kwenye daftari akajaza kwamba ni Msabato, msimsajili kwanza mpaka aje kwangu! Sijui kama Wasabato wameendelea kupokewa kwenye hicho chuo cha magereza lakini ninachotaka askari wote wa majeshi yetu yote na vikosi vyote, ni kwamba askari unaweza kusimama kwa miguu yako na kufikiri kwa akili yako mwenyewe!
  Ndugu zangu askari, nchi imefika mahali ambapo Waingereza hupenda kupaita ‘critical point'. Ni mahali ambapo wananchi wako tayari kwa mabadiliko na watawala wako tayari kwa mapambano ili kubaki madarakani.

  Katika point hii askari wetu wanakuwa na nafasi kubwa ya aidha kuwezesha mabadiliko hayo kutokea kwa wakati wanaoutaka wananchi, tena kwa amani ama kuyachelewesha (si kuyazuia) na kusababisha yatokee baadaye kidogo kuliko wananchi walivyotaka, tena baada ya kumwaga damu nyingi ya Watanzania wasio na hatia!

  Napenda kurudia kwamba hakuna jeshi lolote duniani hata kama tungekusanya majeshi yote ya dunia hii na kuyaleta Tanzania hawataweza kuizuia nguvu ya umma pale inapokuwa imeamua kufanya mabadiliko.

  Napenda tena kurudia kwamba si lazima askari mfanye kile ambacho wakubwa wenu wanataka na kuwaamuru kufanya. Tunaweza kusimama imara na kutetea haki za Watanzania tukiwamo na sisi askari. Niliwahi kugoma kutii amri ya kukamatwa na kuwekwa rumande.
  Lakini pia mifano ni mingi na nisingependa kuchukua mifano kutoka nchi za Ulaya kama Uingereza ambako tulishuhudia wananchi wakiandamana mitaani na askari wao hawakuwahi hata kumpiga kofi tu mwandamanaji hata mmoja.
  Walipohojiwa na vyombo vya habari walisema dhahiri kwamba waandamanaji ni raia halali wenye haki ya kufanya kile wanachokifanya kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi yao. Katiba ya Tanzania na sheria za nchi hii zinatoa haki kama zile za Uingereza. Tofauti ni utekelezaji wa matakwa hayo ya kikatiba na kisheria. Watawala wa Uingereza wako tayari hata kung'oka madarakani ili kutekeleza matakwa ya nguvu ya umma.

  Lakini wale wa Tanzania wako tayari kung'oa uhai wa raia wengi ili mradi kuzuia nguvu ya umma inayodai haki na wananya hivyo kwa sababu ya hofu ya kung'oka madarakani, jambo ambalo hawataki kabisa kulisikia. Na ndugu zangu askari napenda kuwaambia kwamba yote yanafanywa na watawala wetu kwa kuwategemea nyinyi.

  Wanaminya haki zenu nyinyi wenyewe, haki za wazazi wenu, dada na ndugu zenu, marafiki zenu, jamaa zenu na majirani zenu. Chukulia mfano rafiki zangu Mtaki na Edwin. Tumesoma wote shule ya msingi pale Magu.

  Nilichaguliwa kujiunga na Mazengo Sekondari, shule kubwa na ya muda mrefu ambayo sasa imegeuzwa kuwa chuo kikuu bila mabadiliko ya majengo.

  Shule iliyokuwa na maabara nne kwa maana ya maabara ya baiolojia, kemia, fizikia na jiografia. Ilikuwa ni sekondari ya ufundi na hakuna karakana ambayo haikuwapo.

  Shule iliyokuwa na walimu wa kutosha, vyumba vya kutosha vya madarasa na vya kulala mabwenini.
  Katika bweni la Ujamaa kwa mfano, nilikokuwa naishi mimi, kuna vyumba kadhaa havikuwa na watu. Darasa la Form IVA ambalo nilikuwamo lilikuwa na wanafunzi 21 tu darasani.

  Na mazingira mengine mengi ambayo sitaweza kuyataja hapa ambayo yanafanya wanafunzi wa leo wa Chuo Kikuu cha Mt. John wajiulize kama kweli ile ilikuwa ni shule ambayo haina maktaba wala vitabu vya kutosha, na mengineyo mengi mnayoyafahmu.

  Nikafaulu kwa kiwango cha daraja la juu lililoniwezesha kuendelea mpaka chuo kikuu na kupata kazi nzuri kwenye Umoja wa Mataiifa.

  Rafiki zangu nakumbuka mlivyoamua kujiunga na Jeshi la Polisi si kwa sababu mlipenda kazi hiyo ama kwamba mlikuwa na wito wa kuwa polisi kama mnavyodanganywa kwamba jeshi ni wito.

  Nakumbuka mlijiunga huku mkilalamika kwamba mnalazimika kujiunga huko kwa sababu kiwango chenu cha ufaulu hakiwapi fursa ya kazi bora zaidi ya hiyo. Lakini mimi nawafahamu vizuri. Najua uwezo wenu wa darasani. Mliathiriwa na mazingira ya hovyo ya shule mlizosoma.

  Rafiki zangu nyinyi wote leo ni wakuu wa vituo vikuu vya polisi vya wilaya katika wilaya za Mbozi na Igunga.
  Leo hii mimi nimeacha kazi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kushiriki vema katika mapambano ya kutafuta ukombozi wa taifa hili.

  Wadogo zenu na wadogo zangu mnawajua wako katika juhudi za kutafuta maisha lakini ni magumu. Wengine walikosa kabisa nafasi ya kujiunga hata na hiyo Magu Day.

  Wakaishia Bulima na Kinango, ambako hali ilikuwa mbaya zaidi. Wakafeli kabisa na leo wanahangaika hapa na pale lakini watawala wanawawekea mazingira magumu mno ya kuendesha maisha.

  Na sasa chukulia nao wametambua hali yao duni inasababishwa na watawala walafi na walaghai. Wamejaribu kutumia njia za kidiplomasia kudai haki zao wanakutana na watu wanaitwa wakuu wa wilaya na mikoa.

  Wanaamua kuandamana, mnashiriki kuamrisha askari walio chini yenu kuwapiga na kuwaweka rumande na hatimaye kuwafungulia kesi za kubumba!

  Askari wetu igeni mfano wa askari wa Misri! Pale wananchi walipoamua kuandamana kukomesha utawala wa kidhalimu wa miaka 30 chini ya Hosni Mubarak, askari waliwalinda badala ya kuwapiga.

  Walikataa kwa sababu hata wao walikuwa wakiumizwa na Mubarak lakini zaidi ya hayo, waliokuwa wakiandamana walikuwa ni dada zao na ndugu zao na marafiki zao.

  Hivi sasa nchi iko njia panda. Ugumu wa maisha umeongezeka mara nne na zaidi. Watawala hawalioni hilo wala hawajishughulishi kurekebisha hali ya mambo hususan hali ya uchumi.

  Wako busy na kujiandaa kwa uchaguzi wa 2015. Mawaziri wako busy na kampeni za kuteuliwa kuwa wagombea wa urais kupitia chama tawala hapo 2015 na rais naye yuko busy kuandaa mtu wake ambaye anadhani akimrithisha jumba jeupe la pale Magogoni atasema mwacheni Ndugu Kikwete apumzike kwa amani.

  Taifa limeamua kuandika katiba mpya, rais na serikali yake na chama chake wameamua kuuteka mchakato ingawa haikuwemo kwenye ilani yao ya uchaguzi ili tu waturudishie katiba ya mwaka 1977 na kuipa jina juu ya jalada KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 2014.

  Natambua juhudi zinazoendelea hasa zikiongozwa na CHADEMA kujaribu kumkumbusha rais kwamba katiba iko juu yake na katiba ni mali ya wananchi na yeye anaajiriwa kwa katiba hiyo na si yeye kujiandalia katiba ili atawale kwa ulaini.

  Lakini juhudi za kidiplomasia zikishindikana hapo ndipo itabidi haki ya watu idaiwe kwa maandamano na hapo askari wote tuungane na kuwa kama Misri, kwa kuwa Katiba mpya ni kwa masilahi yenu pia! Jaribuni kutafakari!
   
 20. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #20
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  oluoch na wenzako KINA Mkoba msifurukute your time is up mmeshindwa kuendesha CWT na kuangalia matumbo YENU this time lazima tuwapige chini matatizo ya walimu yanaanzia na CHAMA CHA WALIMU na mlivyozoea posho mnazolipana hivi mtaweza kurudi kushika chalk..... NAFKIRI mmeshauona moto wa walimu vijana ndo huo tunakuja nao no stone will left unturned Kabla hatujaanza na serikali tunaweza na CWT
   
Loading...