Walimu wataka Waziri awajibike wizi wa malipo kwa walimu hewa

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,138
Walimu wataka Waziri awajibike wizi wa malipo kwa walimu hewa

Na Gedius Rwiza

CHAMA cha Walimu Tanzania CWT, kimemtaka Waziri wa Nchi katika ofisi ya Rais (Menejimenti na Utumishi wa Umma), Hawa Ghasia, kuwajibika kwa hasara ya Sh477 milioni ambaye serikali imeingia kwa kuwalipa walimu hewa.


Naibu Katibu Mkuu, Ezekiah Oluoch aliliambia gazeti hili kuwa tamko la waziri huyo kwamba serikali imepata hasara hiyo, ni ishara ya uzembe katika ofisi yake.


Alisema CWT imeshindwa kuielewa kauli hiyo hasa ikizingatiwa kuwa Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ndio inayoshughulikia masuala yote yanayohusu watumishi wa serikali wakiwemo walimu.


“Kauli hii haiingii akilini hata kwa mtu asiyefahamu taratibu za utumishi. Ofisi Waziri Ghasia ndio inayoshughulika na kumbukumbu za wafanyakazi wote wakiwemo walimu, iweje fedha zilipwe kwa wafanyakazi hewa halafu waziri aone fahari kulitangaza hilo,” alihoji Oluoch.


Alisema kwa kawaida, kila halmashauri nchini inakuwa na kumbukumbu za walimu wote wakiwemo wale waliacha kazi.


“Kumbukumbu hizo ni pamoja na za walimu kuajiriwa au kuacha kazi na zinapelekwa katika wizara hiyo na Ghasia kwa wadhifa wake alipaswa kulijua hilo mapema kabla ya kuiingizia nchi hasara hiyo ya mamilioni,” alisema kiongozi huyo wa CWT.


Oluoch alisema serikali inapaswa kufanya uchunguzi ili kubaini watumishi waliochota fedha hizo na kuwachukulia hatua.


“Waziri Ghasia anapaswa kutoa maelezo ya jinsi fedha hizo zilivyolipwa kwa walimu hao, hili hawezi kukwepa kwa kuwa ndiye anayewajibika,”alisema Oluoch.


Kauli hiyo inafuatia tangazo la hivi karibu la waziri Ghasia la kuwafukuza kazi walimu 463 waliokosa fisa na ambao wameisababishia serikali hasara ya Sh 477 milioni
 

download

Yesu akiwa chini ya ulinzi huku picha ndogo ikionyesha mmoja wa majeruhi akipandishwa kwenye ambulansi.
Thursday, June 04, 2009 5:05 AM
Jamaa mmoja wa Marekani anayejiita Yesu Kristo amewaua watu wawili na kujeruhi watu saba wakati alipovurumusha risasi kwenye chumba cha wanawake wanaosubiria kutoa mimba zao huku akisema 'Ingekuwaje kama bikira maria angeamua kuitoa mimba yangu, je

Jamaa huyo anayejiita Yesu Kristu au Massiah akiwa amevalia kama Yesu, aliingia kwenye kliniki ya utoaji mimba ya Huntsville na kuanza kupiga risasi hovyo kwenye chumba cha mapumziko ambacho wanawake wajawazito hukaa humo wakati wakisubiria kutoa mimba zao.

Walinzi katika kliniki hiyo walifanikiwa kumwahi Yesu Massiah kabla hajaikoki tena bunduki yake Glock 9mm aliyoinunua kihalali kwenye duka moja nchini humo.

"Kutoa mimba ni dhambi" alisema Yesu wakati alipokuwa akipelekwa kituo cha polisi baada ya kukamatwa akiwa amefungwa pingu na kuongeza "Ni kitu ambacho siwezi nikakifumbia macho".

Mashuhuda wa tukio hilo walisema kwamba jamaa huyo aliibuka ghafla na kuanza mashambulizi yake ambayo yalipoteza maisha ya Dr. Nelson Woodring, 51, na nesi Danielle Costa, 29.

"Alikuja kwenye meza ya maulizo na kuuliza kama anaweza kumuona Dr. Woodring," alisema mhudumu kwenye meza ya maulizo na kuongeza "Kilichofuatia baada ya hapo alikuwa akisoma mistari ya biblia huku akipiga risasi kwa kila kitu alichokiona".

"Hali ilikuwa inatisha sana " alisema nesi mmoja ambaye alipigwa risasi ya mkononi na tumboni na hivi sasa amelazwa hospitali akipatiwa matibabu.

"Alimfata Dr. Woodring na kuweka mikono yake kichwani mwake na kumwambia "Nimekusamehe madhambi yako" halafu akampiga risasi kwenye paji la uso".

Maafisa polisi wa Huntsville hawajapata jibu Yesu huyo aliingiaje na silaha kwenye kliniki hiyo pamoja na kwamba kuna ulinzi mkali getini na kukiwa na kamera za ulinzi kila kona.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye selo yake Yesu alisema kwamba hajutii hata kidogo kwa mauaji aliyofanya.

"Kama nilivyosema kwenye John 16:21, maisha ya kila kitu ni ya thamani sana , sio tu kwa wale ambao wameishazaliwa, baba yangu, Mungu anafikiria kama ninavyofikiria".

Yesu aliendelea kusema: " Ingekuwaje kama bikira Maria angeamua kuitoa mimba yangu, ningezaliwa?, inawezekana alifikiria kama hivyo lakini aliamua kutoitoa mimba yake na kunizaa, alifanya jambo sahihi kabisa, kukaa na mimba yake hadi mwisho na kuipatia dunia mkombozi, ni mwanamke aliyebarikiwa sana "

Kwa mujibu wa wataalamu wa sheria, Yesu anaweza akahukumiwa adhabu ya kifo iwapo atapatikana na hatia.

"Kwa jaji sahihi na waendesha mashtaka wazuri Yesu atauliwa tena kwa mara nyingine" alisema profesa wa sheria wa chuo kikuu cha Michigan Profesa Arthur Lipscomb.

Yesu kwa upande wake amesema kuwa haogopi adhabu ya kifo na kusema "Niko tayari kufa kwaajili ya dhambi za wengine".
 
Back
Top Bottom