Walimu wasusa kusahisha mitihani ya mock kanda ya mashariki.

drmkumba

Member
Dec 27, 2010
52
1
Katika kile kinachoonekana kutokurudi nyuma katika kupigania haki zao,walimu ambao waliitwa kusahisha mitihani ya mock kidato cha sita kanda ya mashariki ikijumuisha mikoa ya Morogoro na Pwani wiki iliyopita waligoma katakata kufanya zoezi hilo pale Ruvu sec.

Kwa mujibu wa mmoja wa walimu hao alinukuliwa akisema kwamba wamegomea kufanya kazi hiyo kwa sababu kwa kipindi kirefu wamekuwa wakinyonywa na waratibu wa mitihani hiyo ambao ni wakuu wa shule (TAHOSA EASTERN ZONE) kwa kuwalipa kila karatasi ya majibu ya mtahiniwa mmoja (script) inayosahishwa kwa Tsh 350/= tu.

Amedai kwa sasa waliwataka waandaji hao waongeze kiasi hicho kama sivyo walimu hao wangefungasha virago na kurudi waliko toka.

TAHOSA hawakuwa tayari kuongeza kiasi chochote cha senti kitu ambacho kiliwafanya walimu hao wasusie zoezi hilo nakubeba mabegi yao then kurudi walikotoka.
 
hatutaki tena kusikia mambo ya wengine wafanye kazi wengine wale bure. Tutafika kwa kila mmoja kupigania haki yake.
 
Bado kwenye uchaguzi 2015 CCM walishazoea walimu ndio msaada wao mwaka 2015 hakuna haja ya ulinzi walimu wanatosha kabisa
 
Mimi nadhani upo mwongozo wa serikali ambao unaanisha malipo anayotakiwa kupewa mfanyakazi anapokuwa nje ya kituo chake cha kazi kwa ajili ya kutenda majukumu yake ya kikazi. sasa ni kwa nini waraka huo usitumike Kuwalipa waalimu??. Nani aliyeleta utaratibu wa kulipana kwa idadi ya script zilizosahihishwa? je hamuoni kwamba mwalimu atalipua ili asahihishe japo scripts 100 kwa siku ili apate walau tshs 35,000/= ambayo kwa mimi naona haitamtosha yeye na familia yake aliyoicha nyumbani. Sasa nimepata jibu ni kwa nini kuna wanafunzi waliopo sekondari huku wakiwa hawajui kusoma na kuandika. Naomba tuanze kwa warrant holder aliyeidhinisha huo utaratibu,Pili twende kwa huyo mhasibu aliyeshindwa kumshauri boss wake kuhusu huo ukiukwaji. Tatu kwa wakaguzi wa ndani na nje ambao hawakuukosoa, na katibu mkuu wa wizara Wakishaachia ngazi tuwaombe radhi waalimu warudi kuendelea na kazi . Nawasilisha
 
Back
Top Bottom