Walimu wasipoangaliwa wataliangamiza taifa kwa kuzalisha wajinga!!!???

rifwima

JF-Expert Member
Apr 21, 2010
507
212
Huu ni ujumbe wao unaosambazwa kwa kasi sana kwenye mitandao na simu baada ya Serikali kutupilia mbali mdai yao ya msingi:

"Ndugu Mwalimu, katika somo au masomo yako hakikisha humwandai mwanafunzi kupata A,B,C wala D. Mwandae katika kiwango cha F kwa sababu hata akipata A juhudi zako ni sawa na bure. Hii ndo silaha yetu ya mwisho. TUMA MSG HII KWA MWALIMU YEYOTE"

Kama serikali haitaliangalia hili swala kwa makini - Kuna hatari kubwa sana katika taifa hili.
 
hali ni mbaya serikali inabidi ikae tu chini na waalimu c huwa rais anasema serikali yake ni serikali sikivu akae basi na hawa waalimu kabla mambo hayajaharibika kikubwa awasikilize wanataka nini na kuwe na uwazi na ukweli kwenye mazungumzo yao hayo
 
mwalimu ni daraja muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa lolote lile duniani isipokuwa Tanzania.Inaonekana juhudi za kukomboa taifa zinawezekana tu kwa kualika wageni kukalia nchi yetu, na ili kufanikisha hili,elimu kwa mzawa lazima iangamizwe na kuunda Taifa la wajinga wengi na watu tegemezi.Tatizo la walimu ni la Watanzania wote na linahitaji nguvu ya umma bila hivyo tunaiuza nchi yetu-Wtanzania tuamke sasa
 
Mbona hata watu wazima wajinga tayari???una werevu gani wewe usiyejua hata umaskini wako unaletwa na nn???
 
walimu hawawezi fanya upuuzi kama huo. Haya ni maneno tu ya wahuni wa mtaani!
 
walimu hawawezi fanya upuuzi kama huo. Haya ni maneno tu ya wahuni wa mtaani!


Unasema usemayo kwa sababu unauhuru na umeshiba.

Kuna idad kubwa ya walim wananjaa watafundisha watafundisha vipi? Wanahitaji kupata huduma za lazima kutoa huduma bora.
 
Back
Top Bottom