Walimu wapya Wilaya ya Mbinga hatujapata mishahara, Waziri Jafo tuaomba ushughulikie hili

Nimeongea na mtu mmoja analia. Hata nguvu ya kuingia darasani kesho na kesho kutwa hana.

Yuko Kijijini kabisa hakuna hata zahanati wala Umeme.
Alihakikishiwa atapewa na Afisa Elimu Leo wote wamepewa lakini yeye bila bila. Afisa Elimu anamwambia avumilie maana hata wao walikaa sana enzi zao.

Nilifikiri ni njama kumbe ni kitu planed kama hata huko mnalia. Mwezi wa Tatu sasa bila mshahara. Alafu umemtupa porini.

Hapa nimeona hii nchi haiko siriasi na Elimu kama wanavyosema kwenye mabarabara. Shule inawanafunzi 800 walimu saba. Anaongezeka mmoja kuingia Kijijini anafundisha humlipi. Na wenzake wanamuhakikishia hata ukilipwa hutapewa hizo mishahara zilizopita. Utaomba na maombi yatatelekezwa.

Hakuna Kukata tamaa
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom