Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Jambo hili limezua mashinikizo ya damu na hata vifo. Sababu kubwa inayotolewa na serikali katika zoezi hili ni kuwa kuna mlundamano wa walimu sekondari na uhaba wa walimu shule za msingi. Labda ni rahisi kuelewa hilo na kusema kimsingi, labda ni jambo jema kufanya namna fulani ya kusawazisha. Lakini ukweli ni kwamba kuna mambo ya kutafakari;
Na je, serikali imefikiria athari za kuwapeleka hawa walimu wa sekondari kwenye shule za msingi wakasimamiwe na wakuu wa shule ambao ni wadogo kwao ki-daraja? Mwalimu gani wa sekondari ataona ni sawa kwenda kuamriwa na mwalimu mkuu wa msingi akijua kwamba anamzidi kidaraja? Je serikali yetu katika upofu wake wa kuongoza haijaona kwamba inatatua tatizo kwa kutengeneza tatizo huko mashuleni msingi?
Tukirudi katika suala la haki za raia wa Tanzania, kinachofanywa na serikali ni uonevu uliopita mipaka. Najiuliza, chama cha walimu kiko wapi? Kwa nini hamjaenda mahakamani kupinga hili suala? Kwa nini hamjaitisha mgomo wa walimu wote wa sekondari nchini kupinga na kulaani jambo hili?
Kama serikali iliona kuna tatizo la usawaziko kati ya sekondari na msingi, basi ilipaswa ihamishe walimu kwa hiari yao, labda kwa kuwapa motisha ya fedha kwamba kutakuwa na nyongeza ya 30% kwenye mshahara wa mwalimu atakaekubali uhamisho wa namna hii, zaidi ya marupurupu ya uhamisho. Huenda tungekuwa na walimu wengi wa kujitolea kuhama kwa hiari. Lakini huwezi tu kuamua kwa ubabe kwamba kwa kuwa una madaraka nakushusha cheo, nakuhamishia msingi toka sekondari, na sikupi hela ya uhamisho.
Raisi Magufuli alikuwa mwalimu wa sekondari miaka kadhaa iliyopita. Yeye angefurahia enzi hizo kufanyiwa jambo kama hili? Kwa nini basi uwafanyie wengine jambo ambalo wewe binafsi usingekubali ufanyiwe?
Huu ubabe wa serikali unazidi sasa, na umefikia hatua ya kutovumilika.
Kama serikali inaona hili ni sawa, basi iende hata jeshini JWTZ na kuwaambia wanajeshi wenye rank za Major wanaosimamia kombania (company) na kuripoti kwa Luteni Kanali sasa wanaweza kuhamishwa, bado wakiwa Major, na kwenda kusimamia Platoon na kuripoti kwa Captain na mshahara wao hautabadilika.
- walimu wanahamishwa kwa lazima bila kuwa na uraratibu waliokubaliana na mwajiri
- walimu wanaohamishwa wanalazimishwa kuhama bila kupewa fedha za uhamisho
- walimu wanaohamishwa wanaenda msingi kuwa walimu wa kawaida huku wakisimamiwa na headteacher ambaye kidaraja ni mdogo kwao