Walimu Wanaokwenda Kusoma Bila Ruhusa Ajira Mashakani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walimu Wanaokwenda Kusoma Bila Ruhusa Ajira Mashakani

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by tatanyengo, Sep 27, 2012.

 1. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Walimu mnaokwenda kujiendeleza katika vyuo vikuu na vyuo vingine mnapaswa kuomba ruhusa katika mamlaka husika. Bila kufanya hivyo, mtahesabiwa kama watoro kazini na hivyo kuiweka ajira yenu rehani. Naibu waziri wa Elimu Mh. Phillipo Mulugo atahakikisha kwamba utaratibu huo unazingatiwa.

  Kwa uzoefu nilionao ni kwamba hata wale wanaoomba ruhusa wengine huwa wanatiliwa ngumu na wakubwa wao kuanzia kwa wakuu wa shule, maafisa elimu, wakurugenzi nk. Unaweza ukaambiwa shule ina mwalimu mmoja tu wa somo fulani sasa ukiondoka nani atafundisha au wewe hauko kwenye mpango mwaka huu na sababu nyinginezo.

  Sasa ndugu zangu uamuzi ni wako: uende kusoma ajira ikome na ukihitimu uanze upya au ubaki shuleni usiende kusoma.
   
 2. A

  AWIKA Senior Member

  #2
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 17, 2012
  Messages: 165
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Itakuwa vizuri kwa serikali kuweka utaratibu mfano miaka mitatu baada ya kuajiriwa mtu atakiwe kwenda kusoma pasipo kuzuiwa na mtu awaye yote.Kigezo cha Shule kutokuwa na waalimu wa kutosha kisiwe sababu,watafutwe wengine.
   
 3. J

  Joan Joel333 Member

  #3
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  babo hana hooja ya msingi mwalim kama ameshamaliza mda wake aruhusiwe kwenda kusoma kwani hawa DEO na wakurugenzi wana usumbufu sana, mfano kuna mwalimu moshi rural ambaye alishwekwa kwenye orodha ya watakoruhusiwa kwenda kusoma mwaka huu lakin alipokwenda kuomba release letter alikataliwa kwa madai hajaonyesha mfadhili wake wa masoma ni nani. mm naona ni ukiritimba tu kwan hamna anaeyeeenda chuon akiwa hajui ada lazima ilipwe na pia anawena akaomba mkopo n a akajisomesha . moshi rurul achen ukiritimba
   
 4. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  Hayo hayo ya kuajiliwa. Kasome ukirudi utaonambele kuna nini. Sasa unakaa bila elimu ili kesho iweje. Muulize Mulugo nini kilimtoa kwenye ajira yake akakimbilia ubunge. Wangelikuwa watoto wake angeliwazuia. Hopeless!
   
 5. Kijuche

  Kijuche JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2012
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 419
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ualimu Kenya bana. Tanzania magumashi tu.
   
 6. m

  matc JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2012
  Joined: Sep 14, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Mini mwathirika kabisa wa hilo..masomo yangu ni fizikia na hesabu,nilipotaka kwenda shule nikaambiwa walimu wa sayansi wakipatikana ndo niende..HIVI KUNA SIKU WALIMU WA SAYANSI WATAPATIKANA?Na hiyo ilikua ni mwaka 2009 na kibaya zaidi nilikua peke yangu kituon nikiwa na vipindi 103 kwa wiki wakati nilitakiwa kuwa na vipindi 24 tu.
   
 7. gbrother

  gbrother JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ki2 cha msingi na muhimu ni kuwa na maamuzi magumu, elimu ndio kila ki2 ndugu zangu, hizo ajira zipo bt muda haupo, umepata chuo nenda kapige kitabu, MISINGI YA KUWA NA MAISHA MAZURI SIKU ZOTE UWA INAKULAZIMU KUFANYA MAAMUZI MAGUMU, KAMU MUNGU ALIKUSAIDIA UKAPATA HIYO AJIRA ULIPOMALIZA DIPLOMA, JUA KAMWE HATAKUACHA UKIMALIZA DEGREE, NENDA KASOME NDUGU YANGU, UMETIMIZA MIAKA KUANZIA MIWILI NA UMETHIBITISHWA KAZINI, NARUDIA TENA NENDA KASOME
   
 8. s

  sugi JF-Expert Member

  #8
  Sep 29, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  Kuna baadhi ya shule unakuta headmaster au second master ni diploma holder na anaogopa kwenda shule kwa kuhofia nafasi yake kuchukuliwa sasa unadhani atakuacha ukasome???lazima akubanie tu!cha msingi kweli ni kufanya uamuzi mgumu,sometimes you have to take risk,sasa utakaa bila kusoma mpaka ln??au ndo unavizia nafasi za kusimamia,kusaisha n.k,we have to think beyond that friend!!GO TO SCHOOL
   
 9. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #9
  Sep 29, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Ni Ajabu jingine la dunia hili, yafaa tulipigie kura ili liingie kwenye maajabu. Ni tanzania pekee walimu hawatakiwi kujiendeleza kielimu wakati huu ambapo dunia ina badilika kwa kasi sana. Na kwa nini iwe ni walimu tu kujadiliwa suala la kusoma, je kada nyingine zikoje? Huyo Muhogo sijui mulugo yeye alifikaje huko bila ya kujiendeleza? Na alishafanya utafiti akagundua kwa nini walimu wanaondoka bila ya ruhusa?
   
 10. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #10
  Sep 29, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,198
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Utaratibu ni kwamba Unaweza kuwekwa kwenye mpango wa masomo baada ya miaka miwili tangu uajiriwe. Lakini jiweke kwenye nafasi ya DEO....Mwaka huu wameajiriwa Walimu 100 na wote baada ya miaka miwili wanastahili kwenda masomoni. Utawaruhusu wote wakasome? Kumbuka wapo wa mwaka jana na mwaka juzi hawajapata ruhusa bado. Suluhu sio kutoroka, omba mwaka mmoja kabla ili uwekwe kwenye mpango wa masomo. Kaka unataka kujilipia, eleza kwa uwazi kabisa. Mwaka unaofuata fanya application na ikifika mwezi June andika barua ya kukumbushia ruhusa, Usipojibiwa subiri admission letter ambatanisha tena kwenye barua yako... Kabla ya kuondoka kumbushia tena na tena kuhusu release latter. Ni mwajiri kichaa pekee ambaye hatakupata ruhusa. Ukiona DEO anazingua kaonane na Mkurugenzi au Mamlaka ya Ajira na Nidhamu kwa Walimu (Tume ya Utumishi wa Walimu). Kuacha kazi sio kitu rahisi kama watu wengine wanavyojaribu kutushawishi hapa....
   
 11. T

  TEGETA KIBAONI JF-Expert Member

  #11
  Sep 29, 2012
  Joined: Aug 12, 2012
  Messages: 622
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  UOGA wako ndio umasikini wako,mpaka ufundishe mipindi mingi namna hiyo kwa hela gani unayolipwa kaka/dada?achana nao badala yake fundisha vipindi vinavyoendana na ajira yako kisha Fikiria kufanya shughuli nyingine zitakazo kuongezea kipato badala ya kulilia kwenda kusoma ndugu yangu elimu uliyonayo inakutosha sana,fikiria distance learning na kukomaa kuitafuta shilingi zaidi kwani hata ukisoma bado mizenguo kibao kwenye kada hiyo,ni maoni yangu kwako tu.
   
 12. s

  sugi JF-Expert Member

  #12
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  tatizo la kuwa na mawaziri machizi/wana mtindio wa ubongo,umzuie mwalimu kusoma halafu utegemee elimu bora????
   
 13. M

  Msafwa wa swaya JF-Expert Member

  #13
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 4, 2012
  Messages: 426
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  kweli best mi nina miaka 5 kazn lakin ni miongon mwa watu ambao mpaka sasa hakielewek kitu kuhusu ruhusa napigwa karenda tu chuo kinafungua trh 1 nilichopanga kufika trh 7 bado nafanya maamuz magum boom nimepata et wananizingua sasa liwalo na liwe!
   
 14. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #14
  Sep 30, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Hii mada imenigusa sana kwa kweli mimi ni mhanga wa hili tatizo,ilibidi nichukuwe maamuzi magumu.Mijitu mingine ina roho mbaya sana.Ila malipo ni hapa hapa.
   
 15. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #15
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,784
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  walimu nao , wote mnataka kwenda kusoma shule tufunge? isitoshe uliajiriwa kwa sifa uliyonayo (hapa natania). siku hizi umekuwa mtindo hasa kwa walimu (wale masharubaru) akipangiwa asikokutaka huyoooo chuo kikuu ,wanasumbua kweli!
   
 16. BUMIJA

  BUMIJA JF-Expert Member

  #16
  Sep 30, 2012
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 2,661
  Likes Received: 459
  Trophy Points: 180
  Mimi nilifundisha matipwili bagamoyo kmm100 kutoka Dar,miaka4,nikaomba kusoma mwezi wa tisa nikapata na DEO Akanihamishia moreto lugoba,,akasema hutaenda kusoma hadi miaka3,n,likua na kadiploma,nikachapa mwendo,nina swali hivi mshahara ni nini,afe aliyekat
   
 17. BUMIJA

  BUMIJA JF-Expert Member

  #17
  Sep 30, 2012
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 2,661
  Likes Received: 459
  Trophy Points: 180
  Tutasoma tu,na wakate mshahara mana wanajua tunawapita Elimu,Mfikishieni taarifa DEO Wa bagamoyo kua afungue huo mshahara ama nimshushe busha wallah
   
 18. ndupa

  ndupa JF-Expert Member

  #18
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 4,448
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  jamni nadhani mmejifunza yaliyotokea kenya...chukua hatua!!!!
   
 19. BUMIJA

  BUMIJA JF-Expert Member

  #19
  Sep 30, 2012
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 2,661
  Likes Received: 459
  Trophy Points: 180
  MA DEO Wanaonea sana,nimekaa miaka4
  Sehemu haina umeme,haina gari ni bodaboda,simu uhnapanda juu ya mnazi.Lakini nimesoma naenda kuingia 2year.Ila nimedhulumiwa na sina wa kunisaidia,nimesoma kwa kula nikate UD Napiga buku kwa uchungu,Mungu ndie refa
   
 20. u

  usungilo JF-Expert Member

  #20
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 499
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 60
  ukisubiria sana utaishia kuwa mtumwa. Kuna jamaa alimaliza form four nikiwa form one,akaenda grade A. Toka hapo ni miaka zaid ya kumi imepita lakini wamemnyima ruhusa kwenda kusoma. Nilipokutana naye analalamika nilitamani kumnasa vibao!
   
Loading...