Walimu, wanafunzi walazimishwa kuhudhuria mkutano wa JK Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walimu, wanafunzi walazimishwa kuhudhuria mkutano wa JK Dodoma

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Oct 2, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wadau, nimeipata stori hii katika Tanzania Daima ya leo uk. wa 3:

  Ujanja wa CCM wagundulika

  N Mwandishi wetu, Dodoma

  MBINU chafu za Chama cha Mapinduzi (CCM), zinazotumika katika kukusanya na kujaza watu kwenye mikutano ya mgombea urais wa chama hicho, zimegundulika baada ya baadhi ya walimu wa shule za msingi mjini Dodoma kutoboa siri.

  Ilibainishwa jana mjini Dodoma, kuwa agizo limetolewa kwa walimu wote walioko kwenye shule zilizoko kwenye mji huo, kuhudhuria kampeni za mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete, kesho; huku onyo likitolewa kwa watakaoshindwa kuhudhuria kuwa watawajibishwa.

  Kwa mujibu wa baadhi ya walimu waliozungumza na Tanzania Daima, walimu wakuu wa shule walipokea ujumbe kutoka kwa waratibu wa elimu wa kuwataka watoe matangazo kwa walimu wao kuhudhuria mkutano huo bila kukosa.

  Walimu hao, walisema baada ya kupewa tangazo na walimu wao wakuu walihoji na kuambiwa kuwa ni agizo kutoka kwa waratibu wa elimu.

  Mbali ya walimu, agizo hilo limewalenga wanafunzi wa darasa la tano na la sita kwa baadhi ya shule kutokana na wanafunzi wa darasa la saba kuhitimu shule wiki chache zilizopita.

  Baada ya kupata habari hizo, Tanzania Daima ilitembelea baadhi ya shule na kuzungumza na walimu na baadhi ya wanafunzi ambao walikiri kuwepo kwa hali hiyo, huku wengine wakidai hawajaelewa wanakwenda kufanya nini kwenye kampeni hizo.

  Kwa upande wa wanafunzi waliozungumza na Tanzania Daima katika shule za Makole, Medeli na Nkuhungu, walisema wametangaziwa na walimu kuwa wafike nje ya Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma majira ya saa 8 siku ya Jumapili bila kukosa.


   
 2. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #2
  Oct 2, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,356
  Likes Received: 3,122
  Trophy Points: 280
  Waalimu tena!............wakipewa epa wanasahau kila kitu na baada ya mwezi mmoja tu malalamiko kibao
   
 3. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #3
  Oct 2, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Walimu wako kweny kundi linaloathirika na mishahara kiduchu ni vema wakachukua maamuzi mazito kuipiga chini CCM kwanza wao ndiyo wanakuwa wasimamizi wasaidizi.Wabaki na lao moyoni la kumpa DR.Slaa
   
 4. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #4
  Oct 2, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280
  Kaka nakijana ansoma CITY SECONDAY yupo form One, naye nimeongea naye ansema wameambiwa wasikose kuja.
  Mmiliki wa shule hii ni mgombea ubunge wa dodoma mjini, wakati wa kura za maoni, aliwapa kadi za ccm wanafunzi washule yake wakaenda kumpigia kura, akaibuka mshindi.
   
 5. e

  emalau JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 272
  Trophy Points: 180
  Ha ha ha ha, unaweza kumlazimisha punda kwenda mtoni lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji
   
 6. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #6
  Oct 2, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tarime juu. Wanatarime katika ile video iliyowekwa katika JF wametoa ujumbe mzuri " mkipewa vitu na ccm, pokeeni lakini mnajua cha kufanya siku ya uchaguzi, Chagua CHADEMA". TARIME JUU
   
Loading...