Walimu wanafunzi wagomea posho ya Sh 500 kwa siku | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walimu wanafunzi wagomea posho ya Sh 500 kwa siku

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Feb 15, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Wanafunzi hao wameazimia kugoma kutokana na uongozi wa chuo hicho kutaka kuwapa Sh 500 kwa siku ikiwa ni posho ya mazoezi ya vitendo nje ya chuoni hapo.

  Wameutaka uongozi wa chuo hicho wakae na wapange upya na wao wakiwa wanataka wapewe japo Sh 5000 kwa siku na sio hiyo iliyopangwa awali.

  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Meja Jenerali Said Kilembo aliwataka wanafunzi hao kuachana na mgomo huo kwani hautawasaidiaa chochote katika kozi yao hiyo.

  Pia alimtaka mkuu wa chuo hicho kusikiliza maombi ya wanafunzi hao kwa kupeleka ombi hilo Serikali ya Mkoa na kuweza kutatuliwa na wanafunzi hao waweze kuongezewa posho hiyo kwani iliyopangwa awali ni kama uzalilishaji kwa wanafunzi hao.

  Alisema anaamini fedha hizo zipo na kinachotakiwa kujipanga na kupeleka fedha hizo serikali ya Mkoa na ikishindikana lipelekwe Serikali Kuu ili fedha hizo kuongezwa na w anafunzi hao waaanze mara moja mazoezi hayo ya vitendo nje ya Chuo.

  Wanafunzi hao wamesema kutokana na gharama za nauli na gharama nyingine za kujikimu kwa siku kiasi hicho kilichopangwa haitawezekana hata kidogo na wameomba kama fungu hilo halipo basi wasifanye mazoezi hayo kabisa na maksi zilizotakiwa kujazwa kwa ajili ya mazoezi hayo kipengele hicho kiondolewe.
   
 2. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  sh. 500/- kwa siku? utanunua nini????

  kweli ualimu ni wito!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  halafu mtashangaa elimu kushuka na kasi ya maambukizi ya ukimwi kuongezeka miongoni mwa vijana??au utovu wa maadili ya kazi ya ualimu kama kuuza mitihani, vtwisheni vinavyoishia kujifariji kwa kupachika mimba visichana vya shule!!!!!!!!!!!! sasa serikali iwe serius jamani......................

  angalizo:
  kalembo yuko tanza sasa hivi, morogoro yuko isa machibya kama sikosei......
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...