Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,809
- 34,193
Walimu wamelalamika kuhusu "Saa za chabo" zinazouzwa kwenye mitandao zinazowasaidia wanafunzi kuibia kwenye mitihani. Saa hizi za kidijitali, zina "kitufe
cha dharura" ambacho ukibonyeza haraka kinaondoa maandishi na kurejesha saa. Saa hizi zinaweza kuhifadhi taarifa katika mifumo mbalimbali ikiwemo maandishi
ambayo yanaweza kutumiwa kwenye mitihani. Msomi mmoja kutoka Bath ameonya kuhusu "soko hili la kificho" ambalo linaweza kuwashawishi wanafunzi kuibia kwenye
mitihani. Saa hizo zinazonadiwa kwenye tovuti ya Amazon, inadai zimetengenezwa mahsusi kwa ajili ya "kuibia kwenye mitihani". Aina moja ya saa hizo yenye uwezo
wa kuhifadhi 4GB kwa maandishi au picha, inaahidi kukupa uwezo wa kusoma kupitia skirini yake. Na mtu anapobofya kitufe cha dharura, kila kitu kinaacha kufanya kazi mara moja na skrini ghafla inaonesha majira. Saa hiyo inayodaiwa "kurahisisha
kusoma" pia inanadiwa pamoja na kifaa kingine unachobandika sikioni cha kukupa sauti, bila hata kuhitaji waya - wireless.
Soma zaidi: 'Cheating watches' warning for exams - BBC News