Walimu Wakuu wavuliwa vyeo udanganyifu matokeo darasa la saba

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
WALIMU WAKUU watano wa shule za msingi Manispaa ya Temeke jijini wamevuliwa vyeo vyao kwa kosa la kubainika kufanya udanganyifu katika mitihani ya darasa la saba iliyofanywa mwaka jana nchini kote.
Mitihani ilizua migogoro kufuatia kufanana wka matokeo na kuchaguliwa wasiokuwa na sifa wasiojua kusoma wala kuandika kuipita mitihani hiyo hali iliyolazimika Wizara ya elimu kuandaa mitihani ya majaribio kwa wanafunzi hao

Wizara ya elimu iliandaa mitihani ya majaribio kubaini wasiojua kusoma wala kuandika na kutoa ahadi kwa watakaobainika kufanya udanganyifu wa aina yeyote kupitisha wanafunzi hao kuwawajibisha

Afisa Elimu wa Manispaa ya Temeke, Honorina Mumba, aliiambia nifahamishe kuwa tayari walimu hao wameshavuliwa vyeo vyao na kuwa walimu wa kawaida katika shule zingine.

Alitaja walimu waliovuliwa vyeo hivyo walitoka katika shule ikiwemo Keko Magurumbasi, Taifa, Unubini Bokorani na Mgulani.

Awali Wizara ya Elimu ilitangaza kuwafutia matokeo jumla ya wanafunzi 458 katika shule za msingi za serikali

Hata hivyo Wizara ya elimu bado inaendelea na uchunguzi kubaini wale wote waliohusika kufanya udanganyifu katika mitihani hiyo

Walimu Wakuu wavuliwa vyeo udanganyifu matokeo darasa la saba
 
Back
Top Bottom