Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
Kwa ufupi
Wilaya hiyo ni kati ya wilaya ambazo zimekuwa zikishikilia mkia katika matokeo mbalimbali ya mitihani, jambo lililosababisha mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali kuungana na Serikali kuwekeza nguvu katika kupambana na changamoto zinazokwamisha elimu.
By Tumaini Msowoya, Mwananchi
Walimu wakuu 26 wa shule za msingi katika Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara wamevuliwa vyeo baada ya uchunguzi uliofanywa na wilaya hiyo kubaini wameshindwa kutimiza wajibu wao kikamilifu ikiwamo kusimamia elimu.
Wilaya hiyo ni kati ya wilaya ambazo zimekuwa zikishikilia mkia katika matokeo mbalimbali ya mitihani, jambo lililosababisha mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali kuungana na Serikali kuwekeza nguvu katika kupambana na changamoto zinazokwamisha elimu.
Akizungumza leo wakati ufunguzi wa wiki ya maadhimisho ya elimu, yaliyofanyika wilayani humo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Adam Dambaya amesema uchunguzi wa kina umeonyesha bila kuacha shaka kwamba walimu wakuu hao wameshindwa kutimiza wajibu wao kikamilifu.