Walimu wakimbia shule kwa kubakwa na wanafunzi

Bramo

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
13,160
10,001
Mmoja wa walimu hao ambaye hakutaka kutajwa gazetini akihofia kushughulikiwa na wanafunzi hao alisema amelazimika kuikimbia pamoja na walimu wenzake wote, kwa kuwa wameshindwa kudhibiti tabia hiyo kutokana na vijana hao kuungwa mkono na wazazi wao.

WALIMU wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Ruaruke wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani, wameitelekeza shule hiyo kutokana na kukithiri kwa vitendo vya baadhi ya wanafunzi kuwadhalilisha kimapenzi, ikiwamo kuwabaka baadhi yao.
Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa mbali na udhalilishaji huo, wanafunzi hao wamekuwa wakiwatishia maisha walimu wao kwa namna mbalimbali. Katika moja ya vitisho hivyo, wamechoma moto nyumba zao tatu.Habari hizo zimeeleza kwamba walimu hao wamelazimika kuikimbia shule hiyo baada ya baadhi ya walimu wa kike kutongozwa na wanafunzi, kupigwa mabusu kwa nguvu hadharani, kutishiwa kuchomwa visu na kuchorwa vikatuni vya kudhalilisha.

Source Mwananchi 12/06/2012

My Take.
Hii ni Laana ya CCM na Serikali yake
 
Haya mambo yanafanyika nchi gani? Chama gani kinatawala? Viongozi wa chama hicho wanashughulika na nini zaidi ya wanachi kama hawa walimu?
 
Nyie wapumbavu sana mnaoangalia kila kitu tatzo ni chama fulan, hilo nalo kweli linauhusiano na chama. Mambo mengine muwekage pembeni tofauti zenu za vyama.
 
ni sera ya chama chetu cha magamba.. kuua, kubaka na mengineyo maovu...
 
Ndio maana huo mkoa umebaki nyuma kimaendeleo kama mwanafunzi anamfanyia mwalimu ujinga mzazi anachekelea ni haki yake kupata ziro.Kuna mbunge wa mkoa huo aliwahi kusema maendeleo yao yaliporwa na watu wa kaskazini kumbe hawayatafuti wanashabikia ujinga wa watoto wao
 
Mwisho wa Kidato cha Nne hawa hawa wataanza kumlaumu Dr. Joyce Ndalichako kwamba anawapendelea baadhi ya watahiniwa. Kitendo cha kutaka ndoa kwa nguvu tena kwa waalimu wao ni UTOVU WA NIDHAMU.
 
hao walimu waliokimbia shule kwa kubakwa na wanafunzi wachunguzeni akili zao kama ziko sawa, kwani mwanafunzi kumbaka mwalimu wake si jambo la kawaida hiyo inawezekana kama mwalimu alikuwa anamfundisha mtoto mapenzi
 
Sina cha kushangaa hapo, mkoa wa PWANI. Ingekuwa Kaskazini ningeshangaa, huko binadamu wanaelewa shule maana yake nini
 
Nyie wapumbavu sana mnaoangalia kila kitu tatzo ni chama fulan, hilo nalo kweli linauhusiano na chama. Mambo mengine muwekage pembeni tofauti zenu za vyama.

Ok, nani aingilie kati kama si Serikali, na hapa Tanzania unaweza ukataja hili li serikali bila kutaja CCM.
Pwambaf
 
Nyie wapumbavu sana mnaoangalia kila kitu tatzo ni chama fulan, hilo nalo kweli linauhusiano na chama. Mambo mengine muwekage pembeni tofauti zenu za vyama.
Another Mulugu
 
Mfumo kristo ha ha ha ha.Dr Ndalichako anatuonea sana lazima tumg'oe.
 
WALIMU wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Ruaruke wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani, wameitelekeza shule hiyo kutokana na kukithiri kwa vitendo vya baadhi ya wanafunzi kuwadhalilisha kimapenzi, ikiwamo kuwabaka baadhi yao.
Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa mbali na udhalilishaji huo, wanafunzi hao wamekuwa wakiwatishia maisha walimu wao kwa namna mbalimbali. Katika moja ya vitisho hivyo, wamechoma moto nyumba zao tatu.Habari hizo zimeeleza kwamba walimu hao wamelazimika kuikimbia shule hiyo baada ya baadhi ya walimu wa kike kutongozwa na wanafunzi, kupigwa mabusu kwa nguvu hadharani, kutishiwa kuchomwa visu na kuchorwa vikatuni vya kudhalilisha.

Source Mwananchi 12/06/2012

My Take.
Hii ni Laana ya CCM na Serikali yake

Mijitu mingine bwana hovyo kabisa!!!!! Mada umeianza vizuri lakini umeimalizi vibaya. Kwani hao wanafunzi wanaowabaka waalimu ni wanachama wa CCM???? We vipi??? Au umelewa? Kama laana ni ya serikali nakuuliza swali moja. Kati ya waalimu na wanafunzi nani ni part ya serikali? Yaani nani anaonekana kuwa anaiwakilisha serikali?
 
badae hawa waislam wataanza kulalamikia mfumo kristo... Upuuzi kama huu huwezi kuusikia kwenye mikoa ya watu wenye akili na wapenda shule
 
Au wanalipiza visasi kiaina baada ya dada zao kwa miaka mingi kupigwa mimba na walimu dume?au pengine wanawatega maana viwalimu vya sasa vimewapita wa enzi zetu!
 
hao walimu waliokimbia shule kwa kubakwa na wanafunzi wachunguzeni akili zao kama ziko sawa, kwani mwanafunzi kumbaka mwalimu wake si jambo la kawaida hiyo inawezekana kama mwalimu alikuwa anamfundisha mtoto mapenzi

Naomba kukuuuliza maswali kadhaa:
je una dada au mama?;
- je una ndugu, hususani wa kike, anayeishi vijijini kabisa?
- je umewahi kusikia madhara ya kubakwa (madhara ya kimwili na kisaikolojia)?;
- je unahisi madhara ya kudhalilishwa na mtoto au mdogo wako kijinsia?
"WAALIMU TUNA HALI NGUMU, JAPO TUNA UMUHIMU".
Sijutii kwa kusomea Ualimu, ila nasikitika kwa kuwa jamii haithamini nafasi ya Mwalimu katika kujenga mustakabali wa taifa.
 
Maeneo haya kuwapelekea walimu na shule ni kuwakosea haki zao za msingi. Huko wangewapelekea maduka ya dawa za asili na .......... lakini sio shule.

Uliotamalaki huko ni ushirikina na maisha ya hovyo hovyo.
 
Mkuu mi nimefanya kazi rufiji mwaka 2008 hadi 2009. Idadi ya Madrasatul inazidi idadi ya shule za msingi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom