Walimu wajifunze karate na kungfu,bure ghali!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Katika kutekeleza mpango wa kusafiri bure uliobuniwa na DC Makonda wa Kinondoni,walimu wanapaswa kujifunza na kufuzu karate na kungfu,kiufupi,martial arts.

Wenzao JWTZ wamesaidiwa na mapigo yao. Wamewazima madereva na makondakta. Wamejiokoa toka udhalilishaji,unyanyasaji na kadhalika. Walimu nao wajiandae na hayo. Wakijua martial arts,mambo yatakwenda sawia.

Kuwasaidia walimu si kuwasafirisha bure kwa saa zilizopangwa. Kuwasaidia ni ima kuwanunulia magari yao au kuwapa posho za nauli kila mwezi. Amasivyo,ni martial arts ndizo zitakazolinda hadhi zao!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Ila ninyi CHADEMA mnazidi kwa kubeza. Yaani kila jambo jema kwenu mnachukulia masihara tu. Nimemsikia mwenyekiti wenu Mbowe akiwatetea wanaotumbuliwa majipu
 
Nampongeza Dc Makonda kwa kuwapa kipaumbele walimu. Kwa kitendo hiki sina shaka Dc Makonda anatambua umuhimu wa elimu kwa maendeleo ya taifa letu. Kongole Dc Makonda.

Sikubaliani na wazo la kuwanunulia magari yao walimu. Kwa vile yatakuwa ni magari ya umma uendeshaji wake utakuwa wa gharama.

Njia bora kabisa ya wazo hili ni kuwapa posho ya nauli kila mwezi kwa ajili ya nauli. Hii itawapa motisha walimu na tija itaonekana.
 
Katika kutekeleza mpango wa kusafiri bure uliobuniwa na DC Makonda wa Kinondoni,walimu wanapaswa kujifunza na kufuzu karate na kungfu,kiufupi,martial arts.

Wenzao JWTZ wamesaidiwa na mapigo yao. Wamewazima madereva na makondakta. Wamejiokoa toka udhalilishaji,unyanyasaji na kadhalika. Walimu nao wajiandae na hayo. Wakijua martial arts,mambo yatakwenda sawia.

Kuwasaidia walimu si kuwasafirisha bure kwa saa zilizopangwa. Kuwasaidia ni ima kuwanunulia magari yao au kuwapa posho za nauli kila mwezi. Amasivyo,ni martial arts ndizo zitakazolinda hadhi zao!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
na maneno

yan watanyanyaswa adi bas wajipange makonda asubil mrejesho to
 
Back
Top Bottom