Walimu waijia juu Serikali, wasema Kikokotoo bado kipo kinasubiri kuwaliza watumishi

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Chama cha kutetea haki na maslahi ya walimu Tanzania CHAKAMWATA kimelia kilio cha uchungu mkubwa sana kwamba kuna uonevu mkubwa sana unaofanywa na serikali ya awamu ya 5.

Kimedai kwamba serikali iliwadanganya kusitishwa KIKOKOTOO na FAO LA KUJITOA. Kwamba hivi vitu bado vipo na vinasubiri muda kuanza kutumika. Haya ni majibu waliyopewa na Waziri Jenister Muhagama na katibu mkuu wake wa wizara.

Walimu mliopigiwa simu kupitia kwa Waziri Jenister mkaambiwa kua mnapendwa mkafurahi jipimeni na fikirieni maisha na familia zenu.
 
Attachments

  • VID-20201019-WA0016.mp4
    19.2 MB
  • VID-20201019-WA0015.mp4
    18.3 MB
Absolutely, Mh Rais amefilisi mifuko ya hifadhi jamii na kuisababishia ukata.

Hiki ndicho chanzo cha kupunguza kiasi cha fedha kinacholipwa kwa mkupuo ili kuipa nafuu serikali ili wasilipe kiasi kingi cha deni kwa mkupuo

Hii 25% ni ya Magufuli bila kupepesa macho.

Wastaafu walimu wanalia
Wakati wastaafu marais wanajengewa makasri.

Watumishi ninyi ndio wa kutetea maslahi ya kesho ya watoto wenu

Ni lazima muungane kwa hili
Mpinge dhulma hii.

Walimu, maaskari, madaktari ni wanyonge zaidi wakiwa na malipo duni wasioweza kujenga hata nyumba za kuishi.

Wao marais na mawaziri ambao mshahara mmoja au miwili tu anajenga nyumba, nyumba kwao za nini?
 
Kikokotoo hakiwezi kuwa na faida kwa wastaafu kwa kuwa fedha wanazokatwa kwa ajili ya mafao yao huchukuliwa na serikali badala ya kuwekezwa ktk kuboresha maslahi ya wafanyakazi. Ndio maana wanacholipwa ni kidogo sana.

Hivyohivyo kwa bima ya afya fedha nazo hubebwa na serikali na sasa ndio maana wameondoa matibabu ya magonjwa mengi na wameacha malaria tu.
 
FAO LA KUJITOA liliondolewa na CCM ...

Maelfu ya wanyonge sekta binafsi Wana hasira na NSSF

CCM walipitisha FAO la kukosa ajira, mkataba ikiisha, yanalipwa 33% ya mshahara kwa miezi 6 ...na sio akiba yako yote

Je, Kwa akili za maccm, afya... hospital utalipa 33%...Je ...Kodi ya Nyumba utalipa 33%?

Magufuli rudisha Fao la kujitoa kwa wanyonge.
 
Serikali ya kinyama hii
Chama cha kutetea haki na maslahi ya walimu Tanzania CHAKAMWATA kimelia kilio cha uchungu mkubwa sana kwamba kuna uonevu mkubwa sana unaofanywa na serikali ya awamu ya 5.

Kimedai kwamba serikali iliwadanganya kusitishwa KIKOKOTOO na FAO LA KUJITOA. Kwamba hivi vitu bado vipo na vinasubiri muda kuanza kutumika. Haya ni majibu waliyopewa na Waziri Jenister Muhagama na katibu mkuu wake wa wizara.

Walimu mliopigiwa simu kupitia kwa Waziri Jenister mkaambiwa kua mnapendwa mkafurahi jipimeni na fikirieni maisha na familia zenu.
 
Chama cha kutetea haki na maslahi ya walimu Tanzania CHAKAMWATA kimelia kilio cha uchungu mkubwa sana kwamba kuna uonevu mkubwa sana unaofanywa na serikali ya awamu ya 5.

Kimedai kwamba serikali iliwadanganya kusitishwa KIKOKOTOO na FAO LA KUJITOA. Kwamba hivi vitu bado vipo na vinasubiri muda kuanza kutumika. Haya ni majibu waliyopewa na Waziri Jenister Muhagama na katibu mkuu wake wa wizara.

Walimu mliopigiwa simu kupitia kwa Waziri Jenister mkaambiwa kua mnapendwa mkafurahi jipimeni na fikirieni maisha na familia zenu.
Tuwe tunatenda haki kwa Mhe. Rais Dr. JPJM kwa namna alivyolishughulikia suala la kikokotoo. Unaposema Kikokotoo bado kipo unamaanisha nini wakati Walimu (Waliokuwa PSPF) wanaendelea kulipwa kwa Kikokotoo cha 1/540 Accrued Factor, 15.5 Reducing Factor na Mkupuo wa 50% kama ilivyokuwa hapo awali. Kikokotoo cha 1/580, 12.5 & 25% kilipigwa stop hadi 2023 na Wafanyakazi tunafahamu Serikali imeshaanza mazungumzo na Wadau ili kupata kikokotoo kitakachokidhi haja za pande zote (Mifuko na Wanachama).

Ni vyema mabaya tuyaseme lakini yanapofanyika mazuri pia tuyaseme. Lazima Kikokotoo kipya kitengenezwe kitakachojali Uhai wa Mifuko na wakati huo huo kiwapatie wastaafu mafao yatakayowapatia maisha yenye staha wakiwa nje ya ajira. Walimu waendelee kuwasiliana na CWT ambayo ipo ndani ya TUCTA waweze kujua ukweli wa jambo hili na kuepuka uchichezi usio wa lazima baina ya Walimu na Mhe. Rais.
 
Huu uwongo wa Chadema mwisho wao ni October
hahahaha pa kuponea hampaoni ..na sio waalimu tu..wapo wengi wana uchungu mkali sana na uchungu wao watauonesha oktoba 28 kwa kumpigia kura Lissu kua rais wa Tanzania kwa miaka kumi mfululizo.
 
Tuwe tunatenda haki kwa Mhe. Rais Dr. JPJM kwa namna alivyolishughulikia suala la kikokotoo. Unaposema Kikokotoo bado kipo unamaanisha nini wakati Walimu (Waliokuwa PSPF) wanaendelea kulipwa kwa Kikokotoo cha 1/540 Accrued Factor, 15.5 Reducing Factor na Mkupuo wa 50% kama ilivyokuwa hapo awali. Kikokotoo cha 1/580, 12.5 & 25% kilipigwa stop hadi 2023 na Wafanyakazi tunafahamu Serikali imeshaanza mazungumzo na Wadau ili kupata kikokotoo kitakachokidhi haja za pande zote (Mifuko na Wanachama).

Ni vyema mabaya tuyaseme lakini yanapofanyika mazuri pia tuyaseme. Lazima Kikokotoo kipya kitengenezwe kitakachojali Uhai wa Mifuko na wakati huo huo kiwapatie wastaafu mafao yatakayowapatia maisha yenye staha wakiwa nje ya ajira. Walimu waendelee kuwasiliana na CWT ambayo ipo ndani ya TUCTA waweze kujua ukweli wa jambo hili na kuepuka uchichezi usio wa lazima baina ya Walimu na Mhe. Rais.
Umeongea kipovu sana kama kada mtiifu wa Lumumba lakini ndio hivyo la kuvunda halina ubani.

Si umemsikia mheshimiwa huko Bagamoyo mwenyewe anaongea kwa kukata tamaa kwamba mkichagua wale sijui watatupeleka wapi na wapi.
 
Back
Top Bottom