Walimu wafanyiwe haya kama motisha na fidia yao katika utumishi huu wa Miaka Mitano

fake ID

JF-Expert Member
May 19, 2014
375
500
Wakuu habari zenu,

Niwapongezeni kwa kuchagua Tanzania kuwa kijani kibichi, hakika sasa tutegemee maendeleo ya kasi ya 5G maana wale waliokuwa wanapinga maendeleo sasa hawapo tena! bila shaka sasa hakuna tena visingizio! mishahara kwa watumishi itapanda! madaraja watapanda pengine kuanzia mwezi huu, kila kitu kitakuwa bien!

Baada ya hizo salamu fupi sasa nirudi kwenye mada yangu, sina haja ya kukumbusha jinsi walimu wa Tanzania walichokipata kwa miaka hii mitano. Nikiwapa kongole wale walioajiriwa mwaka 2014 ambao wametimiza miaka SITA, ndio MIAKA SITA bila kupanda daraja, naam!

Kwa kuwa serikali yetu ni sikivu na iliahidi endapo itachaguliwa YENYEWE tu bila MCHANGANYO basi watu wategemee NEEMA ambayo haijawahi kuwepo tangu kuumbwa misingi ya dunia na kwakuwa watanzania ni WASIKIVU basi wakaitikia kwa KISHINDO na kuifanya nchi yetu kuwa KIJANI! Hivyo ni matumaini yangu sasa ushauri huu ufuatao utafanyiwa kazi mahususi kwa walimu wa tanzania.

1. Nyumba za Walimu: hili lipo ndani ya uwezo wa serikali yetu sikivu, naomba sana walimu hawa wajengewe nyumba zenye hadhi walau wale ambao wamepanga watoke kwenye adha ya KODI na hako kasalio wakatumie kwenye mambo mengine, sijui kama hili lipo kwenye ilani ila TUSIANGALIE ilani sana tutakwama!

2. Utaratibu wa walimu kwenda kazini walimu ubadilike: Mfano Mwalimu Y hana kipindi siku ya Jumanne, basi siku hiyo asiende kazini abaki nyumbani auze genge lake, ama Mwalimu X ana kipindi saa 1 asubuhi mpaka saa 3 asubuhi basi akimaliza kipindi chake aende shambani kwake kumalizia bustani yake! hapa kwanza mwalimu ataokoa nauli ambazo hazikuwa na ulazima.

3. Uhamisho: Walimu aruhusiwe kuhama kwenda anapotaka kama ya shule yake inaruhusu, vinginevyo akipata mwalimu wa kubadilishana nae basi ichukue muda mfupi tu zoezi likamlike kuliko ilivyo sasa Mwalimu anatumia miaka mitatu kwenye uhamisho hii sio haki.

4. Posho ya "chakula": suala hili linawezekana kabisa kila katikati ya mwezi (Mfano Tarehe 15) Walimu wapatiwe kiasi kidgo mfano laki 1 tu flat hii itawasaidia kupunguza makali ya maisha.

5. CWT: Sheria ibadilishwe haraka sana, Walimu waruhusiwe kujiunga na kukatwa kwa HIARI yao badala ya ilivyo sasa ambapo CWT WANAJISEVIA tu mshahahara wa Mwalimu halafu hawana wanachomsaidia mwalimu.

Hapa itungwe sheria Mwalimu mwenyewe akiona kuna ulazima wa kukatwa akatwe kwa hiari yake, sijawahi kuona faida ya chama cha Walimu Tanzania, jiulize tu hawa Walimu walioajiriwa mwaka 2014 mpaka leo hawajapanda daraja na CWT ipo hapo na pesa wanakata ndipo utaona hiki chama ni MZIGO mwingine kwa walimu.

Kwa leo tuishie hapo naamini sitakuta gari nje ya nyumba yangu linanisubiri. (nimetania tu)
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
6,089
2,000
Miss wa kugawana loot. Ngoja tuone Ile sehemu ya simba nani atachukua.

Usisahau pia kuwa majizi mengi hudakwa kwenye magawano.
 
GKado

JF-Expert Member
Oct 7, 2017
557
1,000
Naunga mkono hoja namba mbili MWALIMU ahudhurie vipindi vyake vikiisha akaende kuongeza kipato.
Siyo MWALIMU hata ukitaka kutoka nje ya shule kunywa chai aombe ruhusa kwa mkuu.​
 
sir_liar

Member
Oct 30, 2016
29
125
Kumbuka walimu ndo wasimamizi wa kura.

wacha wale matunda yao
We jamaa hebu jiongeze acha kukariri,inaonekana kwa ufinyu wa kushindwa kifikiri kwako wewe ni kosa mwalimu kusimamia kituo cha uchaguzi.
Jaribu kutofautisha kati ya kusimamia na kuchakachua kura ni mambo yanayofanywa na watu wawili tofauti.
 
Mtukutu wa Nyaigela

JF-Expert Member
Sep 4, 2018
3,063
2,000
We jamaa hebu jiongeze acha kukariri,inaonekana kwa ufinyu wa kushindwa kifikiri kwako wewe ni kosa mwalimu kusimamia kituo cha uchaguzi.
Jaribu kuto
fautisha kati ya kusimamia na kuchakachua kura ni mambo yanayofanywa na watu wawili tofauti.
kumbe
kula mtori nyama ziko chini
 
kson m

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
5,708
2,000
Wakuu habari zenu,

Niwapongezeni kwa kuchagua Tanzania kuwa kijani kibichi, hakika sasa tutegemee maendeleo ya kasi ya 5G maana wale waliokuwa wanapinga maendeleo sasa hawapo tena! bila shaka sasa hakuna tena visingizio! mishahara kwa watumishi itapanda! madaraja watapanda pengine kuanzia mwezi huu, kila kitu kitakuwa bien!

Baada ya hizo salamu fupi sasa nirudi kwenye mada yangu, sina haja ya kukumbusha jinsi walimu wa Tanzania walichokipata kwa miaka hii mitano. Nikiwapa kongole wale walioajiriwa mwaka 2014 ambao wametimiza miaka SITA, ndio MIAKA SITA bila kupanda daraja, naam!

Kwa kuwa serikali yetu ni sikivu na iliahidi endapo itachaguliwa YENYEWE tu bila MCHANGANYO basi watu wategemee NEEMA ambayo haijawahi kuwepo tangu kuumbwa misingi ya dunia na kwakuwa watanzania ni WASIKIVU basi wakaitikia kwa KISHINDO na kuifanya nchi yetu kuwa KIJANI! Hivyo ni matumaini yangu sasa ushauri huu ufuatao utafanyiwa kazi mahususi kwa walimu wa tanzania.

1. Nyumba za Walimu: hili lipo ndani ya uwezo wa serikali yetu sikivu, naomba sana walimu hawa wajengewe nyumba zenye hadhi walau wale ambao wamepanga watoke kwenye adha ya KODI na hako kasalio wakatumie kwenye mambo mengine, sijui kama hili lipo kwenye ilani ila TUSIANGALIE ilani sana tutakwama!

2. Utaratibu wa walimu kwenda kazini walimu ubadilike: Mfano Mwalimu Y hana kipindi siku ya Jumanne, basi siku hiyo asiende kazini abaki nyumbani auze genge lake, ama Mwalimu X ana kipindi saa 1 asubuhi mpaka saa 3 asubuhi basi akimaliza kipindi chake aende shambani kwake kumalizia bustani yake! hapa kwanza mwalimu ataokoa nauli ambazo hazikuwa na ulazima.

3. Uhamisho: Walimu aruhusiwe kuhama kwenda anapotaka kama ya shule yake inaruhusu, vinginevyo akipata mwalimu wa kubadilishana nae basi ichukue muda mfupi tu zoezi likamlike kuliko ilivyo sasa Mwalimu anatumia miaka mitatu kwenye uhamisho hii sio haki.

4. Posho ya "chakula": suala hili linawezekana kabisa kila katikati ya mwezi (Mfano Tarehe 15) Walimu wapatiwe kiasi kidgo mfano laki 1 tu flat hii itawasaidia kupunguza makali ya maisha.

5. CWT: Sheria ibadilishwe haraka sana, Walimu waruhusiwe kujiunga na kukatwa kwa HIARI yao badala ya ilivyo sasa ambapo CWT WANAJISEVIA tu mshahahara wa Mwalimu halafu hawana wanachomsaidia mwalimu.

Hapa itungwe sheria Mwalimu mwenyewe akiona kuna ulazima wa kukatwa akatwe kwa hiari yake, sijawahi kuona faida ya chama cha Walimu Tanzania, jiulize tu hawa Walimu walioajiriwa mwaka 2014 mpaka leo hawajapanda daraja na CWT ipo hapo na pesa wanakata ndipo utaona hiki chama ni MZIGO mwingine kwa walimu.

Kwa leo tuishie hapo naamini sitakuta gari nje ya nyumba yangu linanisubiri. (nimetania tu)
Nami nimeliona.CWT ni mzigo na kero kwa walimu.ni lijambazi lingine linalowaibia walimu likijificha nyuma ya kiitwacho vyama vya wafanyakazi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom